Ripoti Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC): Wanawake Viwandani wananyanyasika kingono

Ripoti Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC): Wanawake Viwandani wananyanyasika kingono

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) wakati kikizindua Ripoti ya 10 ya Biashara na Haki za Binadamu leo August 27, 2024, Afisa Program Mwandamizi wa Tafiti kutoka kituo hicho, Fundikila Wazambi amesema kuwa wamebaini kuwepo kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za Binadamu kwenye Viwanda na Makampuni mbalimbali ya kibiashara.

Amesema kuwa wamebaini kwamba Wanawake wamekuwa wakikumbana na ukatili wa kingono sambamba na rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi hususani kwenye Viwanda vidogo na vya kati.

Lakini amebainisha kuwa upande wa Wanaume nao wamekuwa wakikumbana na uonevu, vitisho pamoja na ukatili wa kisaikolojia na kimwili ikiwemo kupigwa mateke na makofi.

Sanjari na hilo ripoti hiyo inabainisha maeneo mbalimbali ya kibiashara ambayo haki za binadamu zishindwa kuzingatiwa ipasavyo.

Maeneo hayo ni kama wafanyakazi kupata ujira duni, kunyimwa haki za kujiunga na vyama vya Wafanyakazi, kucheleweshewa malipo ya mishahara, kukosa mikataba n.k

Baadhi ya wafanyakazi ambao wametajwa kukumbana na changamoto zanazokienda kinyume na haki, ikiwemo kufukuzwa bila utaratibu pamoja na kukosa mikataba ni walinzi wa makampuni binafsi ya ulinzi pamoja na madereva.

Katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kingono vinapungua zaidi kwenye maeneo ya kibiashara hususani viwandani LHRC wanashauri Serikali kuridhia azimio la Shirika la kazi Duniani ILO (Violence and Harassment Convention, 2019 (No. 190).

Azimo hilo linajielekeza kuthibiti vitendo vya unyanyasaji wa kingono ambavyo vinaweza kusababisha madhara ya kimwili, kisaikolojia, kingono au kiuchumi kutokea katika mazingira ya kazi.



LHRC: HAKI YA KUPUMZIKA NI NDOTO KWA MADEREVA NA WAFANYAKAZI WA HOTELI
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kuhusu Viwanda na Makampuni ya Kibiashara Nchini imeonesha kuwa kuna changamoto ya Watumishi kukosa nafasi ya kupumzika.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya 10 ya Biashara na Haki za Binadamu, leo Agosti 27, 2024, Afisa Programu Mwandamizi wa Tafiti wa LHRC, Fundikila Wazambi amesema changamoto hiyo hasa imebainika kuwepo kwa madereva wa mabasi, malori pamoja na Wafanyakazi wa Hotelini.
-
Ameongeza kuwa 40% pekee ndio Wafanyakazi wamekiri ulipwa malipo ya ziada.


51% YA WAFANYAKAZI HAWAUELEWI WARAKA WA VIWANGO VYA MISHAHARA
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kuhusu Viwanda na Makampuni ya Kibiashara Nchini kimesema kuna changamoto ya uelewa kuhusu Waraka wa Serikali wa Wiwango vya Mishahara kutoeleweka kwa Wahusika wengi.

Akisoma ripoti ya Biashara na Haki za Binadamu, leo Agosti 27, 2024, Afisa Programu Mwandamizi wa Tafiti wa LHRC, Fundikila Wazambi amesema “Tunafanya kazi tupate pesa, tumekuwa tunapigia kelele sana kupata waraka mpya hatimaye tuliupata Mwaka 2022 lakini Asilimia 51 ya Wafanyakazi hawaueleweli huu waraka huo.”

Ameongeza “Hivyo, kuna uhitaji mkubwa wa kutoa elimu ili waweze kufahamu kuhusu vima vya chini vya mishahara waweze kudai haki yao, baadhi ya Waajiri wanatumia fursa hiyo kulipa kiwango cha chini kwa Watumishi wao.”


JOYCE KOMANYA: KUNA UKIUKWAJI WA HAKI ZA ARDHI, WENYEJI HAWASHIRIKISHI
Akichangia Ripoti ya Biashara na Haki za Binadamu ya Mwaka 2023/24, leo Agosti 27, 2024, Joyce Komanya amesema bado kuna changamoto nyingi kwenye uwekezaji wa ardhi hasa unaofanywa katika shughuli za uchimbaji wa Madini.

Joyce ambaye ni Msimamizi Kitengo cha Biashara wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) amesema kuna ukiukwaji wa Haki za Ardhi ikiwemo kukosekana kwa ushirikishwaji kutoka kwa Mwananchi dhidi ya Kampuni ya Mwekezaji anayepewa ardhi kwa ajili ya kuwekeza.

Akitoa mfano mabadiliko ya matumizi ya ardhi, Sheria zinaonesha Serikali za Kijiji hazina mamlaka ya kuwapa wawekezaji Ardhi, kinachotokea ni kukosekana ushirikishwaji wa Wakazi katika mchakato huo na hivyo kusababisha mgogoro.
 
haki za watu zisimamiwe! hivi mtu unapigwaje kazini..? ya kwamba unitandike teke walahi nang'ata komwe la mtu!.
 
Back
Top Bottom