Ripoti: Necta 2011 results - mkoa wa arusha

Ripoti: Necta 2011 results - mkoa wa arusha

Kwa ambaye hakupata bahati ya kuona hii ripoti, imeambatanishwa. Labda itasaidia kujua kwanini watoto wetu wanafeli, pamoja na ukweli wa hizi ripoti.

Nimeipitia, inasikitisha na inashangaza. Sijui wanaotoa mapendekezo baraza lirudie kusahihisha sasa hapo unasahihisha nini tena? Ripoti kama hizi ni za muhimu sana zikarudi kwa wadau ili tujue tulipo maana tunaweza kuendelea kujidanganya.

Tatizo lipo kubwa kwa walimu.Walimu ni mbumbu sana hawana uwezo ,tatizo lingine ni lugha, ukisoma sample za reactions za wanafunzi utaona lugha nikichomi kubwa pia.
 
Nimei-print ili niipitie baadaye kwa umakini, hizi report zingekuwa zinatolewa kwa wazazi na wanafunzi ili wajue kilichopo nyuma ya pazia, tusiwe watu wa kulalamika tuu.. BABA E's
 
Last edited by a moderator:
Mimi napata wakati mgumu sana ninapofikiria ni jinsi gani Taifa hili litakapofanikiwa kuimarisha mfumo wa Elimu.Hebu anzia majumbani uangalie vipindi vinavyoonyeshwa kwenye Luninga za Tanzania.Karibu zote kuanzia asubuhi mpaka usiku vipindi ni nyimbo na Maigizo ya Mapenzi na hili haliishii tu Luninga hata Redio ni hivyo tena kwa kwenda mbele.Watoto wa Taifa hili wanaanza kufundishwa Mapenzi hata kabla ya Shule za Chekechea na huu ndiyo unakuwa utaratibu wa Maisha yao kiasi kwamba inapofika kwenye ngazi ya Elimu ya Sekondari tabia hii na yenyewe inakua na kufanya akili za hawa Watoto hasa wanaosoma shule za kutwa kutotambua mambo mengine zaidi ya Mapenzi.Upuuzi huu ni tatizo kubwa ambalo kama halitapatiwa ufumbuzi,Sisi kama Taifa tusitegemee kupata Mwarobaini wa kufeli kwa Watoto katika ngazi zote za elimu katika nchi hii.Elimu ina miiko na taratibu zake ambapo visipozingatiwa mbadala wake haupo.Tunaweza kuangalia mifano katika Shule binafsi hasa za Madhehebu ya Dini fulani ambao pamoja na Mazingira mazuri ya kusomea lakini kubwa zaidi ni kusimamia nidhamu katika Shule hizo na kuwajengea Watoto mazingira ya kujitambua.
 
Ukiisoma vizuri hii ripoti nadhani baraza hawana la kulaumiwa. Waache wafeli tu jamani. Wako busy sana hawa madenti hawana mda wa kusoma.
 
Ukiisoma vizuri hii ripoti nadhani baraza hawana la kulaumiwa. Waache wafeli tu jamani. Wako busy sana hawa madenti hawana mda wa kusoma.

Kwakweli inasikitisha sana. Inatakiwa walimu na wazazi na pia wanafunzi walioko shuleni waisome.
 
Ukiisoma vizuri hii ripoti nadhani baraza hawana la kulaumiwa. Waache wafeli tu jamani. Wako busy sana hawa madenti hawana mda wa kusoma.

Siku hizi maadili yameporomoka kabisa, watoto wako busy na ulimwengu. Ukiangalia familia nyingi nafasi ya mzazi haionekani, kuna watoto wengine wameachiwa jamii iliyowazunguka ndo iwalee. Kwa hiyo mtoto akikutana na watu wenye tabia mbaya na yeye anakua hivyo hivyo.
 
Nimesoma ripoti hiyo ya matokeo ya CSEE 2011 kwa mkoa wa Arusha, sijaamini hata kidogo kama mhitimu wa Kidato cha nne anakuwa na uwezo mdogo kiiasi hicho. Hakika elimu ni janga la taifa maana kama mhitimu wa kidato cha nne hawezi kuelewa kwa kiasi hicho, ni jambo la hatari sana. Hivi hiyo ripoti iliwafikia Wahusika wasimamizi wa elimu? Kama iliwafikia hatua zipi zilichukuliwa? Na kama hakuna hatua zilizochukuliwa kwa nini tushangae matokeo ya sasa?

Hakiki yaliyooandikwa na badhi ya wanafunzi ni maajabu ya dunia
 
Nimeipitia, inasikitisha na inashangaza. Sijui wanaotoa mapendekezo baraza lirudie kusahihisha sasa hapo unasahihisha nini tena? Ripoti kama hizi ni za muhimu sana zikarudi kwa wadau ili tujue tulipo maana tunaweza kuendelea kujidanganya.

Pamoja na kwamba nakuballiana na wewe na umuhimu wa hii ripoti. Lakini pia ukiona sample ya maswali unaweza kukubalina na wanaolalamika kuwa mitihani huwa haiendani na kiwango cha vijana wa kidato cha nne. Kuna swali kwa mfano linauliza: The role of hypothesis in research. Hypothesis kwa mtoto wa kidato cha nne mmhhh labda watoto wa sasa hivi ni wakali wa Quantitative Research na Statistics
 
Nadhani jambo la msingi tuanzie kwenye mitaala yao. Kama katika maudhui wanyotakiwa kufundishwa na role ya hypothesis ipo. huwezi kusema maswali ni ya kiwango cha juu. kwa sisi walimu kabla ya kusema mtihani ni mgumu au la inabidi kuangalia ni nini ambacho wanafunzi wanapaswa kufundishwa katika elimu ya sekondari. Mtihani mzuri ni ule unao cover mambo yote ambayo mwanafunzi amefundishwa katika level husika. Kwa hiyo kabla ya kusema kama mitihani ya ngazi yoyote ile ni migumu au la ni vema kuangalia yanayofundishwa. Kwa upande mwingine inawezekana mitaala yetu imeweka mambo yaliyo magumu sana kwa uwezo wa wanafunzi kwa hiyo haya mambo ya mitaala na mitihani yanapaswa kuangaliwa kwa pamoja.
 
Pamoja na kwamba nakuballiana na wewe na umuhimu wa hii ripoti. Lakini pia ukiona sample ya maswali unaweza kukubalina na wanaolalamika kuwa mitihani huwa haiendani na kiwango cha vijana wa kidato cha nne. Kuna swali kwa mfano linauliza: The role of hypothesis in research. Hypothesis kwa mtoto wa kidato cha nne mmhhh labda watoto wa sasa hivi ni wakali wa Quantitative Research na Statistics

Hapo ndipo pa kuanzia kwani unatakiwa uende kwenye syllabus uone contents na competency anayotakiwa kuwa nayo candidate then tuwe kwenye position ya kujudge kama swali liko nje ya scope au vipi???
 
mkuu neno hypothesis nililisikia kwa mara ya kwanza nikiwa form one kwenye kipindi cha
 
.
Ukisoma hiyo Ripoti, kwa kweli wanafunzi ni Mbumbumbu kabisa

Yaani hata Intelligence Quotient - IQ zao ziko chini kabisa, bure kabisa!

.
 
Hapo ndipo pa kuanzia kwani unatakiwa uende kwenye syllabus uone contents na competency anayotakiwa kuwa nayo candidate then tuwe kwenye position ya kujudge kama swali liko nje ya scope au vipi???

Mkirua hivi umeyaangalia yale maswali kweli au unaamua kubisha tu? Yale maswali mengi waliyoyaweka yanahitaji analytical skills ambazo sidhani kwa mtoto wa kidato cha nne atakuwa nazo.
 
.
Ukisoma hiyo Ripoti, kwa kweli wanafunzi ni Mbumbumbu kabisa

Yaani hata Intelligence Quotient - IQ zao ziko chini kabisa, bure kabisa!

.
Hiyo report siyo scientific kiasi hicho bwana. Wangekuwa wametoa majibu yote tungeweza kujudge vinginevyo wamefanya kitu kwenye research tunakiita selective observations (only choosing to look at things that are in line with your preferences or beliefs).
 
mkuu neno hypothesis nililisikia kwa mara ya kwanza nikiwa form one kwenye kipindi cha

Kipindi cha nini?
Ulifanya research form one? Hapa hawajauliza kama ulishawahi kusikia neno hypothesis, wamemuuliza mwanafunzi kama anaweza kuelezea umuhimu wa hypothesis kwenye research.
 
NECTA wenyewe wanakwambia, katika masahihisho yao ya majibu ya wanafanzi, kwamba moja ya matatizo ya kupeleka huduma za afya kwa wote Tanzania ni kwamba watu wako "spacily populated".

I used to oppose the idea of using English as a medium of communication.

I am not so sure anymore.

Ukiisoma hiyo PDF utaona hata hayo majibu yaliyotolewa mfano kwamba ni mabaya kuna vi idea vipo ila inawezekana kabisa moja ya matatizo makubwa kabisa ni kwamba wanafunzi wanashindwa kujieleza Kiingereza.

NECTA wanashindwa kujieleza kiingereza (spacily populated? does anybody proofread anymore?), itakuwa wanafunzi?

Halafu nilitegemea kitu kiwe statistically based kilichojaa demographics and what not.

Kuja kusoma the whole thing is highly anecdotal and subject to any whim.

How do we know what was picked is not some unrepresentative extreme that covers for NECTA's incompetency?
 
Mkirua hivi umeyaangalia yale maswali kweli au unaamua kubisha tu? Yale maswali mengi waliyoyaweka yanahitaji analytical skills ambazo sidhani kwa mtoto wa kidato cha nne atakuwa nazo.

Sidhani kama umenisoma, mimi nakwambia kabla ya kujudge kuwa mtoto wa form four hatakuwa na analytical skills nenda kwenye muhtasari uone ni competency gani mwanafunzi anapaswa kuwa nazo ndipo uje hapa kuargue kuwa hilo swali limekosewa. Otherwise argument zako ni baseless.
 
Tatizo lipo kubwa kwa walimu.Walimu ni mbumbu sana hawana uwezo ,tatizo lingine ni lugha, ukisoma sample za reactions za wanafunzi utaona lugha nikichomi kubwa pia.

acha kuwatukana walim kwani wewe ulifundishwa na nani hadi hapo ulipo? Huwezi kugombana na mpishi ukategemea chakula kitamu. JIPANGE
 
Back
Top Bottom