BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wanyamapori wa aina 46 tofauti wameongezeka katika mfumo wa ikolojia ya Ruaha – Rungwa na Katavi – Rukwa baada ya kudhibitiwa kwa matukio ya ujangili.
Takwimu hizo zimebainishwa katika ripoti ya sensa ya wanyamapori ambayo imefanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri) kuanzia Septemba 21, 2021 hadi Octoba 10, 2021.
Katika sensa hiyo, imebainika kuwa Tanzania kuna idadi kubwa ya nyati kuliko nchi yoyote barani Afrika ambapo eneo la ikolojia la Nyerere, Selous na Mikumi lina nyati 66,546.
Utafiti huo umebaini pia ikolojia ya Katavi – Rukwa kuna nyati 35,273 na ikolojia ya Ruaha – Rungwa wamebainika nyati 20,911.
Akisoma matokeo ya sensa hiyo leo Novemba Mosi, 2022, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana amesema sensa hiyo imebaini uwepo wa aina 22 katika mfumo wa ikolojia wa Katavi – Rukwa.
Dk Chana amesema nyati wameongezeka hadi kufikia 35,273, kongoni 9,027, pundamilia 5,223, tembo 4,132, pofu 3,947 na ngiri 3,922.
Waziri Chana amesema katika mfumo wa ikolojia ya Ruaha – Rungwa pia wanyamapori aina 24 wamebainika ambapo wanyama walio wengi zaidi ni nyati ambao wapo 20,911, tembo 15,751, pundamilia 10,550, swala 8,643 na palahala 6,996.
Amesema katika sensa hiyo imebainika kuwa idadi ya tembo imeongezeka katika maeneo hayo, tofauti na sensa ya mwaka 2018 kutokana na kudhibitiwa kwa matukio ya ujangili.
Mtafiti Mkuu wa Tawiri, Dk Edward Kohi amesema sensa imefanywa katika maeneo ya hifadhi, mapori ya akiba, mapori tengefu na maeneo ya mapito ya wanyamapori.
“Tulikuwa na ushirikiano mzuri kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa), Kurugenzi ya wanyamapori na Wakala wa misitu (TFS) na taasisi binafsi za WCS na FZS,” amesema.
Wakizungumzia sensa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Dk Ernest Mjingo na Kamishna wa Uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema wamesema itasaidia serikali kujua idadi ya wanyama na changamoto zao.
Mwenyekiti wa bodi ya Tawiri, Dk David Manyanza amesema sensa hiyo, itasaidia pia mikakati ya kutangaza utalii na kukabiliana na ujangili.
MWANANCHI