SI KWELI Rigathi Gachagua aonekana dirishani akiwachungulia Rais Ruto na Mfalme Charles III

SI KWELI Rigathi Gachagua aonekana dirishani akiwachungulia Rais Ruto na Mfalme Charles III

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nimekutana na picha hii mtandaoni ikimuonesha naibu wa Rais nchini Kenya Gachagua akiwa anawatazama kupitia dirisha Rais wa nchi hito William Ruto akiwa na King Charles III alipotembelea nchi hiyo, nikapata mashaka juu ya uhalisia wa picha hiyo naomba msaada wa kuihakiki.

GX77nzMWgAAtqGf.jpeg

 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa tovuti ya naibu wa Rais nchini kenya inaeleza kuwa Rigathi Gachagua alikuwa ni mtumishi wa umma nchini umo mara baada ya kumaliza masomo yake katika chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya, mwaka 2017 alichaguliwa kuwa mbunge wa Mathira mpaka mwaka 2022 ambapo alichaguliwa kuwa naibu wa Rais nchini Kenya.

Mnamo Oktoba 31 2023 Mfalme Charles III akiambatana na Malkia Camilla wa Uingereza alianza ziara ya siku nne ya kiserikali nchini Kenya, ambapo alitembelea maeneo mbalimbali nchini humo akianzia katika ikulu ya Rais jijini Nairobi huku akikabiliwa na matakwa mengi ya kuomba radhi kwa ukoloni wa zamani wa Uingereza katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Matukio mengi ya ziara hiyo yalirekodiwa kwa njia ya picha pamoja na video. Kumekuwepo na picha ambayo imesambaa zaidi mtandaoni ambayo ilikuwa ni sehemu ya matukio yaliyokuwa yakijiri mara baada ya Mfalme Charles III kuwasili, Picha inamuonesha Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua akiwatazama kupitia dirisha, Rais wa Kenya William Ruto akimtambulisha katibu mkuu wa baraza la mawaziri Musalia Mudavadi pamoja na King Charles III alipotembelea taifa la Kenya.

Uhalisia wa picha hiyo upoje?

Kwa kutumia Google reverse image search, JamiiCheck imebaini kuwa picha hiyo imehaririwa, na uhalisia wake kupotoshwa kwa kuambatanisha picha naibu wa Rais Rigathi Gachagua katika sehemu ya dirisha, picha halisi haioneshi uwepo wa Naibu wa Rais Gachagua katika picha hiyo.

Aidha picha hiyo ilipigwa na mpiga picha anayeitwa Samir Hussein Oktoba 31 2023 baada ya kuwasili kwa Mfalme Charles III na Malkia Camilla ikulu ya Nairobi nchini Kenya wakati ambao Naibu wa Rais hakuwepo nchini humo ambapo alikuwepo nchini Ubelgiji kumuwakilisha Rais William Ruto katika mkutano wa Mkutano wa Global Gateway Forum.

Hata hivyo kuna video inayomuonesha Mfalme na Malkia wakiwasili na hata kufikia alipokuwa akitambulishwa Katibu mkuu wa baraza la mawaziri Musalia Mudavadi Lakini video hiyo haioneshi uwepo wa naibu wa Rais Gachagua.

77208823-12691863-Queen_Camilla_and_King_Charles_III_are_greeted_by_President_Will-a-205_1698741644312.jpg

Picha halisi imechapishwa hapa na hapa
Back
Top Bottom