seems siasa bado zinawabeba wamarekani, nimejaribu kuangalia medali zote na medali za kuogelea hapa
msimamo wa medali
msimamo wa medali za kuogelea
hivyo ukiangalia hapo medali 16 kati ya 30 za dhahabu za marekani zimetokana na kuogelea, hio ni zaidi ya asilimia 50. ukitoa medali za kuogelea wote china na uingereza wapo juu ya marekani kwenye michezo mingine.
pia ukichunguza michezo ya kuogelea historia yake ni toka kipindi cha cold war, iliekwa mingi ili marekani ampite urusi, kuna events nyingi sana za kuogelea, mfano hizi ni events za mita 100 kuogelea
-breaststroke
-backstroke
-freestyle
-freestyle relay
-medley relay
-butterfly
events hizo hizo utazikuta mita 50, 200, 400 na kuendelea kwa wanawake na wanaume.
michezo ambayo marekani si sana kupata medali nyingi hukuti events nyingi, mfano kukimbia. kama sijakosea kumbia kupo kwa kawaida, kupokezana vijiti na kuruka viunzi. inabidi na sisi Africa tupige kelele ili tuekewe michezo yetu tunayoiweza kama kukimbia na mguu mmoja, mbio za kuvaa magunia, mbio za kueka yai juu ya kijiko na kukimbia hali ya kuwa kijiko kipo mdomoni etc.