PreGE2025 Richard Mabala ataka Makalla atoe uthibitisho kuhusu kauli yake ya Ebola au achukuliwe hatua kwa kusema uongo

PreGE2025 Richard Mabala ataka Makalla atoe uthibitisho kuhusu kauli yake ya Ebola au achukuliwe hatua kwa kusema uongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwanasheria msomi JEBRA KAMBOLE anaenda kufungua kesi...hii kauli inahatarisha sio usalama Bali hata utalii utakufa
Anafungua kesi ya Nini!?..huo so ndiyo uhuru wenyewe ambao hata chadema huropoka hovyo dhidi ya watu
 
Analeta propaganda ambazo hazina afya kwa mustakabali wa nchi ,ndiyo yale yale ya mahita kuhusu CUF kuleta kontena la silaha...

Mpaka hao CDM walete virusi ina maana nchi yetu haina ulinzi?
 
Ile lugha ya huyu mtu Makala ni lugha ya hovyo na ya kudharau mno!
Nahisi tuwapime hawa watu kwa misemo hayo ili kuwaondoa kabisa kuongea mbele za watu kwani inaonekana
"ukomo wao wa busara umefikia tamati".
 
Mwandishi mkongwe wa vitabu ikiwemo kitabu cha "Mabala the farmer" kupitia ukurasa wake wa X amemtaka Amos Makalla atoe uthibitisho kuhusu kauli yake ya Ebola na M-Pox au achukuliwe hatua kwa kusema uongo,

ameandika;

"Kauli hii ni zito na haitaki kupuuzwa.Ama athibitishe kauli hii ama achukuliwe hatua kwa kusababisha taharuki kwa wananchi kwa kusema uongo."

View attachment 3281015
Soma: Pre GE2025 - Makalla: CHADEMA wanataka kuingiza Ebola Tanzania ili wazuie uchaguzi!
CCM na wanachama wake wamefilisika kiakili

Yaani Mtanzania aende sijui wapi zinakonunuliwa virusi vya Ebola na MPox kisha alete awapakaze ndugu zake kisa wanatofautina kiitikadi?!

Yafuatayo itakuwa suluhisho kutokana na mzaha alioufanya huyo Mluguru wa Kiegea

1. Waliothirika na kauli zake zisizo na uthibitisho ikiwa pamoja na CDM na Watanzania wamshaitaki mahakamani akathibishe madai yake hayo.
2. CCM wamwondoshe haraka huyu maana huko waendako wanaenda kutumbukia shimoni.
3. Tuhuma zilizotolewa chanzo chake inawezekana ni Peter Msigwa aliyenunuliwa kwa vipade thelathin vya shekeli
4. Lissu na CDM kwa ujumla vunjeni uhusiano na urafiki na Peter Msigwa maana ndiye mtia sumu kwa CDM pamoja na kujinasibu kwamba yeye na Lissu ni marafiki
 
Ni kama utani vile. Bila kusikiliza hiyo 'clip', ni vigumu sana kuamini kwamba kiongozi kama huyo anaweza kutamka, au hata kufikiri tu habari ya namna hiyo!
Hii ni dalili nzuri kwa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom