Rio Olympics 2016: 31st Games set for opening ceremony

Rio Olympics 2016: 31st Games set for opening ceremony

Nimewaona watz, wametia huruma aisee. Ungekuwa enzi za jk tungewasindikiza bwana. Dah
 
Yaani majirani zetu wa Kenya wamenda wengi wako 80 Wa TZ wako saba tu .
Duh mpaka aibu kwakweli yaani hatuthamini michezo kabisa yaani.
Hata Refugee Olympic Athletes wametushinda wako 10 .
Hatuwezi kuwa na hamasa maana hata Chanel moja tu ya kuonesha hiyo michezo haipo wote wanaonesha katuni tamthiliya mziki na waziri akipita kukagua mitaro hamasa itoke wapiiii?tz ni shida sana.
 
Go Go Go Team Tanzania. Washiriki saba, Gold Medal saba. Tupeleke watu mia moja hela zenyewe ziko wapi? Ngoja tununue madawati kwanza (In Magu voice)
 
daah watz wametia huruma..wamepita kama wanakimbizwa huku wamenuna, wakati nchi nyingine walikuwa wanapita huku wakicheza kwa furaha
 
Kwa mwonekano ule wa watanzania yaani ni dalili tosha kwamba tumeendaa kutalii Rio sio kushindana na kushinda!
 
Ni aibu kubwa sana Pilot. Kuna mataifa mengi ya Afrika ambayo wamekuwa na vita wao kwa wao na nchi kuwa nyeng'enyeng'e lakini wamepeleka wanariadha wengi kuliko Tanzania. Uganda tuliwakomboa kutoka kwa nduli na uchumi wao ulianguka vibaya sana lakini wametupita wana wanariadha 21 mara tatu ya idadi yetu.

Yaani majirani zetu wa Kenya wamenda wengi wako 80 Wa TZ wako saba tu .
Duh mpaka aibu kwakweli yaani hatuthamini michezo kabisa yaani.
Hata Refugee Olympic Athletes wametushinda wako 10 .
 
4654.jpg

Yusra Mardini powers through the water during her Women’s 100m Butterfly heat.
 
Adam Peaty breaks 100m breaststroke world record!
A stunning heat from the favourite for the 100m breaststroke, Britain’s Adam Peaty, who sets a ridiclous time of 57.55s. What a statement.

2274.jpg

Adam Peaty, right, on his way to setting a new world record.
 
3005.jpg

Greg Van Avermaet celebrates after crossing the finish line to win the men’s cycling road race
 
Halafu kumbe nchi nyingi sana kule Ulaya zina watu wachache sana, nyingi zikiwa chini ya milioni 15. Kuna nchi zina watu elfu sabini! Yule jamaa liyebeba bendera ya visiwa vya Tonga alinogesha ufunguzi sana.
 
mwe nimefurahi sana kuona "Refugee team" kwenye olympic.
Nitakuwa nawafuatilia. Hivi wa TZ wanacheza michezo gani kwenye Olympic?

Na pia nasubiri kwa hamu kuangalia Rugby sevens.

Asante kwa kufungua thread BAK.
Rugby? Ulikulia Australia!
 
Shukrani sana afrodenzi. Nimeshangaa sana hata Burundi pamoja na matatizo yao yote ya machafuko ndani ya nchi na kutokuwa na rasilimali nyingi kama Tanzania wamepeleka wanariadha 10 na population yao ni 10 million, sisi wenye polupation ya 49 million na rasilimali chungu nzima walionyesha tumepekeleka wanariadha 7 tu. Kama sikosei idadi ya wanariadha wetu walioenda Rio tumewazidi Somalia kwa wanariadha wawili au watatu hata Somalia jamani!!!! Duh!!!! Kweli nchi hii michezo haipewi kipaumbele kabisa. Najua wewe mpenda Rugby huu mchezo nimejaribu kuufahamu lakini umenipiga chenga. Ukanifunga kamba kwamba utanipa tuition ya nguvu ili niufahamu lakini hadi hii leo bado sijaujua lol!

Unajua kuna maafisa wangapi waliowasindikiza hao wanariadha saba?
 
Halafu kumbe nchi nyingi sana kule Ulaya zina watu wachache sana, nyingi zikiwa chini ya milioni 15. Kuna nchi zina watu elfu sabini! Yule jamaa liyebeba bendera ya visiwa vya Tonga alinogesha ufunguzi sana.
Yaani jamaa anatrend mitandaoni saizi. Akina dada ndo wako hoi kabisa wakisaka jina lake
 
Dada zetu wa Zimbabwe wamekuwa kichwa cha mwendawazimu kwenye mpira wa miguu!

Ila dah! naona huyu namba kumi amefunga bao la ukahika sana.- bado siyo kichwa cha mwendawazimu!
 
Sijui Mkuu Kichuguu safari hii waliamua kuonyesha population ya kila nchi, wanariadha wangapi iliowaleta na medals ngapi ilipata 2012. Channels mbili tofauti moja ilionyesha population ya Tanzania ni 48.9 million na nyingine 51.1 million na wanariadha watakaoshiri ni 7.

Unajua kuna maafisa wangapi waliowasindikiza hao wanariadha saba?
 
Sijui Mkuu Kichuguu safari hii waliamua kuonyesha population ya kila nchi, wanariadha wangapi iliowaleta na medals ngapi ilipata 2012. Channels mbili tofauti moja ilionyesha population ya Tanzania ni 48.9 million na nyingine 51.1 million na wanariadha watakaoshiri ni 7.

In- fact mimi niliangalia ile iliyosema tuko millioni 51.1 halafu nikalinganisha na nchi zote za Ulaya nikagundua kuwa hatutakiwi kuwa tunapata misaada kutoka nchi kama Norway, Sweden, Denmark na Finland! Hata kidogo
 
Rugby? Ulikulia Australia!
Hapana napenda tu rugby na ninafuatilia kwa I karibu . Ni Kama vile Mtanzania anae shabikia Man U .

Anyway nimefurahi mno kuona Hurricanes wameshinda super rugby final last night wamewashinda Lions kutoka RSA. Ooohhh by the the way OZ hatasio wazuri kivile ikija kwenye rugby union . Wenyewe ni wazuri kwenye rugby league. Sevens ambao ndio wako kwenye Olympic Hilo Taji nawapa Fiji . Nasubiri kwa hamu kuangalia sevens .
 
Back
Top Bottom