RIPOTI YA CAG:TASAF, TANROADS ZAKALIA MAMILIONI YA FEDHA ZA WANANCHI

RIPOTI YA CAG:TASAF, TANROADS ZAKALIA MAMILIONI YA FEDHA ZA WANANCHI

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
413
Reaction score
471
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/22, imebaini hundi zilizochacha zenye thamani ya Sh352.12 milioni zilitolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kwa waathirika wa miradi miwili mkoani Dodoma.

Hali kadhalika, CAG alibaini kuchelewa kulipa fidia kwa waathirika wa miradi ya Shi1.7 bilioni kwa waathirika wa miradi iliyoko chini ya Tanroads. Mbali na hilo, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) haukupeleka Sh651.85 milioni zilizoidhinishwa kwenda kwenye miradi tisa katika Wilaya za Ludewa na Makete mkoani Njombe kwa watu 186 wanaoishi katika kaya hatarishi.

Katika ripoti ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya mwaka 2021/2022 iliyowasilishwa juzi bungeni, CAG Charles Kichere aliitaja miradi ambayo waathirika walipata hundi zilizochacha ni mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato na Barabara ya Mzunguko wa nje katika Jiji la Dodoma kwa Kiwango cha lami (112.3)


Alisema kanuni za fedha za umma za mwaka 2001 (zilizorekebishwa 2004) zinahitaji kulinganishwa kwa taarifa za kibenki na daftari la fedha husika kila mwezi na kuwa hundi iliyochacha hutambuliwa ikiwa haijawasilishwa benki kwa malipo kwa siku zinazozidi 180 au miezi sita.

Alisema hivyo, hundi iliyochacha huwa haiwezi kulipwa na benki, lakini ukaguzi wake ulibaini hundi zilizochacha zilizo- tolewa kwa waathirika wa miradi zenye thamani ya Sh352.12 milioni. Alisema hali hiyo, ilisababishwa na uwepo wa malalamiko na migogoro baina ya waathirika wa miradi ambayo ilisababisha kutochukua hundi hizo zilizoandikwa kwao kwa ajili ya malipo.

"Ninapendekeza Wakala wa Barabara kuwasiliana na waathirika wa miradi na kuwapatia hundi zao kwa wakati bila kuchelewa zaidi,"Alisema

Ucheleweshaji wa fidia

Kichere alisema alibaini kuna ucheleweshaji wa kulipa fidia kwa waathirika wa miradi ambapo Sh11.37 bilioni zilizopaswa kulipwa katika miradi mitatu iliyo chini ya Tanroads zimecheleweshwa.

Alibaini Sh512.34 milioni zilizokuwa zitolewe kwa waathirika wa mradi wa ujenzi wa barabara ya kimataifa Ya Bagamoyo-Horohoro /Lunga - Lunga-Malindi unaotekelezwa na Tanroads hazikulipwa kwa waathirika wa mradi422.

Alisema hali hiyo ilitokana na mchaka-to mrefu wa malipo ya fidia kwa waathiri-ka wa miradi na hivyo kushindwa kulipa fidia kwa waathirika wa mradi ndani ya miezi sita.

Pia alibaini mradi wa miundombinu ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) awamu ya pili unaotekelezwa na Tanroads ulikuwa na madai ya fidia yenye thamani ya Sh4.63 bilioni kwa waathirika 15 wa mradi kwa zaidi ya miaka miwili.

Kichere alisema ulibaini madai ya fidia kwa waathirika 1,039 wa mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato yenye thamani ya Sh6.22 bilioni ikiju-muisha madai halisi Sh3.92 bilioni na riba ya Sh2.3 bilioni hayajalipwa.

"Kuchelewesha malipo ya fidia kwa waathirika wa miradi kunasababisha Serikali kulipa riba isiyostahili
ya ucheleweshaji ambayo ingeweza kuepukwa kwa kulipa fidia kwa wakati kulingana na ripoti ya tathmini ya mwa-ka 2011," alisema.

Alipendekeza Tanroads kuharakisha malipo ya fidia kwa waathirika wa miradi yenye thamani ya Sh11.37 bilioni kwa waathirika wa miradi 1,476.

Kaya hatarishi hazikulipwa

Kichere alibaini Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) haukupeleka Sh 651.85 milioni zilizoidhinishwa kwenda kwenye miradi tisa katika Wilaya za Ludewa na Makete mkoani Niombe kwa watu 186 wanaoishi katika kaya hatarishi.


CAG alisema Tasaf inatekeleza mradi Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) kwa jumla ya wanufaika 186 wanaoishi kwenye kaya hatarishi katika wilaya hizo mbili.
 
Wazee na kaya masikini wanataabika huko halafu kuna watu wanakalia hela zao kweli jamani huu ni ubinafsi mkubwa sana, mama nyoa hao
 
TANROADS ya sasa "imerelax" wakandarasi nao "wamerelax" hakuna "pressure" ni mwendo wa "business as usual".

Barabara kubwa ya njia nne kuanzia kimara mwisho mpaka kibaha inakosa hata taa za barabarani!!!??? paia barabara ya mwendo Kasi hadi Leo imesimama!!!
 
Back
Top Bottom