Muulize kwamba kwanini pamoja na hoja yake kwamba KYECU inanunua kwa bei nzuri lakini wakulima wanaamua kuuza kwa bei ya chini kwa walanguzi ?
Mimi pia natoka Kyela , naijua KYECU
Haya mambo ndiyo huwa yananipa taabu sana kuyaeleza watu wayaelewe vizuri, na nina wasiwasi (suspect) hata wewe huenda tusielewane juu ya hili, kutokana na maneno machache uliyotumia hapa.
Niulize: Je KYECU ni kweli wananunua kwa bei ya juu kuliko bei wanayolipa wafanya biashara, halafu bado wananchi wanaamua kuuza mazao yao kwa wafanya biashara? Hili linaingia akilini kweli?
Na kama bado hunielewi ni hivi: KYCU, bila shaka ina matatizo yake makubwa ndiyo maana wananchi hawaendi huko.
Na mimi nasema:
kwani ni lazima KYECU iwe na matatizo hayo?
Inakubalika kwamba ni jambo la kawaida KYCU kuwa na hayo matatizo?
Inategemewa na kukubalika na watu, na viongozi, kwamba KYECU inabidi iwe na matatizo hayo?
KYCU haitazamiwi kufanya kazi zake kwa ufanisi?
Hawa wafanya biashara binafsi hawana mchango wowote katika matatizo ya KYCU?
Kwa nini?
Ninaomba tu unielewe mkuu wangu Erythro, kwa haya ninayoyasema hapa, kwa sababu najua hii ni sehemu ambayo tunapishana (kidogo), lakini tunapishana kwa kuheshimiana. Na naomba ibaki hivyo hivyo.