Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, amejigamba kwa kudai kwamba yeye ndie pekee aliesababisha na kuchangia pakubwa Rais Dr. William Ruto akashinda uchaguzi wa 2022, la si hivyo bila jina lake kuwako kwenye karatasi za kupigia kura, kamwe asingeshinda urais wa Jamuhiri ya Kenya wakati huo.
Hata hivyo naibu wa Rais huyo wa Kenya, ana mlaumu, na kumtuhumu Rais William Ruto, kwa kupanga njama chafu dhidi yake, ikiwa ni pamoja na kuwafadhili wabunge kwa fedha, ili wambandue kwenye wadhifa wake.
"Acha kuwapa wabunge fedha za kunifukuza kazini, sitakubali jitihada zao. Wanataka nijiuzulu lakini sitaki". Alisema Gachagua kwa lugha yake ya asili.
Gachagua alimtaka Rais Ruto kuheshimu wapiga kura wa mlima Kenya, eneo ambalo anatoka, na kumsihi amuache ahudumu na amalize muhula wake kabla hajamchagua yeyote anaetaka kumchagua wakati wa azma yake ya kuchaguliwa tena 2027.
Hoja ya kumtimua Gachagua ofisini, iliwasilishwa bungeni mnamo Alhamisi Sept.26,2024 huku wabunge 242 wakiridhia na kuunga mkono hoja hiyo.
Tofauti za za kisiasa kati ya Naibu wa Rais huyo wa Kenya na bosi wake Dr.William Ruto ziliongezeka zaidi na kujidhihirisha bayana baada ya maandamano ya Gen z na hatua ya Ruto kumkatibisha hasimu wake wa kisiasa wa muda mrefu serikalini, Raila Odinga na hata kuwajumuisha baadhi ya wanachama wake kwenye baraza la mawaziri.
Gachagua anatuhumiwa kwa kuvunja sheria na katiba ya Kenya, matumizi mabaya ya ofisi, rushwa, ukabila, vitisho kwa watumishi wa umma na Boss wake pia, kugomea maamuzi ya baraza la mawaziri, kupinga sera na na mipango ya serikali na kutoa siri za baraza la mawaziri, kufadhili wahalifu ndani ya maandano ya gen z n.k.
Mpaka hapa unadhani tatizo linaweza kua ni katiba au ubinafsi wa kiongozi huyu mwenyewe?