Ripoti ya CAG: Ishara ya Uwazi wa Rais Samia

Anna Nkya

Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
69
Reaction score
341
Mijadala inaendelea kila mahali sasa hivi watu wakijadili yale yalioandikwa kwenye Ripoti ya CAG.

Kwa sehemu kubwa yanayojadiliwa ni madudu yaliyoko kwenye taasisi za umma.

Jambo la kufurahisha ni kwamba tayari kuna hatua zimeanza kuchukuliwa kuwawajijibisha waliotafuna pesa za Umma.

Wizara ya Nishati imetangaza kufukuzwa kwa vigogo wa TAN OIL, Wizara ya Fedha imesema waliohusika kwenye kuongeza fedha za manunuzi ya ndege watawajibika.

Lakini hii Ripoti ya CAG ni ripoti ya uwazi wa Rais Samia Suluhu kwa maana kwamba inaonesha jinsi gani yeye ni kiongozi anayependa uwazi.

Huko nyuma CAG alikuwa anaogopa kusema madudu ya Serikali, tunakumbuka kilichotokea kwa Assad. Lakini sasa Rais hana shida na kuambiwa ukweli.

Bila Rais kuruhusu uwazi, madudu yote haya yasingeonekana,

Bila shaka hatua zitafuata kwa kuzingatia sheria za Taznzania.
 
Sifa za kijinga kabisa, uwazi unatakiwa uwe kwenye ukamilishwaji wa miradi ya wananchi, na siyo uwazi wa kujionyesha ulivyo huna uwezo wa kuongoza hadi kusababisha ufisadi kila kona.
 
Mijadala inaendelea kila mahali sasa hivi watu wakijadili yale yalioandikwa kwenye Ripoti ya CAG.

Kwa sehemu kubwa yanayojadiliwa ni madudu yaliyoko kwenye taasisi za umma.

Jambo la kufurahisha ni kwamba tayari kuna hatua zimeanza kuchukuliwa kuwawajijibisha waliotafuna pesa za Umma.

Wizara ya Nishati imetangaza kufukuzwa kwa vigogo wa TAN OIL, Wizara ya Fedha imesema waliohusika kwenye kuongeza fedha za manunuzi ya ndege watawajibika.

Lakini hii Ripoti ya CAG ni ripoti ya uwazi wa Rais Samia Suluhu kwa maana kwamba inaonesha jinsi gani yeye ni kiongozi anayependa uwazi.

Huko nyuma CAG alikuwa anaogopa kusema madudu ya Serikali, tunakumbuka kilichotokea kwa Assad. Lakini sasa Rais hana shida na kuambiwa ukweli.

Bila Rais kuruhusu uwazi, madudu yote haya yasingeonekana,

Bila shaka hatua zitafuata kwa kuzingatia sheria za Taznzania.
Slogan feki ya eti 4Rs
1. Reconciliation-R
2. Reform-R
3. Restoration-R
4. Resilience-R
Yote hayo hapo juu katika uhalisia hayapo. Huwezi kuriadhiana na mtu binafsi ukaacha taasisi za kijamii na wananchi kama wangekuwa kwenye mtanziko ndio ungesema niridhiane nao lakini mtu fulani ili umwache afanye atakayo bila udhibiti ndio mariadhiano huku mtu huyo huyo akitumika kusulubu viongozi wa awamu iliyopita?
 
Back
Top Bottom