Ridhiwani: Barua za Utumishi zijibiwe haraka kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kujibu kwa wakati barua za masuala ya kiutumishi ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima ambayo yamekuwa yakielekezwa katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa idara hiyo kilicholenga kufahamu majukumu yanayotekelezwa na kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Kikwete amewasisitiza watumishi wa idara hiyo ya Utawala wa Utumishi wa Umma kutosita kujibu barua za wadau kwa wakati hata kama zina mapungufu, ili wahusika wafahamu mapungufu yaliyopo kwenye masuala yao ya kiutumishi ambayo yamewasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kupata kibali au kutolewa maamuzi.

“Natambua kuna mapungufu ya masuala ya kiutumishi katika barua mnazolalamikiwa kutozijibu kwa wakati, lakini mnapaswa kuzijibu kwani msipofanya hivyo, mnatoa mwanya kwa wahusika kuilalamikia ofisi na hatimaye kuichafua taswira nzuri ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,” Mhe. Kiwete amefafanua.

Aidha, amewataka watumishi wa idara hiyo kuchakata utoaji wa vibali vya uhamisho wa watumishi wa umma kwa kuzingatia takwimu zinazoainishwa na Mfumo wa Tathmini ya Hali na Mgawanyo wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili vibali vya uhamisho vinavyotolewa visiathiri utendaji kazi wa baadhi ya taasisi katika eneo la utoaji huduma bora kwa wananchi.

Kuhusiana na utendaji kazi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kwa ujumla, Mhe. Kikwete amewapongeza watumishi wa idara hiyo kwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu licha ya kuwa ni mengi na yenye changamoto nyingi.

Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, watumishi wa idara hiyo wanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kutimiza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
 
Wafukuze wote walojihodhia mamlaka na kufanya bodi za taasisi na mashirika ya umma kushidwa kufanya majukumu yake ipasavyo.

awali bosi hizo zilikuwa zinawajibika kwa rais pekee au waziri na maamuzi mengi yaliishia ngazi za board hivyo kifanya mashirika ku perfom vizuri
 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kujibu kwa wakati barua za masuala ya kiutumishi ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima ambayo yamekuwa yakielekezwa katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa idara hiyo kilicholenga kufahamu majukumu yanayotekelezwa na kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Kikwete amewasisitiza watumishi wa idara hiyo ya Utawala wa Utumishi wa Umma kutosita kujibu barua za wadau kwa wakati hata kama zina mapungufu, ili wahusika wafahamu mapungufu yaliyopo kwenye masuala yao ya kiutumishi ambayo yamewasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kupata kibali au kutolewa maamuzi.

“Natambua kuna mapungufu ya masuala ya kiutumishi katika barua mnazolalamikiwa kutozijibu kwa wakati, lakini mnapaswa kuzijibu kwani msipofanya hivyo, mnatoa mwanya kwa wahusika kuilalamikia ofisi na hatimaye kuichafua taswira nzuri ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,” Mhe. Kiwete amefafanua.

Aidha, amewataka watumishi wa idara hiyo kuchakata utoaji wa vibali vya uhamisho wa watumishi wa umma kwa kuzingatia takwimu zinazoainishwa na Mfumo wa Tathmini ya Hali na Mgawanyo wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili vibali vya uhamisho vinavyotolewa visiathiri utendaji kazi wa baadhi ya taasisi katika eneo la utoaji huduma bora kwa wananchi.

Kuhusiana na utendaji kazi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kwa ujumla, Mhe. Kikwete amewapongeza watumishi wa idara hiyo kwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu licha ya kuwa ni mengi na yenye changamoto nyingi.

Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, watumishi wa idara hiyo wanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kutimiza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Utumishi kwelii kabisaa pale watu hawajali Mimi Toka mwaka 2020 barua yangu niliipeleka hawajajibu na Kila nikifatikia napewa Sasa barua ipo kwenye mchakato!daah wanaumiza sanaa
 
Back
Top Bottom