JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema katika kipindi cha Januari hadi Mei 2022, imekamata kilo 877.217 za dawa za kulevya, imezuia uingizaji wa kilo 122,047.0855 na lita 85 za kemikali bashirifu nchini.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya ametoa takwimu wakati akizungumzia operesheni waliyoifanya ya ukamataji wa dawa za kulevya katika kipindi cha miezi mitano.
Kamishna Jenerali Kusaya alisema kati ya kiasi hicho cha dawa za kulevya walichokamata heroine ni kilo 174.122 zilizowahusisha watuhumiwa sita ambao kwa sasa wameshafikishwa mahakamani.
"Mei 12 mwaka huu katika eneo la Tabata Relini, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, mamlaka ilikamata kilo 174.77 za dawa za kulevya aina ya heroine. Katika tukio hilo, Salum Mpangula alikamatwa kwa tuhuma za kusafirisha dawa hizo," alisema.
Kuhusu kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya, alisema DCEA inaendelea kufanya ukaguzi wa kufuatilia watu wanaokiuka taratibu za uingizaji na usambazaji.
Alisema katika kipindi cha Januari hadi Mei mwaka huu DCEA kupitia mfumo wa kielektroniki ilifanikiwa kuzuia uingizaji wa kilo 122,047.085 na lita 85 za kemikali bashirifu.
Pia alisema katika kipindi hicho, DCEA imeteketeza ekari 21 za mashamba ya bangi mkoani Arusha na kilo 250.7 za dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine ambazo mashauri yake yalimalizika mahakamani.
Kamishna Jenerali Kusaya alisema: "Katika kuhakikisha jamii inapata elimu sahihi juu ya tatizo la dawa za kulevya, DCEA imeandaa mwongozo utakaotumika kutoa elimu, imeshiriki kuandaa ujumbe juu ya tatizo la dawa za kulevya katika mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea na kutoa elimu kwa kamati za ulinzi na usalama, kamati za afya na watendaji wa serikali za mitaa ili wasaidie kuongeza uelewa wa tatizo la dawa za kulevya kwa jamii."