Ripoti: Hali ya Utekelezaji wa Adhabu ya Kifo Barani Afrika

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Nchi 13 za Afrika (24%) Bado zinatekeleza Hukumu ya Kifo katika Sheria zake na Utendaji wake wakati Nchi 25 sawa na (46%) zimemeifuta kabisa.

Nchi 15 za Afrika (28%) ikiwemo Tanzania zinaruhusu Adhabu ya Kifo kwa uhalifu wa kawaida, lakini hazijaitumia kwa zaidi ya miaka 10 na baadhi zimeanza michakato ya kuifuta Adhabu hiyo.

Nchi 1 ya Afrika (2%) imefuta Adhabu ya Kifo kwa uhalifu wote isipokuwa kwa makosa yaliyotendwa kipekee ikiwemo wakati wa vita.

================

Mataifa ambayo yametekeleza hukumu ya kifo kati ya mwaka 2013 na 2021​

Afghanistan, Bahrain, Bangladesh, Belarus, Botswana, Chad, China, Egypt, Equatorial Guinea, India, Indonesia, Iran, Iraq, Japan, Jordan, Kuwait, Malaysia, Nigeria, Korea Kaskazini, Oman, Pakistan, Palestina,
Saudi Arabia, Singapore, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Taiwan, Thailand, United Arab Emirates, Marekani, Vietnam na Yemen.

Nchi ambazo hazijatekeleza adhabu hiyo licha kuwepo kisheria kati ya 2013 na 2021

Tanzania si nchi pekee ambayo haitekelezi adhabu hiyo licha ya kuwepo kisheria.

Nchi nyengine zinazofanya hivyo ni pamoja na Antigua na Barbuda, Bahamas, Barbados, Belize, Comoros, Cuba, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Dominica, Ethiopia, Gambia, Guyana, Jamaica, Lebanon, Lesotho, Qatar, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadines, Trinidad na Tobago, Uganda na Zimbabwe.
 
Tanzania nchi yangu pls FUTA adhabu hii,adhabu hii ni ukatili wa kijima na haina tija yeyote katika kuzuia murders
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…