Rigathi Gachagua adinda kujiuzulu, asema bila yeye Ruto asingeingia Ikulu

Rigathi Gachagua adinda kujiuzulu, asema bila yeye Ruto asingeingia Ikulu

Tatizo wanasiasa wa Kenya hawajui "kumalizana" kwa ndumba na ajali za barabarani. Wanategemea kanisa. Gachagua amkodi tu Faustine Mafwele akamalize hiyo kazi. Ruto atashushwa kwenye ndege mchana kweupe na kesho yake mwili utaokotwa kwenye mashamba ya miwa huko Siaya.
 
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Renson Ingonga ameidhinisha mashtaka dhidi ya watu watano kwa madai ya kupanga, kuhamasisha na kufadhili maandamano ya kupinga serikali yaliyoongozwa na vijana mwezi Juni.

Barua iliyotumwa kwa Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Amin Mohamed, DPP aliidhinisha kwamba watu hao ambao ni washirika wa Naibu Rais, Rigathi Gachagua wakabiliwe na mashtaka.
 
Afrika Ina safari ndefu sana , Kama Kenya walitengeneza katiba mpya na bado kuna uhuni kwenye siasa ni masikitiko makubwa.
 
Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, amejigamba kwa kudai kwamba yeye ndie pekee aliesababisha na kuchangia pakubwa Rais Dr. William Ruto akashinda uchaguzi wa 2022, la si hivyo bila jina lake kuwako kwenye karatasi za kupigia kura, kamwe asingeshinda urais wa Jamuhiri ya Kenya wakati huo.

Hata hivyo naibu wa Rais huyo wa Kenya, ana mlaumu, na kumtuhumu Rais William Ruto, kwa kupanga njama chafu dhidi yake, ikiwa ni pamoja na kuwafadhili wabunge kwa fedha, ili wambandue kwenye wadhifa wake.

"Acha kuwapa wabunge fedha za kunifukuza kazini, sitakubali jitihada zao. Wanataka nijiuzulu lakini sitaki". Alisema Gachagua kwa lugha yake ya asili.

Gachagua alimtaka Rais Ruto kuheshimu wapiga kura wa mlima Kenya, eneo ambalo anatoka, na kumsihi amuache ahudumu na amalize muhula wake kabla hajamchagua yeyote anaetaka kumchagua wakati wa azma yake ya kuchaguliwa tena 2027.

Hoja ya kumtimua Gachagua ofisini, iliwasilishwa bungeni mnamo Alhamisi Sept.26,2024 huku wabunge 242 wakiridhia na kuunga mkono hoja hiyo.

Tofauti za za kisiasa kati ya Naibu wa Rais huyo wa Kenya na bosi wake Dr.William Ruto ziliongezeka zaidi na kujidhihirisha bayana baada ya maandamano ya Gen z na hatua ya Ruto kumkatibisha hasimu wake wa kisiasa wa muda mrefu serikalini, Raila Odinga na hata kuwajumuisha baadhi ya wanachama wake kwenye baraza la mawaziri.

Gachagua anatuhumiwa kwa kuvunja sheria na katiba ya Kenya, matumizi mabaya ya ofisi, rushwa, ukabila, vitisho kwa watumishi wa umma na Boss wake pia, kugomea maamuzi ya baraza la mawaziri, kupinga sera na na mipango ya serikali na kutoa siri za baraza la mawaziri, kufadhili wahalifu ndani ya maandano ya gen z n.k.

Mpaka hapa unadhani tatizo linaweza kua ni katiba au ubinafsi wa kiongozi huyu mwenyewe?
Huyu keshakula chuma tena ajiandae kuishi kwa aibu. Yale maneno ya shombo aliyokua anayatoa yote yatakua yanamrudia kwenye njozi. Hataacha kuweweseka. Wakenya wameamua kumstaafisha bila hiari 🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Kituo fuatacho ni Ruto mwenyewe.
 
Kwa namna wanasiasa Kenya wanavyopenda pesa. Riggy G yupo Sana. Pesa itagawawia Kwa wabunge na Maseneta na watabadili Gia angani. Njaa mbaya
 
"Watu wa Mlima", hiyo ni kati ya kauli inayomgharimu sana na anapenda sana kuitumia.
Sehemu kubwa ya kauli zake ni kama anaigawa nchi.
Anakasirika Ruto kumuita Raila inaonyesha hana ukomavu na hafai kuwa kiongozi. Alitaraji waemdelee na mipasho ilihali unajua unayeshindana naye ni almost mna nguvu na influence sawa? Kwa faida gani?
Pona Yake Riggy atumie pesa za wakikuyu kutoa hongo kwa Maseneta (Seneti)
 
Back
Top Bottom