Richmond case study: Je, Waziri Mkuu Majaliwa atavuka kikwazo cha Lowassa kwa ma-V 8 haya?

Nadhani haka ''kautamaduni'' ka ukiwa waziri mkuu basi usahau kuwa Rais wa JMT sio kazuri.
Kama taifa tutakuja kukosa kiongozi mzuri katika nafasi ya Urais, eti kwa sababu tu, aliponzwa na Uwaziri mkuu.

Nafikiri hoja hapa ni nani aliyeidhinisha ununuzi wa magari hayo. Naomba sana KM aendelee kuwa waziri mkuu. Sidhani kama alijua hayo maddy yaliyokuwa yanafanyika
 
Katika uongozi kila mtu huwa nawajibika kwa ngazi yake.Mambo yanapozama basi kunakuwa na Uwajibiji wa Jumla.Je swali la kununua hayo magari initiator ni nani?Vilitumika vigezo gani?Je utaratibu sahihi ulifuatwa?Mfano kama DED na halmashauri walifanya uamuzi wa kununua magari wakati mambo mengine yamekwama basi DED anapaswa kuwajibishwa.

Huo ni mtazamo wangu.Suala OWM kutoa ruhusa linategemea na justifications na utaratibu wa manunuzi ulivyo ila wa kuwajibishwa ni DED ambaye ndio atakayepanda hilo gari na mwenye maslahi nalo PERIOD.
 
Nafikiri hoja hapa ni nani aliyeidhinisha ununuzi wa magari hayo. Naomba sana KM aendelee kuwa waziri mkuu. Sidhani kama alijua hayo maddy yaliyokuwa yanafanyika
Sawa sasa kama amewabaini kwa nini asiwasimamishe mapema kupisha uchunguzi maana wako wengi ukimuacha yule wa kahama
 
Hahahah nimejikuta nacheka kwani mtu akiomba lazima apewe kwanini alipewa kama walijua ni makosa

Waliweka kuwa ofisi ya PM ipitishe walitaka kupunguza haya matatizo na kama bado yapo inakuwaje wasiwajibishwe
 
Hapa si swala la kufanyiwa zengwe. Ofisi ya Waziri Mkuu haiko makini katika utendaji kazi wake.
Swali dogo: una mke na familia ukatoa pesa ya matumizi na kutoa maelekezo kipi kinunuliwe katika hayo matumizi. Baada ya muda familia inakuomba kufanya manunuzi ya vitu ambavyo havimo kwenye maelekezo yako, fimilia ikanunua, unawezaje kuilamu familia kwa matumizi mabaya ya pesa. Waziri Mkuu anatakiwa ajiuzuru tu ameahindwa kusimamia ofisi yake. Lakini kingine cha kushangaza hiyo sheria kwa nini wakurugenzi wa halimashauri walio chini ya Tamisemi wakaombe kibali ofisi ya Waziri Mkuu badala ya wizara husika?
 
DED anahujumu uchumi utaombaje kitu ambacho unajua ni haramu kwako ? VXR unajua sio hadhi yako kuwa nayo ww ukaomba hili ni kosa, alie idhinisha unaweza kuta alipewa Document ambazo ziko general na vitu vingi akapitisha kumbe kuna mzoga ndani yake
 
Niliwahi ongea na gwiji la kisiasa miaka kadhaa nyuma.
Yeye aliniambia katika siasa za Tanzania kuna silaha inaitwa FITNA.
Akasema silaha hii hutumiwa kwa hadhari sana na huleta mafanikio yanayotarajiwa.

Mtu wamepigwa na silaha hii huwa wala huaelewi hata suala lenyewe lilivyoibuka.

Na ilitumiwa sana miaka ya Kikwete.
 
Zilikuwa mali ya CCM kwa matamshi ya Pole×2
... jengeni mifumo imara acheni kujenga personalities! Zile VX-R V8 T CCM 2020 zilizofunika nchi nzima kwa maelfu ziliidhinishwa na nani? Ni mali ya CCM? Zinafanya nini kwa sasa? Kama kuna kipindi ubadhirifu wa kutisha umewahi kufanyika nchi hii ...
 
Nadhani haka ''kautamaduni'' ka ukiwa waziri mkuu basi usahau kuwa Rais wa JMT sio kazuri.
Kama taifa tutakuja kukosa kiongozi mzuri katika nafasi ya Urais, eti kwa sababu tu, aliponzwa na Uwaziri mkuu.

Jiwe alimtishia Majaliwa siku anawaapisha mawaziri wake kuwa hata yeye kama PM nafasi yake haikuwa na guarantee ya miaka mitano!!! Hiyo ndipo staili ya utawala wa jiwe kutishia ili watu wamuogope na wafuate yale ayatakayo.

Jiwe akumbuke kuwa mtu akisha kuwa Waziri mkuu kwa muda fulani hata akiondolewa na kuwekwa mwingine kuna gharama fulani taifa lazima lizibebe mpaka kufa kwake!!! Hivyo Jiwe wakati wowote anapofikiria kumbadilisha waziri mkuu; ni lazima azitilie maanani gharama hizo kwa Taifa katika uamuzi wake na sio kukurupuka tu ili kumuweka mwingine ampendae!!
 
Jina linalipitishwa huko CCM kugombea urais ndiye rais.

Watanzania hatuna kumbukumbu.
 
... hayo mamigari ya 400m/- yaliyojaa kama utitiri huko serikali ya wanyonge utamuuzia nani? Hayanunuliki jombaa labda watanzania wachache mno na wenye uwezo huo wanaagiza brand new hawanunui used mengine yamewekewa matunguli na walioyatumia!
Na ukiyanunua jiandae na uchunguzi
 
Hivi shida ni kiasi cha hela kilichotumika au shida ni utaratibu uliotumika kupata hela ya kununulia hilo gari. Naona kuna watu watatutoa kwenye mjadala hapa..
 
Kiuhalisia hii ni aibu ka chama, na mtu wa kwanza kulaumiwa ni Msukuma amei expose serikali bila kujua kina mikono ya mabosi wake ipo ndani yake, alipaswa aongee na DeD KIKAO CHA NDANI, Matokeo yake amekwenda kuropoka mitandaoni amemtia waziri mkuu matatizoni na sijui atajisafisha vipi, mambo kama haya ni mengi mno yanatokea na ya kutisha zaidi sema watu hawasemi hazarani kwasababu itawaletea matatizo makubwa, mimi najua mbili tatu ambazo zikitangazwa au zikijulikana hata mkuu credibility yake itashuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…