Ripoti ya makusanyo ya mapato kwa kipindi cha robo ya tatu (Januari-Machi) mwaka wa fedha 2022/2023

Ripoti ya makusanyo ya mapato kwa kipindi cha robo ya tatu (Januari-Machi) mwaka wa fedha 2022/2023

TRA Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
128
Reaction score
370
MAKUSANYO 1.jpg
MAKUSANYO 2.jpg
 
Kukusanya siyo shida, shida matumizi yake

Mkatawanye kwa mafisadi tena? Inauma sana, ila Hongereni kwa kazi nzuri
 
Bado tupo kwenye wastani wa 15.5% ya GDP.... tunafeli wapi? Kiuhalisia hakuna ongezeko lolote, tupo pale pale. Tufike angalau 20% ambayo itakuwa almost 32 Trillioni.
 
Hongera TRA kwa kutoa taarifa JF.

Bado napendekeza usimamizi wa tiketi za mabasi uimarishwe. TRA ishirikiane na Jeshi la Polisi maeneo ya stendi au njiani kufanya ukaguzi wa kushtukiza. Bado hawatoi tiketi hizo.

Pia napendekeza ukusanyaji wa Kodi ya ardhi usimamiwe na TRA kwa niaba ya Wizara ya Ardhi, ilipwe katika mfumo wa LUKU, angalau kwa maneneo maalum kama kariakoo, Masaki, mikocheni, mbezi, baadae usambae kwa wengine in phases.

Pia ufanyike uhakiki wa mashamba makubwa yote nchi nzima kwa mfumo wa kidigitali, uzoefu unaonyesha wamiliki wa mashamba wanalipia ardhi kidogo wakati ardhi waliyonayo ni kubwa. Pitia mashamba ya chai, miwa, na mengineyo.

Pia utafiti ufanyike ili mfanyabiashara alazimike kuwa na LIPA NAMBA, ambayo asilimia fulani ya mauzo yake atumie mfumo huo.

Kwa udhibiti wa biashara kariakoo, uimarishwe, pale bado mapato yanavuja.

Napendekeza stendi zote, mabasi yawe na kadi maalum za kulipia malipo ya stendi, anakuwa anachanja, inakata Hela, geti linajifungua lenyewe. Na kama atakwepa kupita katika kituo, basi ijikate automatically kwenye mfumo.
 
Hongera TRA kwa kutoa taarifa JF.

Bado napendekeza usimamizi wa tiketi za mabasi uimarishwe. TRA ishirikiane na Jeshi la Polisi maeneo ya stendi au njiani kufanya ukaguzi wa kushtukiza. Bado hawatoi tiketi hizo.

Pia napendekeza ukusanyaji wa Kodi ya ardhi usimamiwe na TRA kwa niaba ya Wizara ya Ardhi, ilipwe katika mfumo wa LUKU, angalau kwa maneneo maalum kama kariakoo, Masaki, mikocheni, mbezi, baadae usambae kwa wengine in phases.

Pia utafiti ufanyike ili mfanyabiashara alazimike kuwa na LIPA NAMBA, ambayo asilimia fulani ya mauzo yake atumie mfumo huo.

Kwa udhibiti wa biashara kariakoo, uimarishwe, pale bado mapato yanavuja.
Ili lifanikiwe yatakiwa Machinga nao wapewe EFD, tofauti na hilo bado zitaendelea vuja maana mwenye duka atatafuta ndugu yake, kisha atampa vitu auze jioni ampe pesa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kabisa, vinginevyo inabidi bidhaa ambazo zinaonekana kuuzwa sana na machinga, Kodi yake ipigwe hukohuko bandarini kupunguza hasara ya kukimbizana mitaani
 
Matumizi je!?

Mimi nalia na wale wa ndege tu, bado wako kazini? Mh. Rais alitoa amri watupishe, sijasikia mtu kajiuzulu hata mmoja, hawa watu wanamdharau Mh. Rais nini? Hao walita kuiba hela ndio matumizi ya wizi na ufisadi mkubwa sana from $ 37 mil to $ 86 mil walikongeza $ 49 mil sawa na ongezeko la tshs 135 bilioni.. Huu ni ufisadi mkubwa sana sanana, laana kuu iwauwe hao wezi wa kalamu.
 
Nilichogundua huu mwaka naona ni mzuri kwa Tanzania,vijana ndipo simamisha biashara mwaka huu,jiandae kufa masikini.
 
Niisiwe muongo!..

Nikinunua kitu muuzaji hata asiponipa risiti sawa tu! Na wala huwa sihangaiki kudai.
.
Ya nini kukomaa kuumiza kichwa wakati hela zenyewe zinaenda huku?
Screenshot_20230329-152212_Telegram.jpg
 
Kwa hili ninaacha haya niliyoandika
Hongereni....kazi iendelee
 
Back
Top Bottom