BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakati bado wananchi wakiwa kwenye sintofahamu ya nini kilitokea kwenye utaratibu wa kumaliza kesi za uhujumu uchumi uliotumika na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Hayati Rais Magufuli, swali jipya linaibuka zikiwa zimebaki siku chache mwezi Machi 2023 kumalizika na hakuna taarifa yoyote kuhusu ujio wa ripoti hiyo.
Ikumbukwe Rais Samia na CAG Kichere waliahidi mbele ya vyombo vya habari kuwa uchunguzi wa Plea Bargain umeanza na ripoti itatoka mwezi Machi 2023. Tumebaki na wiki moja tu hadi sasa wahusika hata hawagusii chochote.
Tuwakumbushe tu wenye mamlaka, Wananchi hawajasahau au kuipotezea ripoti hiyo. Wanaisubiri kwa hamu zote ili wajue zilipopelekwa fedha hizo ambazo zinadaiwa kuwa ni mabilioni kama sio trilioni kabisa. Rais Samia aliwahi kunukuliwa akisema uchunguzi ulionesha kuna fedha zilipelekwa China.