Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Ukaguzi wa kiufundi wa ufungaji na matengenezo ya vifaa vya barabarani na ishara za mawasiliano ya barabara uliofanywa kwa TANROADS na TARURA umebaini mapungufu katika upangaji wa miradi, usimamizi wa mikataba, na matengenezo, hali ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa usalama wa barabara na ufanisi wa mfumo wa usafirishaji.
Miundombinu ya alama za barabarani katika makutano muhimu jijini Dar es Salaam imepitwa na wakati, hali iliyosababisha hitaji la udhibiti wa foleni kwa mikono kupitia askari wa usalama barabarani. Aidha, ukosefu wa bajeti ya kutosha umekwamisha juhudi za matengenezo, ambapo Shilingi bilioni 1.8 hutengwa kwa mwaka ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Shilingi bilioni 200.
Pia, nilibaini upungufu wa alama za barabarani, ambapo Barabara ya Bagamoyo ina upungufu wa taa za barabarani kwa 73%, ilhali mistari ya barabarani iliyofifia na ukosefu wa alama za barabara vikiongeza hatari za ajali. Udhibiti wa ubora haukuwa wa kuridhisha, kwani rangi za alama za barabarani hazikupimwa kama inavyotakiwa, hali inayohatarisha uimara wake kwa muda mrefu.
Uharibifu wa vifaa vya barabarani kwenye Barabara ya Tabora-Nzega na barabara za Mji wa serikali Dodoma umesababisha hasara ya Shilingi milioni 170.48, huku udhaifu wa hatua za ulinzi ukichangia ongezeko la wizi wa vifaa hivyo.