Hongera TRA kwa kutoa taarifa JF.
Bado napendekeza usimamizi wa tiketi za mabasi uimarishwe. TRA ishirikiane na Jeshi la Polisi maeneo ya stendi au njiani kufanya ukaguzi wa kushtukiza. Bado hawatoi tiketi hizo.
Pia napendekeza ukusanyaji wa Kodi ya ardhi usimamiwe na TRA kwa niaba ya Wizara ya Ardhi, ilipwe katika mfumo wa LUKU, angalau kwa maneneo maalum kama kariakoo, Masaki, mikocheni, mbezi, baadae usambae kwa wengine in phases.
Pia utafiti ufanyike ili mfanyabiashara alazimike kuwa na LIPA NAMBA, ambayo asilimia fulani ya mauzo yake atumie mfumo huo.
Kwa udhibiti wa biashara kariakoo, uimarishwe, pale bado mapato yanavuja.