Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala za kwa maslahi ya taifa.
Makala ya leo ni jinsi Watanzania wanavyoishadadia Ripoti ya CAG ya mwaka huu kushangalia ufisadi, as sasa ndio kuna ufisadi saana, kumbe kwa miaka 10 mfululizo ripoti za CAG zinaonyesha ufisadi na tena nyingine ufisadi mkubwa kuliko huu ambao umepelekea mimi kujiuliza kuwa je, kuna uwezekano sisi Watanzania ni ignorants, fools and very stupid?
Majibu ya swali hili ndiyo yatakayosema kama sisi ni ma ignorants, fools and stupid au la! Kama ni ma ignorants, huu ujinga wetu ni ujinga wa aina gani au tumelogwa? Maswali haya ni kufuatia kujiuliza, haiwezekani kabisa, kwa watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ovyo ya ajabu ajabu kama haya kwenye ripoti ya CAG ya mwaka hadi, mwaka kwa kufanyiwa madudu yale yale.[/SIZE]
Conclusion and Recommendations
CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za fedha za serikali.
Utaratibu wa matumizi ya fedha za serikali kutoka mfuko Mkuu hazina ni huu;
- Wizara, Idara na Wakala, zinatumia fedha za Mfuko Mkuu wa Hazina, hutuma maombi fedha za bajeti zao serikalini katika mafungu mawili, 1. Recurrent expenditure 2. Development budget.
- Hupeleka bajeti hizo serikalini kwa the Councillor of the exchequer (MOF) ambapo Recurrent hupitishwa kama ilivyo.
- Kwenye recurrent upigaji ni mdogo, ukiondoa mishahara hewa, upigaji wa huku ni petty corruption ya kila mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake, just 10% kwa kuongeza kitu kidogo cha juu ambapo GIPSA imesaidia sana kupitia taneps.
- Development budget huangalia chungu kinaruhusu kupitisha bajeti ya kiasi gani na hapa ndipo madudu yote kufanyika na huku ndiko kwenye the grand Corruption.
- Siku zote Tanzania tunapanga bajeti ya kutumia fedha ambazo hatuna na matokeo yake ni kutemea makosanyo, mikopo na ufadhili.
- Siku zote baada ya hatuna ya Bajeti kusomwa wabunge wote hushangilia!, kila nikiangalia wanachoshangilia sikioni nikauliza huku sio kushangilia ujinga?
- CAG Prof. Assad akatoa ushauri wa maana sana lakini akapuuzia.
- Baada ya Exchequer kupitisha bajeti, bajeti hizo hupelekwa Bungeni kujadiliwa kupitishwa na kuidhinishwa.
- Hapa sasa ndipo the role ya Mdhibiti huanzia, fedha haziwezi kutolewa ndani ya mfuko Mkuu wa Hazina bila ya mdhibiti kuridhia.
- Mfano bajeti ya ununuzi wa ndege iliyoidhinishwa na Bunge ni kiasi kadhaa, fedha kabla hazijatoka lazima CAG aidhinishe na huo ndio Udhibiti.
- Fedha pekee kutoka mfuko Mkuu wa Hazina zinazotolewa bila idhini ya CAG ni fedha za dharura na maafa tuu.
- Na baada ya CAG kuidhinisha matumizi ndipo hupita kila taasisi kufanya auditing na kutoa Ripoti ya CAG.
- Kama CAG ndie muidhinishaji, iweje aidhinishe matumizi zaidi ya approved budget?!
- Sasa zaidi ya Ripoti ya CAG ya ukaguzi, lets demands
- Ripoti ya Udhibiti tuone CAG alidhibiti nini kikapuuzwa watu wakapiga pesa!
- Ripoti ya value for money kwa sio tuu kwa kila projects, hata kwenye Recurrent expenditure. Kuna tenda za common user items zina bei za ajabu.
- Sio kila ongezeko la bei ni upigaji. Ongezeko jingine la bei ni genuine
- Sio kila ripoti chafu ya ukaguzi lazima ni upigaji, sometimes ni ukiukwaji tuu wa taratibu.
- Na sio kweli kila audit queries za CAG hazijajibiwa, nyingine zimeisha jibiwa ila ni baada ya exit meeting hivyo ripoti hazionyeshi delivery na mfano mzuri ni ile tenda ya uniform za polisi, by the time ripoti ya CAG imetoka, ikasema polisi wamelipia bilioni 4 kununua mzigo hewa, kumbe mzigo uliisha ingia na yule bidada supplier akavuta mabilioni yake akayamwaga kwa wajumbe wa Kawe, akaongoza kura za maoni za Kawe, Blaza akamchinja na kutupatia yule tapeli kwasababu ni ...
- Hivyo natoa wito kwa CAG aongezwe bajeti, afanye Udhibiti kabla hatujapigwa na tupate ripoti ya Udhibiti na sio ya ukaguzi pekee!.
Paskali