Rio Olympics 2016: 31st Games set for opening ceremony

Rio Olympics 2016: 31st Games set for opening ceremony

seems siasa bado zinawabeba wamarekani, nimejaribu kuangalia medali zote na medali za kuogelea hapa

msimamo wa medali
vtT2KZV.jpg


msimamo wa medali za kuogelea
aFBraa8.jpg


hivyo ukiangalia hapo medali 16 kati ya 30 za dhahabu za marekani zimetokana na kuogelea, hio ni zaidi ya asilimia 50. ukitoa medali za kuogelea wote china na uingereza wapo juu ya marekani kwenye michezo mingine.

pia ukichunguza michezo ya kuogelea historia yake ni toka kipindi cha cold war, iliekwa mingi ili marekani ampite urusi, kuna events nyingi sana za kuogelea, mfano hizi ni events za mita 100 kuogelea
-breaststroke
-backstroke
-freestyle
-freestyle relay
-medley relay
-butterfly

events hizo hizo utazikuta mita 50, 200, 400 na kuendelea kwa wanawake na wanaume.

michezo ambayo marekani si sana kupata medali nyingi hukuti events nyingi, mfano kukimbia. kama sijakosea kumbia kupo kwa kawaida, kupokezana vijiti na kuruka viunzi. inabidi na sisi Africa tupige kelele ili tuekewe michezo yetu tunayoiweza kama kukimbia na mguu mmoja, mbio za kuvaa magunia, mbio za kueka yai juu ya kijiko na kukimbia hali ya kuwa kijiko kipo mdomoni etc.

Nimeielewa point yako mkuu, sana tu!
 
Usa baby inakuwaje palee wamekuwa disqualified wananyang'anywa bronze
 
Tori Bowie atasumbua wenzake sana huko baadae, anaonekana ni mwepesi sana, English anakuja kuja sema bado hajafikia level ya medal, aendelee kujifua zaid btw nimekapenda sana!! Tianna yupo vizur kweny Long jump, pia sio mbaya kwny track.
Kilichonifurahisha ni Allyson Felix kupata angalau Gold Medal, sikupenda kilichomkuta kwenye ile final ya 200m. Hope presha itakua imeshuka walipopashinda usiku wa kuamkia Leo!!
 
Wakuu Lile Sanamu La Rio Lina Nini Cha Muhimu Mle Ndani Mpaka Limekuwa Maarufu
Mwenye Kujua Anijuze Kwenye Hii Thread
 
Mitä 1500 M Kenya imechemka. ...

Mitä 800 W. ... Semenya ameshinda akifuwatiwa na Mburundi huku mdada toka Kenya akishika nafasi ya tatu
 
Matokeo 5000 M
  1. Mohamed Farah GBR
  2. Paul Kipkemoi Chelimo USA
  3. Hagos Gebrhiwet ETH
 
Julius Yego amejitoa kwenye kurusha mkuki baada ya kuumia mguu, hadi wakati amejitoa alikuwa katika nafasi ya kwanza kwa kurusha mkuki kwa umbali wa mita 88.24, na baadae kupitwa na Röhler wa Ujerumani, kwa umbali wa mita 90.30.
 
Back
Top Bottom