Ripoti ya CAG, kuna uwezekano Watanzania ni wajinga kushadadia kutibu matokeo badala ya kushughulika na chanzo?

Ripoti ya CAG, kuna uwezekano Watanzania ni wajinga kushadadia kutibu matokeo badala ya kushughulika na chanzo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala za kwa maslahi ya taifa.

Makala ya leo ni jinsi Watanzania wanavyoishadadia Ripoti ya CAG ya mwaka huu kushangalia ufisadi, as sasa ndio kuna ufisadi saana, kumbe kwa miaka 10 mfululizo ripoti za CAG zinaonyesha ufisadi na tena nyingine ufisadi mkubwa kuliko huu ambao umepelekea mimi kujiuliza kuwa je, kuna uwezekano sisi Watanzania ni ignorants, fools and very stupid?

Preamble
Mtu mwenye akili na mwenye busara anapojikwaa na kuanguka, anaangalia mahali alipojikwaa ili kuipata sababu iliyomfanya ajikwae na kuanguka, badala ya kuangalia alipoangukia tuu, anaamka na kuendelea na safari yake. Hivyo huko mbele anaweza kuja kujikwaa tena pale pale alipojikwaa mwanzo na kuanguka tena pale pale na this time sio akaukwaa na akaanguka tuu, hivyo kuinuka, kujifuta vumbi na kuendelea na safari yake, this time anaweza kujikwaa akaanguka na kutumia hata akashindwa kuinuka na kuendelea na safari yake, hivyo safari ikaishia hapo!.

Hii Ripoti ya CAG ni ripoti ya matokeo tuu wakati tumeshapigwa na sio chanzo. Siku zote tunasisitiza ili Tanzania tupate maendeleo ya kweli we need an effective system yenye maximum transparency and accountability, kudhibiti kabla hatujaibiwa na sio mnaipa fedha mijizi, mnaiangalia jinsi inavyotafuna, kisha ndio mnakuja kukagua na kutoa Ripoti ya CAG ya ukaguzi kuonyesha tumeibiwa.

The role ya CAG kama Mdhibiti ni nini? Mbona bado tunaibiwa tuu na kuendelea kufanywa shamba la bibi?

Tena ripoti yenyewe ya CAG ya mwaka uliopita sio mbaya kama ripoti nyingine za CAG za nyuma lakini watu wanashadia na wanashupalia matokeo badala ya kujiuliza chanzo cha madudu haya ni nini na nani? Huu kama sio ignorance, foolishness na stupidity ni nini hiki?

Je, Watanzania ni Ignorants, fools and stupid? Yaani Sisi Watanzania ni Wajinga ma Wapumbavu?

Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "Ma-ignorants!", fools na stupid kabisa, yaani wengi wetu vichwani ni watupu kabisa, empty shells, na wengine wetu ni vichwa maji kabisa. Uwezo wa kufikiri (ogical thinking) na kufanya tafakuri tunduizi (critical analysis) wa wengi wetu ni mdogo au sifuri, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya maana kwa wakati sahihi (to make informed decisions), hali inayopelekea ripoti za CAG kila mwaka kuwa na madudu yale yale mwaka hadi mwaka. Halafu ripoti ya mwaka huu watu ndio wanajifanya wakali, wanashangaa!

Kila ripoti ya CAG inaandamana na mapendekezo ya CAG, Bunge letu linajadili na kutoa Azimio la Bunge, na kuipeleka serikalini kwa utekelezaji, and that's done. There is no follow up ya utekelezaji wala hakuna mrejesho wa nini kimetekekezwa, mpaka ripoti ya CAG ya mwaka inayofuata na madudu yale yale yakijirudia, huu kama sio ujinga ni nini?

Tena tunapelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe au mazuzu kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi na kushupalia vitu vidogo vidogo ambavyo ni non issues na immaterial ambazo sio chanzo bali ni matokeo tuu. Badala ya kudeal na real issues halisi zenyewe ambazo ndicho chanzo, cha haya madhila, kilichopelekea haya yatokanayo yatokee, vyanzo havitafutwi, haviuliziwi, havishungulikiwi, havizungumzwi, haviguswi, tuna deal na matokeo tuu!

Mwisho wa siku kuja kuvikamata vidagaa tuu, lakini mapapa na makambale, ya chanzo cha the grand Corruption hawaguswi, ni untouchable, huu kama sio ujinga ni nini?
Mimi ni mtu wa mastori mastori, kama wewe sio mtu wa mastori, then jump to conclusions, wale wa mastori ya Pasco Tuendeleeni.

Ujinga huu wa Watanzania, kutojiuliza chanzo cha tatizo umeanzia wapi na uko wapi?

Hii ignorance, foolishness na stupidity ya baadhi ya Watanzania kushadadia matokeo ya kuibiwa kwa kupiga sana kelele kuwa "Tumeibiwa" badala ya kudeal na chanzo kuzuia tusiibiwe, ina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya Bunge letu tukufu.

Tuna wabunge mule ni vilaza fools and ignorants wa ajabu hakuna mfano! Ndio maana Mbunge anasoma headline ya gazeti, gazeti limeandika Bunge linajipendekeza kwa serikali? M mbunge kilaza haoni alama ya kuuliza, anasimama Bungeni na gazeti na kumuomba Mhe. Spika muongozo kuwa Bunge limedhalilishwa! Mbunge kama huyu, ukiwaita baadhi ya wabunge wetu ni vilaza, utakuwa umewakosea?, Spika nae anakuwa mkali kweli kweli Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge


Tuna baadhi ya viongozi wetu wengi tuu ni ma ignorants, fools and stupid sana hadi ndani ya cabinet yetu, kuna baadhi ya mawaziri wetu ni ma ignorants na stupid kabisa! Uthibitisho ni jinsi baadhi ya mawaziri wetu wanavyo vurunda hivyo wengine kutimuliwa na wengine kutumbuliwa kila uchao.

Count the number of mini reshuffles from time to time, hii ni kutokana na udhaifu kwenye vetting wanampelekea Rais Samia mabomu na Mama anateua. Kuna mawaziri kwenye some few key miniseries ni misfits hivyo soon itafanyika tena reshuffle, na kufuatia uhaba wa capable people, tegemea recycling.

Kwenye hili la udhaifu wa uteuzi, naomba nimuwekee Mama caveat Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Tuna baadhi viongozi wa taasisi za umma ambao ni ma ignorants, fools and very stupid, na jambo kubwa na la ajabu, tuna hadi viongozi wetu wakuu wa taasisi nyeti na hadi baadhi ya wakuu wa vyombo vya dola, kitu ambacho ni hatari sana, na kuna kipindi (kimepita) hadi baadhi ya wakuu wa mihimili, jambo ambalo ni very dangerous na very risky kwa our national security.

Hii ignorance imekata across the society yetu left, right and centre hadi sisi wana JF pia, wengine wetu humu ni ma ignorants, fools and very stupid people, nikiwemo mimi mwana JF, mwenzenu Paskali, pia ni ignorant, fool na stupid fulani!

Mtu mwenye akili zake timamu hawezi kuuliza maswali magumu hivi kwa viongozi wake! Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Je, mtu kuwaita Watanzania wenzako kuwa ni wajinga, ignorants, fools and stupid ni kuwatukana?

Kumuita mtu yoyote kuwa ni mjinga, ignorant, fool and stupid, kama huyo mtu sio hivyo, then huko ni kumtukana, lakini kama mtu ni kweli ni mjinga, ni stupid, ni fool, na very stupid, kumuita hivyo sio kumtukana ni kumwambia ukweli.

Naomba kuweka wazi kuwa kwenye bandiko hili, sijamtukana mtu yoyote wala sijawaita watu ni humu kuwa ni wajinga, ignorants, fools and stupid, bali nimeuliza tuu swali kuwa, Je, aisi Watanzania ni wajinga, ignorants, fools and stupid?

Majibu ya swali hili ndiyo yatakayosema kama sisi ni ma ignorants, fools and stupid au la! Kama ni ma ignorants, huu ujinga wetu ni ujinga wa aina gani au tumelogwa? Maswali haya ni kufuatia kujiuliza, haiwezekani kabisa, kwa watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ovyo ya ajabu ajabu kama haya kwenye ripoti ya CAG ya mwaka hadi, mwaka kwa kufanyiwa madudu yale yale.


Conclusion and Recommendations
CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za fedha za serikali.
Utaratibu wa matumizi ya fedha za serikali kutoka mfuko Mkuu hazina ni huu;
  1. Wizara, Idara na Wakala, zinatumia fedha za Mfuko Mkuu wa Hazina, hutuma maombi fedha za bajeti zao serikalini katika mafungu mawili, 1. Recurrent expenditure 2. Development budget.
  2. Hupeleka bajeti hizo serikalini kwa the Councillor of the exchequer (MOF) ambapo Recurrent hupitishwa kama ilivyo.
  3. Kwenye recurrent upigaji ni mdogo, ukiondoa mishahara hewa, upigaji wa huku ni petty corruption ya kila mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake, just 10% kwa kuongeza kitu kidogo cha juu ambapo GIPSA imesaidia sana kupitia taneps.
  4. Development budget huangalia chungu kinaruhusu kupitisha bajeti ya kiasi gani na hapa ndipo madudu yote kufanyika na huku ndiko kwenye the grand Corruption.
  5. Siku zote Tanzania tunapanga bajeti ya kutumia fedha ambazo hatuna na matokeo yake ni kutemea makosanyo, mikopo na ufadhili.
  6. Siku zote baada ya hatuna ya Bajeti kusomwa wabunge wote hushangilia!, kila nikiangalia wanachoshangilia sikioni nikauliza huku sio kushangilia ujinga?
  7. CAG Prof. Assad akatoa ushauri wa maana sana lakini akapuuzia.
  8. Baada ya Exchequer kupitisha bajeti, bajeti hizo hupelekwa Bungeni kujadiliwa kupitishwa na kuidhinishwa.
  9. Hapa sasa ndipo the role ya Mdhibiti huanzia, fedha haziwezi kutolewa ndani ya mfuko Mkuu wa Hazina bila ya mdhibiti kuridhia.
  10. Mfano bajeti ya ununuzi wa ndege iliyoidhinishwa na Bunge ni kiasi kadhaa, fedha kabla hazijatoka lazima CAG aidhinishe na huo ndio Udhibiti.
  11. Fedha pekee kutoka mfuko Mkuu wa Hazina zinazotolewa bila idhini ya CAG ni fedha za dharura na maafa tuu.
  12. Na baada ya CAG kuidhinisha matumizi ndipo hupita kila taasisi kufanya auditing na kutoa Ripoti ya CAG.
  13. Kama CAG ndie muidhinishaji, iweje aidhinishe matumizi zaidi ya approved budget?!
  14. Sasa zaidi ya Ripoti ya CAG ya ukaguzi, lets demands
  15. Ripoti ya Udhibiti tuone CAG alidhibiti nini kikapuuzwa watu wakapiga pesa!
  16. Ripoti ya value for money kwa sio tuu kwa kila projects, hata kwenye Recurrent expenditure. Kuna tenda za common user items zina bei za ajabu.
  17. Sio kila ongezeko la bei ni upigaji. Ongezeko jingine la bei ni genuine
  18. Sio kila ripoti chafu ya ukaguzi lazima ni upigaji, sometimes ni ukiukwaji tuu wa taratibu.
  19. Na sio kweli kila audit queries za CAG hazijajibiwa, nyingine zimeisha jibiwa ila ni baada ya exit meeting hivyo ripoti hazionyeshi delivery na mfano mzuri ni ile tenda ya uniform za polisi, by the time ripoti ya CAG imetoka, ikasema polisi wamelipia bilioni 4 kununua mzigo hewa, kumbe mzigo uliisha ingia na yule bidada supplier akavuta mabilioni yake akayamwaga kwa wajumbe wa Kawe, akaongoza kura za maoni za Kawe, Blaza akamchinja na kutupatia yule tapeli kwasababu ni ...
  20. Hivyo natoa wito kwa CAG aongezwe bajeti, afanye Udhibiti kabla hatujapigwa na tupate ripoti ya Udhibiti na sio ya ukaguzi pekee!.
Paskali
 
Subiria matusi kutoka Kwa hao wapumbavu...

Mtu hata kusoma ripoti vizuri hasomi...
Ripoti inasema upigaji WA mwaka 2020...kuna maeneo ripoti ni ya past seven years...lakini anataka kukomaa na waziri wa sasa na Viongozi wa sasa bila kujiuliza why mambo ya miaka mitatu Hadi Saba yanatolewa Leo? Why hayakutolewa miaka mitatu nyuma?

Ukijaribu kuwaelewesha ni matusi na mihemko tu
 
Kwa Mujibu wa Mshana Jr anasema Nchi hii ina makafara matatu makubwa ila hili linalozunguka kila mahali ndiyo inasemekana linawafanya Watanzania kuwa hivi walivyo.

Watanzania ni kondoo wa kuona mali za Umma zinaibwa hata hawapigi kelele, mkihamasishana kuandamana kupinga Mapolisi wanatumika kuwapiga Wananchi Vilungu kwa Maslahi ya hao Wezi.

Ukiwasema humu mitandaoni wanajitokeza Chawa wao kukujibu eti unawaonea Wivu matajiri walioiba mali za Umma na kufungua miradi ya Mabasi, Viwanda, Migodi n.k
 
Mtoa mada umeeleza uhalisi wa watanzania wengi hasa hawa so called middle class, wengi wao ni watu wanaozichukulia Habari kama kikosi cha zimamoto, moto ukitokea address A wanakimbia kule na once moto ukishazimwa wana move on,tiba ya yote haya ni KATIBA MPYA, maana itaifanya taasisi hii ya mkaguzi mkuu kuwa na meno zaidi, na pia itatupa taasisi kama FBI pale US ambayo taarifa kama hii wataifanyia uchunguzi na kuweza kuwapeleka mahakamani suspects wote, welldone Adv.Mayala kwa mada safi
 
MkuuPaskali makala ndefu ila ujumbe/hoja yako ni ileile ambayo umeitoa kwenye bandiko lingine humu JF kwamba hakuna mifumo ya ufuatiliaji, ukaguzi na udhibiti. Jibu langu SIYO KWELI.

Kila Taasisi na Serikalini kuna "Internal Audits" ambazo moja ya kazi zake ni udhibiti. Swali ni kwa nini hazitimizi wajibu wake?

Narudia tena, ukaguzi wa CAG siyo wa siri, iweje viongozi husika kutokuchukua hatua pale madudu yanapochimbuliwa na CAG?

Mimi naamini Mamlaka za Uteuzi hazitimizi wajibu wake ipasavyo.
 
Naunga mkono hayo majizi kuendelea kupora, maana wanapora uchaguzi kisha tunawasifia kuwa CCM ni bonge la chama na ulitawala milele. Tunashangaa wanaibaje wakati wanaingia madarakani kwa wizi wa wazi? Tena hapo ni kama wameiba kidogo, wapore za kutosha maana hizi ni fedha za maiti hai.
 
MkuuPaskali makala ndefu ila ujumbe/hoja yako ni ileile ambayo umeitoa kwenye bandiko lingine humu JF kwamba hakuna mifumo ya ufuatiliaji, ukaguzi na udhibiti. Jibu langu SIYO KWELI.

Kila Taasisi na Serikalini kuna "Internal Audits" ambazo moja ya kazi zake ni udhibiti. Swali ni kwa nini hazitimizi wajibu wake?

Narudia tena, ukaguzi wa CAG siyo wa siri, iweje viongozi husika kutokuchukua hatua pale madudu yanapochimbuliwa na CAG?

Mimi naamini Mamlaka za Uteuzi hazitimizi wajibu wake ipasavyo.

Hayo ndiyo madhara ya watu kuingia madarakani kwa kunajisi box la kura. Katika mazingira hayo huwezi kukuta taasisi yoyote ikiwajibika ipasavyo, kwani kuanzia rais hadi viongozi wa chini yake ni tunda la wizi wa uchaguzi.
 
MkuuPaskali makala ndefu ila ujumbe/hoja yako ni ileile ambayo umeitoa kwenye bandiko lingine humu JF kwamba hakuna mifumo ya ufuatiliaji, ukaguzi na udhibiti. Jibu langu SIYO KWELI.

Kila Taasisi na Serikalini kuna "Internal Audits" ambazo moja ya kazi zake ni udhibiti. Swali ni kwa nini hazitimizi wajibu wake?

Narudia tena, ukaguzi wa CAG siyo wa siri, iweje viongozi husika kutokuchukua hatua pale madudu yanapochimbuliwa na CAG?

Mimi naamini Mamlaka za Uteuzi hazitimizi wajibu wake ipasavyo.
Tatizo hapa mkuu hatuna utamaduni wa uwajibikaji, hawa waliopewa majukumu wanajua kuwa once umeteuliwa u can do anything with pure impunity, na pia ni lazima hawa CEOs wawajibike kwa Bunge na waombe kujaza hizi post sio kutegemea fadhila za uteuzi wa no 1,na TISS &Jeshi letu la police lifumuliwe na tulijenge upya na tuwe na special units ndani ya jeshi letu la police.
 
PASKALI unataka tuangalie tulipojikwaa badala ya kutazama tulipoangukia, ukiwa na maana kwamba tutazame sheria zetu zinawabana vipi watendaji ili wasije kutuibia, badala ya kuwapa mihela tukijua kwamba lazima watatuibia...

Sasa kama hizo sheria za kuwabana wezi hazipo, na shughuli za kiserikali bado zinaendelea, unataka tuache kulalamikia wizi uliotokea, ili badala yake tuendelee kupigwa tu mpaka pale zitakapopatikana hizo sheria za kuwabana?

Unamaanisha kwasababu hatuna hizo sheria basi ndio tumuachie fisi bucha!, hebu punguza jazba, lazima kelele zipigwe hata kama sheria hazipo, kwasababu mwizi akienda kuiba kwenye nyumba ya mwenye mbwa, kubweka kwa mbwa kutambana asiibe kwa uhuru hata kama huyo mbwa hana meno.
 
Pasco ni mmoja wa members ambao kuna watu wengi humu jukwaani hoja zako uzitumia kama sehemu ya ufahamu wao na premise ya kujengwa arguments zao sehemu zingine kuhusu topic husika.

Mtu akichukua wrong premise kutoka kwako kama sehemu ya arguments zake na yeye conclusion yake aiwezi kuwa sahihi; na kuongeza kitu unachoita ignorance ndani ya jamii.

Busara ni kufanya ata kiji-research kwanza kuhusu mamlaka ya CAG hana hiyo nafasi ya kujulishwa everyday kuhusu matumizi ya serikali; yeye anakagua tu matumizi yao kama yapo sawa kuangalia (Fair Value).

Kwenye auditing kuna concept inayofahamika kama ‘audit expectation gap’. Inaelezea mkanganyiko wa uelewa ndani ya jamii kati ya nini hasa kazi wanazofanya auditors pamoja na majukumu, tofauti na watu wanavyodhania majukumu yao. Ni jukumu la auditors kutoa hiyo elimu na mara nyingi CAG’s wamekuwa wakiliezea hasa wa mwisho watatu kuanzia kwa Assad, mpaka kwa Kichere mara ya mwisho juzi wao wanachafanya.
 
Loo umetiririka vizuri ila miminatakujibu kwamba tatizo hili la upigaji wa pesa zetu halitaisha kama huu mfumo wa utawala ulioko Sasa hautabadilishwa.

Wa kuibadilisha huu mfumo ni sisi na wewe uliwepo.

Ni kuibadilisha kupitia sanduku la kura. Kabla ya kuubadilisha huu mfumo ni lazima kwanza tudai katiba mpya na time huru ya uchaguzi.

Kwa bahati mbaya wewe mwenzetu ni muungaji mkono wa mfumo uliopo, Sasa mpaka hapo fools , ignorants and stupid ni nani?
 
Chanzo cha upigaji na wizi ni CCM.
Na ni chama cha mleta uzi.Haeleweki.Kama analaumu.Kama anashangaa huku anatukana.Kama hataki walaumiwe.Ni kama hataki wala kupenda watu walaumu,waipende ripoti ilivyoibua madudu kwa muda huu.Ni kama anataka lawama,manung'uniko yangeanza miaka 20 iliyopita.Na andiko refu lenye kujichanganya tu kwa kujipiga lenyewe kuanzia mwanzo tu.
 
Ufisadi na wizi upo serikalini, lakini sio mkubwa kama anavyoainisha CAG. ripoti yake ina mapungufu makubwa, na kama serikali ikifuata ushauri wake kwa 100% shughuli nyingi za serikali zitakwama.

Wenye uzoefu na ukaguzi wanajua, ukiona auditor ameibua kasoro nyingi sana au hajaona kasoro yoyote, ujue huyo anashida, na hawezi kukusaidia kuboresha chochote.

Maboresho ni 'incremental process' hatua kwa hatua, na ndio maana wakaguzi wabobevu wanaibua kasoro chache ambazo ni critical kwanza, kisha zinafuatiliwa kwa ukaribu kuona kuwa zimefanyiwa kazi, baada ya hapo anaendelea na nyingine.
 
Back
Top Bottom