Ridhiwani akagua ujenzi wa Hospitali Chalinze ambayo inazidi kumulikwa na Serikali. Wadau wamuunga mkono

Ridhiwani akagua ujenzi wa Hospitali Chalinze ambayo inazidi kumulikwa na Serikali. Wadau wamuunga mkono

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
RIDHIWANI AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI CHALINZE AMBAYO INAZIDI KUMULIKWA NA SERIKALI YA RAIS SAMIA. WADAU WAMUUNGA MKONO.

Jana Jumatano Julai 28, 2022 Mbunge wa Chalinze ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amekagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani ambapo pia amekabidhi gari la Kubebea Wagonjwa lililotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Mtwara Tanzania.

Gari hili ni mojawapo kati ya magari manne yanayotarajiwa kufika katika Halmashauri hiyo ya Chalinze ili kuimariaha upatikanaji wa huduma za afya wilayani hapo.

Hospitali ya Wilaya Chalinze, imepokea gari la Wagonjwa lililotolewa na Serikali ya Rais Samia na Mashine 3 za kuzalisha hewa ya Oxygen kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa wakipata shida ya upumuaji. Serikali ya Rais Samia imekwishatoa Shilingi Bilioni 2.1 hadi sasa kujenga miundombinu na vifaa tiba.

Pia Mhe. Ridhiwani amepokea msaada kutoka Taasisi ya Doris Mollel ambayo imechangia vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 12 kwa hospitali ya Wilaya Chalinze kusaidia watoto wachanga wenye shida ya kupumua ambapo kwa niaba ya Wana-Chalinze, Mhe. Ridhiwani amewashukuru sana ambapo Taasisi hiyo imeahidi kuendelea kusaidizana na mbunge kuimarisha hospitali hiyo.

FB_IMG_1659008691151.jpg
FB_IMG_1659008686687.jpg
FB_IMG_1659008682058.jpg
FB_IMG_1659008673552.jpg
FB_IMG_1659008669440.jpg
FB_IMG_1659008663035.jpg
 
Back
Top Bottom