Ripoti toka kwa Waadau mbalimbali kuhusu Ukatili wa Kingono kwa Watoto

Ripoti toka kwa Waadau mbalimbali kuhusu Ukatili wa Kingono kwa Watoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
LHRC (2020) "Kwa kipindi cha miaka 5 matukio ya ukatili wa kingono, ubakaji na ulawiti dhidi ya watoto yamekuwa yakiongezeka. Tangu mwaka 2015 hadi 2019 jumla ya makosa 36,940 ya ubakaji na ulawiti yaliripotiwa katika Vituo vya Polisi. "

LHRC (2020): "Kwa mwaka 2020 ni makosa 45 tu kutoka Mikoa 13 yalitolewa hukumu na Mahakama. Bado watu wa karibu na hawa watoto ndio wamekuwa wakifanya ukatili huu wa kingono ikiwemo walimu, walezi, ndugu na majirani na ukatili wa wao kwa wao"

CDF: Kwa mwaka 2020, uvunjwaji wa haki za watoto ulijikita katika ukatili wa kingono, vipigo, ukatili wa kihisia, utumikishwaji kazi, ndoa za utotoni na mimba za utotoni

CDF: Ukatili dhidi ya watoto ni ukiukwaji wa haki na ustawi wa mtoto licha ya kuwa na sheria na sera zinazomlinda mtoto mfano, Sheria ya Mtoto (2009), Mkataba wa Kimataifa wa Haki za mtoto na Mkataba wa Afrika wa haki na ustawi wa Mtoto, Sheria ya Elimu na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CDF: Ukatili wa kingono dhidi ya watoto ni vitendo vyovyote vinavyofanywa na mtu mzima dhidi ya mtoto (mtu mwenye umri chini ya miaka 18) au mtoto dhidi ya mtoto mwingine, ambapo mtoto hutumikishwa kingono.

CDF: Ukatili wa kingono dhidi ya watoto huhusisha ubakaji, ulawiti, utekaji na usafirishaji wa watoto kwa ajili ya ngono, matukio yote ya kumshika mtoto via vya uzazi ikiwa ni pamoja na uke, uume na matiti.

CDF: Ukatili wa kingono dhidi ya watoto unahusisha pia matukio ya uoneshaji video za ngono kwa watoto na matukio mengine yoyote yenye lengo la kutazama uchi wa mtoto, kumlaghai mtoto kwa njia yoyote ile kwa ajili ya kutumikishwa kingono.

CDF: Kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, umri wa ridhaa ya ngono ni kuanzia miaka 18 na kuendelea, hivyo vitendo vyote vya kingono vinavyofanywa dhidi ya mtoto hata kama mtoto huyo ameridhia kufanyiwa vitendo hivyo ni ukatili wa kingono na ni kosa la jinai ikiwemo ndoa za utotoni.

WHO (2020): Duniani kote, katika kila wasichana 10 wenye umri chini ya miaka 20, msichana 1 hupitia ukatili wa kingono kwa kulazimishwa kujamiiana au unyanyasi mwingine wa kingono

Mtoto aliyetendewa ukatili wa kingono mara nyingi hukosa amani na furaha, husononeka, kukosa kujiamini na kujithamini.
 
Mimi nikiona hizi ripoti kuhusu ukatili huu kwa watoto moyo wangu unapoa kabisa. Dah
 
Back
Top Bottom