Ripoti ya CAG 2021-2022: Mfuko wa Bima ya Afya Umepata Hasara ya Shilingi Bilioni 189

Kwa sasa michango ni ongezeko la 12% wakati matumizi ni zaidi ya 28%

Huu mfuko umeuawa na serikali kwa kuweka siasa, fedha wanayokatwa watumishi ni ndogo kulingana na huduma wanazopewa, serikali iongeze gharama angalau mtu atibiwe kwa daraja la jinsi anavyochangia.
Hivi sio kwamba watumishi ndio wanachangia kiasi kikubwa kulingana na hizi bima wanakata wananchi wengine!! Na hizo huduma kubwa wanazopata watumishi ni zipi ikiwa kuna limit? Na ukizingatia kuna wanaokatwa miaka na miaka na wala hawatibiwi!!!
 
Hii ni kweli kabisa na sidhani kama katika hili wataelewa,ila ki uhalisia Hospitali binafsi zinachangia kkwa kiasi kikubwa kuuwa mfuko wa Taifa wa bima ya afya.
Serikali ingejikita kwenye kuboresha huduma katika vituo vyake ili watu wasiende kwenye vituo vya watu binafsi bila sababu za msingi.
Hilo ndio la maana

Hospital zote za binafsi huinflate gharama
 
Hospitali binafsi ni wahuni balaa, nilimpeleka mtoto alikuwa na mafua na kikohozi. Akatumia tu ile stethoscope kumpima then akaandika mtoto ana tatizo za mafua na kikohozi. Shughuli ikaja kwenye dawa, aliandikiwa dawa kama aina tano hivi, nikizisoma zote ni antibiotics zenye matumizi sawa. Sikulipia hata dawa nikasepa.
 
Hivi sio kwamba watumishi ndio wanachangia kiasi kikubwa kulingana na hizi bima wanakata wananchi wengine!! Na hizo huduma kubwa wanazopata watumishi ni zipi ikiwa kuna limit? Na ukizingatia kuna wanaokatwa miaka na miaka na wala hawatibiwi!!!
Binafsi wanachangia pakubwa

Mtumishi wa mshahara wa kima cha chini ambacho ni 370,000 huchangia 266,000 kwa Mwaka

Mtumishi anayelipa zaidi ni yule anayelipwa kuanzia milioni 2
 
Hilo ndio la maana

Hospital zote za binafsi huinflate gharama
Na wanafanya makusudi,ukienda hospitali binafsi kama regency,Hindu Mandal, Besta....hutoki huko bila bill ya bima kufika si chini ya laki au laki mbili,utajaziwa dawa na vipimo mpka ushangae.
 
Bora hao wanakupa bill, kuna hospital hazitoi bill hivyo haujui umetibiwa kwa kiasi gani
 
Binafsi wanachangia pakubwa

Mtumishi wa mshahara wa kima cha chini ambacho ni 370,000 huchangia 266,000 kwa Mwaka

Mtumishi anayelipa zaidi ni yule anayelipwa kuanzia milioni 2
Na wananchi si ndio walikuwa na ile bima ya shilingi elfu30 kwa mwaka!! Sasa hapo nani kachangia zaidi?
 
Hospitali binafsi ni wahuni balaa, nilimpeleka mtoto alikuwa na mafua na kikohozi. Akatumia tu ile stethoscope kumpima then akaandika mtoto ana tatizo za mafua na kikohozi. Shughuli ikaja kwenye dawa, aliandikiwa dawa kama aina tano hivi, nikizisoma zote ni antibiotics zenye matumizi sawa. Sikulipia hata dawa nikasepa.
Hii Ishu ni nzito sana, serikali hapa inabidi wafumbe macho private,inabidi wapigwe pini
 
Tuambiwe hasara imepatikanaje? Isije kuwa wahasibu wa mfuko huo walilazimishwa kusaini hundi ili kutoa fedha kwenye mfuko huo kwa ajili ya shughuli zisizoza mfuko.
 
Bora hao wanakupa bill, kuna hospital hazitoi bill hivyo haujui umetibiwa kwa kiasi gani
Kadi namba 333334444444 imetumia Shilingi 351,500.00 kwa huduma za matibabu katika kituo cha gfgfgggg Hospital tarehe 25/02/2023. Kama taarifa hizi sio sahihi piga namba 199 bure kutoa taarifa NHIF.
 
Hii Ishu ni nzito sana, serikali hapa inabidi wafumbe macho private,inabidi wapigwe pini
Na hawana akili, huruma wala utu kwenye afya za watu. Unamrundikia mtu dawa bila kujali madhara ya hizo dawa kwa afya yake kweli!! Hapo daktari anakuwa muuaji.
 
Bora hao wanakupa bill, kuna hospital hazitoi bill hivyo haujui umetibiwa kwa kiasi gani
Bill huwa inakuja kwa njia ya sms kwenye namba ya simu ya mlipaji.
 
Kadi namba 333334444444 imetumia Shilingi 351,500.00 kwa huduma za matibabu katika kituo cha gfgfgggg Hospital tarehe 25/02/2023. Kama taarifa hizi sio sahihi piga namba 199 bure kutoa taarifa NHIF.
Hiyo sio bill, bill ni kama ile unapewa muhimbili, inaonesha huduma zote ulizofanyiwa
 
Na wananchi si ndio walikuwa na ile bima ya shilingi elfu30 kwa mwaka!! Sasa hapo nani kachangia zaidi?
Ile ilikuwa kituko, ile mwisho wake ni huko zahanati
 
Back
Top Bottom