Ripoti Maalum: Kutajwa kwa Vyombo vya Usalama na Wengine kwenye Madawa ya Kulevya ni Mtego kwa JK

Ripoti Maalum: Kutajwa kwa Vyombo vya Usalama na Wengine kwenye Madawa ya Kulevya ni Mtego kwa JK

Status
Not open for further replies.
suala kubwa hapa ni kuwa Watanzania wanaangamizwa na haya madawa lakini juhudi zikianza kama hivi mara wengine mnaibuka na mambo ya dini, makabila, vyama nk.
Vatican wanaweza wakawa wameliona hilo na wanaliongelea kutoka ndani mwao lakini usisahau kuwa hata Saudia kuna adhabu ya kifo kwa dealers ikiwa ni ushahidi kuwa hii kitu haitakiwi huko. Pia usisahau kuwa kuna mtu mmoja prominent aliwahi kufia hoteli moja kubwa hapo Dar es Salaam nafikiri wakati wa awamu ya pili ambapo ilisemekana kisa cha mauti ilikuwa madawa na hakutokea Vatican bali kwenye nchi unazotaka 'kuzitetea'.
Acha kuondoa wachangiaji kwenye hoja ya msingi ambapo ukweli ni kuwa serikali imeshindwa kupambana na wauza madawa kwa maana huenda wameiweka mfukoni au watu wa serikali wenyewe ndio dealers pia kama mleta hoja anavyoainisha.

Saudi Arabia si msikiti wala kanisa ni nchi na ina sheria zake. Vatikan ni makao makuu ya kanisa linalojishughulisha na hizo shughuli. Soma link hizo ujionee.

Nasema Serikali inashughulikia hili, Kikwete si mtu wa kukurupuka na ukikurupuka kwa taasisi kubwa kama Kanisa Katoliki utaumia, lina nguvu sana dunia nzima kwa hiyo inabidi uende ki sayansi.

Ndio maana hata Kikwete akasema tukiwataja nchi itayumba. Unafikiri ni kwa nini? nini au nani hapa anaeweza kuyumbisha nchi? Fikiri!
 
Kwa vile umejua kuchangia 2011 ndiyo unafikiri forum hii ndiyo ya kwanza??

Kwa taarifa tu members wengi wa zamani walikuwa ni members wa BCS toka 2003. Wakati huo Mzee Mwanakijiji akijulikana kama Mwanakijiji na Ze Mutuz / Sauti ya umeme akijulikana kama ES. Marehemu Nyaulawa kwa ambitions zake za kisiasa akaamua kuiua. Sasa hii ya kitu ya uhuru wa maoni wakati wa JK ni uongo uliozidi mipaka. Tatizo lako furum yako ya kwanza ni JF .............. inaelekea hata hujui kuwa ilikuwa inaitwa Jambo Forums before. Na kama ni kweli kuna uhuru wa kuchangia wakati huu wa JK waulize wadau kwa nini jina la Jambo forums lilibadilika baada ya mtandao kuzimika kwa kama wiki na na misukosuko ambayo akina Invisible na Mello waliipata!!

By the way, kama kuna uhuru wa kuchangia kwa nini zaidi ya 99 % ya members hawatumii majina yao ............ including wewe mwenyewe na vijana wa Lumumba!!??

Hunijuwi usingeyasema hayo. Na Zero ni jina lako? sio?

Hivi wewe unafikiri ukichangia kwa jina tofauti ukitakikana ndio hupatikani? unazijuwa haswa kompyuta zinavyofanya kazi? wewe kweli ZERO.
 
Naona Vatican ni shida kwako!kwenye link zako hao maaskofu ulioweka sijaona katoliki babda ni nimeona vibaya nitafurahi ukiendelea leta ushaidi zaidi kwenye hilo ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe!

Vatikan hujaona link zao nilizoweka? pole sana.
 
Kwa huu udini wako .... watoto wako wote wataoa au kuolewa na wakristo.....

Kazi kwao, lakini AlhamduliLlah mmoja kisha olewa wawili wameshaoa na mwingine bado yuko chuo.

Ukisikia Muislaam anaolewa na Mkristo, hakuna ndoa hapo ni zinaa tu.
 
Hunijuwi usingeyasema hayo. Na Zero ni jina lako? sio?

Hivi wewe unafikiri ukichangia kwa jina tofauti ukitakikana ndio hupatikani? unazijuwa haswa kompyuta zinavyofanya kazi? wewe kweli ZERO.

Nani kasema kuwa ukitumia jina halisi huwezi patikana.

Watu wanatumia majina badia kwa vile hawako huru kama wewe unavyependa tuamini, including your self. Period!! Watanzania nidhamu ya uoga iko ndani yetu. Ukienda kwenye blogg za wenzetu nchi nyingine huwezi kuta hizi design za majina kama FF!!
 
Na wanao na Ndugu zako waanze kutumia ili upate akili ya kujua nani upambane nae... Viongozi wa serikali ya CCM wanaojihusisha na Madawa ya kulevya tayari wameniharibia ndugu zangu... wewe watetee ila ulipwe kwa jinsi unavyofikiria....

Dua ya kuku hiyo. Kama wewe ni muuzaji ngoja siku zako, ziko karibu sana.
 
Lugha ya kikristo ni ngumu siyo ya kukaririshwa kama ile nyingine Mkuu

Ndio mnavyojazwa ujinga hivyo.

Lugha ya Kiislaam ni nyepesi sana hata huna haja ya kumtafuta Father Kit Cunningham kukutafsiria, unamjuwa Father Kit Cunningham?
 
Nani kasema kuwa ukitumia jina halisi huwezi patikana.

Watu wanatumia majina badia kwa vile hawako huru kama wewe unavyependa tuamini, including your self. Period!! Watanzania nidhamu ya uoga iko ndani yetu. Ukienda kwenye blogg za wenzetu nchi nyingine huwezi kuta hizi design za majina kama FF!!

Tatizo lako ni Zero.
 
Mwanakijiji,

hivi unategemea nn kama raisi wako alitangaza hadharani kuwa anayolist ya wauzaji na mpaka leo hajaifanyia kitu wala kuongelea, kwanan asiwe mkali kama alivokua mkali kwny ishu ya hao wakimbizi wanaovamia mipaka????? na kwann hajawaita 'wazee wa dar es salaam awashtakie kama ilivo kawaita yake????'

SUCH A DHAIFU PRESIDENT, SUCH A DHAIFU GOVERNMENT, SUCH DHAIFU CITIZENS!!!!
 
Ile kauli ya John Mnyika kua Rais ni dhaifu na serikali dhaifu inaendelea kujidhihirisha!!
Ipo hatari ya dhahiri kuwa, katika safu ya viongozi wa juu kabisa wa serikali, wapo wanaojihusisha na biashara hii haramu ya madawa ya kulevya, na ndiyo siri kubwa inayofanya vijana wanaobeba madawa hayo, waweze kupita kiurahisi pale uwanja wa ndege, wa JK Nyerere, hata wakiwa na mizigo ya mabegi ya madawa ya kulevya, lakini wakifika nchi za nje, kama South Africa, China na Hong Kong wanadakwa kirahisi kabisa!

Nchi haiko salama hata kidogo, kama alivyotaka kutuaminisha JK majuzi, alipokuwa Kagera!
 
Copy halafu ibandike kwenye google translator.
Hiyo google translator ndio nini tena, jamani si wengine tumezaliwa kabla dot.com; mbona kizee weye wapenda kunipa tabu miye, hebu nifasirie Allah atakulipa Inshaallah!
 
SSM kwa miaka 49 ndipo imetufikisha!!! Kikae pembeni kingine kijaribu na kama kikishindwa nguvu ya umma bila uchakachuaji ikiondoe!!! Aibu sana, sana. Halafu utashangaa kesi zote hizo na haya majina yaliyotajwa na pia yanajulikana yatayeyuka kama theluji ya mlima Kilimanjaro inavyoyeyuka kwa sababu ma mabadiliko ya tatiba nchi iletayoe na damage ya Ozone Layer.
 
Hiyo google translator ndio nini tena, jamani si wengine tumezaliwa kabla dot.com; mbona kizee weye wapenda kunipa tabu miye, hebu nifasirie Allah atakulipa Inshaallah!

Hapo unaweza kutafsiri kwa lugha nyingi tu mfano Kiingereza kwenda Kiswahili, fata hii link:Google Translate

Halafu jaribu kuitumia, ingawa tafsiri zake si kama atavyotafsiri binaadam lakini inasaidia sana na inaboreshwa mara kwa mara.
 
Thank you FaizaFoxy, now I can verify that you're truly old-aged woman and also a parent (same) like me. From now onwards, I will (as much as possible) comment consciously and positively to the most of your submissions. アライクム!
 
Saudi Arabia si msikiti wala kanisa ni cnhi na ina sheria zake. Vatikan ni makao makuu ya kanisa linalojishughulisha na hizo shughuli. Soma link hizo ujionee.

Nasema Serikali inashughulikia hili, Kikwete si mtu wa kukurupuka na ukikurupuka kwa taasisi kubwa kama Kanisa Katoliki utaumia, lina nguvu sana dunia nzima kwa hiyo inabidi uende ki sayansi.

Ndio maana hata Kikwete akasema tukiwataja nchi itayumba. Unafikiri ni kwa nini? nini au nani hapa anaeweza kuyumbisha nchi? Fikiri!

Unajichanganya...mara serikali inalishugulikia hili mara suala hili gumu....wee msemaji wa jk? njoo basi with verified user tujue nani annaongea. Vijana wanaangamia bado unatetea udhaif wa serikali ya jk.
 
Sawa mimi najichanganya, wewe usijichanganye zaidi kwa kutokunielewa.
 
mkuu mzee mwanakijiji endapo wenye mamlaka hawakuelewa mwandishi wa barua ile, andiko lako hili lazima watalielewa. Ninachojiuliza ni je, ile orodha ya majina ya wanaofanya biashara hii ya madawa ya kulevya ambayo mh raisi aliwahi kusema kuwa anayo, alichukua hatua gani? Ama ndio ilikuwa mtaji wa mabilioni ya kikwete? Na je, ipo haja kureview mpango ule wa mabilioni ya kikwete ili kuona mafanikio yake?

nchi ina wenyewe mnawaona majukwaani ni mic tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom