Hiki ndicho kinachonizungusha akili nionekane kama hayawani wakati mwingine.
Chama cha Ushirika, kama KYECU ni ya serikali, au ninakusoma vibaya?
Hata hivyo, kiwe au isiwe ya serikali kwa kweli hakuna kinachobadilika, kwa sababu wote tunajua utendaji wao ni mbovu; na ndiyo maana, tokea huko nyuma hadi hapa tulipofikia, wimbo wetu maarufu ni kwamba :Serikali haiwezi kufanya biashara!
Lakini mbona serikali inafanya biashara na wafanya biashara wenyewe kila siku, na hakuna anayeuliza juu ya hilo?
Mkuu, Erythro, tuyaache haya, yapo nje ya uwezo wetu. Hata tuimbe vipi, hakuna kitakachobadilika. Wakulima wataendelea kunyongwa hivyo hivyo, na wafanya biashara wataendelea kuneemeka juu ya migongo ya hawa watu, kwa sababu serikali inayotakiwa kuwa kati kusimamia maslahi ya kila upande haina uwezo wa kufanya hivyo kwa utashi wake yenyewe.
Na hao wakulima wenyewe, hata hawaoni ushiriki wa serikali yao katika kuendeleza uduni wa maisha yao, kila mwaka!
Wafanya biashara, wanakwenda kukopa, ili wakanunue mazao ya wakulima kwa bei itakayowafaa wao; serikali inakwenda kukopa pia, lakini malengo yake ni mbali kabisa na kuwanufaisha wakulima.