Ridhiwani Kikwete anaandaliwa Urais 2030?

Ridhiwani Kikwete anaandaliwa Urais 2030?

Wana JF, hizi taarifa nimezipata kwa mtu mkubwa sana ndani ya TISS na ambaye amewahi kuwa kigogo wa idara hiyo.

Ameniambia Mzee Jakaya Kikwete ndiye yuko nyuma ya Mpango huu na sehemu kubwa ya vigogo ndani na nje ya idara. Moja ya mkakati ulifanikiwa ni kuhakikisha baada ya sheria ilikuwa asomee Masters ya International Relation na kweli tayari amehitimu ili msije kusema haijui Dunia.

Lakini pili nimeambiwa Ulinzi wa Ridhiwan Kikwete ni tofauti na mawaziri wenzake wote. Tayari amezungukwa muda wote na suti nyeusi wawili muda wote kuhakikisha nyendo zake zinakuwa salama. Rais Samia Suluhu Hassan naye anaujua Mpango huu.

Hatua ya tatu ni kuwapoteza watu maboya kwa kumhusisha na kumtaja January Makamba kama mgombea Urais 2030 lakini nia ni Makamba kumficha asionekane lakini mwisho yeye January Makamba atakuja kuwa Waziri Mkuu wa Ridhiwan Kikwete. Nguvu nyingine ni kutoka kwa Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta naye anasaidia mpango kwa Hali na Mali.

Baadhi ya mawaziri wanaojua mpango huu ni pamoja na Jenister Mhagama na Hussein Bashe ambao tayari wameanza "kujisogeza" kwa dogo kwa matumaini ya baadaye.
Flying of ideas, jiangalie vyema huenda unaundergo uchizi, kistori chako cha kwenye toilet papers
 
Sio shida kwa Makamba wala Ridhwan kuwa marais, hakuna mahala katiba imekaza watoto wa viongozi au Marais kuwa viongozi.

Kinachotakiwa wafuate taratibu na raia wenyewe waridhie kuwachagua.
Inawezekana pia wazazi wao wamewandaa vijana wai kuwa viongozi.
 
Wazungu waliita afrika bara la Giza maanake watu wake wapo Kwenye Giza zito
Mbele huoni nyuma huoni
 
We unashangaa nini, CCM hata ikitaka tumbili iongoze hii nchi itaongoza, na wa Tanzania walivyo wanafiki watasema kwenye mitandao tumbili inaupiga mwingi imeleta maji na umeme, wengine watakuwa wanalalama kwa nini waongozwe na tumbili na si binadamu, malalamiko yataishia kwenye social medias na ku post vi memes baadae wanasahau.. Mi hata sishangai.

Yah right ..... WANATUONA NYANI!!
 
Kama ni Mtanzania na ana vigezo vya kuwa Rais acha awe Rais.
 
Huyo ni ngumu kuwa rais japo genge la wauza madawa ya kulevya wa dunia wanatamani sana wafanikishe jambo hilo la kumweka madarakani mtu wao maana anamikataba ya damu na wauza ngada wa dunia...wauza ngada wa dunia wanataka kutengeneza tena tanzania iwe heaven peace ya biashara ya madawa ya kulevya.
Majungu ndo mtaji wa Masikini
 
Tanzania siyo nchi ya kifalme.

Aidha, katika utafiti wangu binafsi niliofanya nimegundua kwamba watu wengi wa ukanda wa Pwani hawako serious kabisa kwenye suala la utendaji kazi hususani zile kazi za uongozi wa nchi na maendeleo yake. Wanachoweza wao ni mambo ya kiswahili-swahili, mipasho na blah blah nyingi za kisiasa. Completely, they are not serious.
Nyie wabara kuweni serious inatosha.
Mtuache sie tuwaongoze tu
 
Kumbe Mkapa aliondolewa na Magufuli?
Unakumbuka maneno ya busara ya Wazee wetu (Mwinyi na Kikwete)kule kwenye msiba wa Mkapa Lupaso kama ulikuwa unafuatilia.Na baada ya kuzika tu Rais haukuwa na uchungu wowote kwa Mkapa alianza kampeni ya tuliibiwa sana maeneo ya Kilwa,Lindi,Mkuranga huku akitafuna mahindi hadharani bila uchungu na kuzawadiwa jogoo mkubwa.
Baada ya hapo uliona uchaguzi Oktoba 2020 ulivyokuwa vyombo vya dola kila mahali utafikiri Sudan,hata DRC wanatushinda.Aliyekuwa kikwazo cha kujimwambafai kwa Magufuri alikuwa Mkapa,hivyo lilikuwa ni jambo la kimfumo ili Magufuri atekeleze malengo yake ya kutawala milele.Ukweli ndiyo huo.
 
kwa mahesabu ya kawaida haitawezekana.
Mama ni Muslim na yeye ni Muslim.kwa mfumo wa nchi hii Rais wa 2030 atakuwa Mkatoliki
 
Back
Top Bottom