PreGE2025 Richard Mabala ataka Makalla atoe uthibitisho kuhusu kauli yake ya Ebola au achukuliwe hatua kwa kusema uongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hamna kitu huyo jamaa
 
Huyu CPA amefikiria angalau kwamba hii kauli yake inaweza kufanya hata watalii wakaogopa kuja Tanzania? Au Royal Tour ni bullet proof kwamba hata tukiwa na Ebola na M-pox za kupandikiza watalii watakuja tu.

This is beyond pathetic! 🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 
Ni kweli achukuliwe hatua za kisheria maana kauli yake imeleta hofu kwa raia!
 
Wanasiasa bado hawataki kubadilika kutokana na mageuzi ya elimu na sayansi. Sasa alilosema makala ni aibu Kwa CCM. Wakati huu sio wakusema uongo.
 
Yaani hajatumia akili kabisaaaaa! Ninawasiwasi na CPA yake, Wenda niyamchongo. Kauli yake itahalibu uchumi wa nchi.
 
Hivi Makala Kwa kabila lako ni nini?Mimi Kwa kabila langu ni mkaa🤣🤣
 
Nilifikiri Amos Makalla ana akili, hili limemshushia sana hadhi kama mtu mwenye intergrity.
 
Mamlaka ya uteuzi ndiyo yenye shida, kuna watu wawili wanahatarisha hii nchi
  1. Makala
  2. Chalamila
 
Mabala anataka kufutiwa uraia? Hafahamu ukiwa ccm uko juu ya sheria, hasa unachokisema kiwe ni kwa ajili ya kuchafua haiba ya wapinzani hususani cdm?
 
Kabisa kauli nzito sana. Athibitishe kama hana ushahidi apewe kesi ya kuzua taaruki.
Hiyo sheria ilitungwa kwa ajili ya wapinzani. Ccm wana kinga ya sheria walizozitunga.
 
Makala alete ushahidi laa sivyo apandishwe kizimbani.
 
Makala aitaje maabara inayouza wadudu wanaoambukiza m-pox na ebola na bei yake kwani anajua kila kitu. Akishindwa aburuzwe mahakamani.
Hii kauli ikiachwa bila uthibitisho itaharibu uchumi wa nchi kwani wawekezqji, watalii na wafanyabiashara toka nje ya nchi watasita kuja nchini kwa hofu ya kuambukizwa!
Kwa upande mwingine ni kuwa ccm imekabwa koo na mabadiliko ya Sheria za uchaguzi na ili hivyo wanajipanga kusambaza wadudu hao ili uchaguzi uahirishwe na kuwasingizia cdm. Watanganyika siyo wajinga Tena, Makala atambue!
Ccm mnaua uchumi wa nchi ili muendelee kuwatawala maskini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…