William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Wana makosa gani wanaosema mkapa ni mwadilifu!!!!!! in this regard hawana. Mzee wa watu kafannya alichoweza kufanya na amemaliza mihula yake miwili, aachwe apumzike!?
Mwakyembe amefanya anyoweza na amemaliza kazi, anayetaka kufanya zaidi kwani kuna tatizo gani kuanza kuandika ripoti yako?
Tumesema sana kuwa viongozi wadilifu hawatachafuliwa hapa hata siku moja, halafu tukanyamaza.
uadilifu wake umepungua pale aliposema kuna mengine kayamezea. Kwa nini kayamezea, mwadilifu na shujaa wa wananchi hawezi kuficha siri ya adui wa wananchi (mafisadi serikalini). Kwa hili uadilifu wake utakuwa kwenye alama ya kuuliza hadi pale atakapoyasema hayo ambayo hajayasema.
Mkuu lakini kumbuka huyu jamaa hata maisha yake yalikuwa HATARINI!
MMESAHAU ALILAZWA MAJUZI?
Mwakyembe amesema kuwa kwa heshima ya serikali, sasa kwako wewe huenda serikali ni mafisadi, lakini sio kwetu wananchi wote tunaoi ona serikali kuwa ni mafisadi, kuna tunaomaini kuwa kuna viongozi wachache serikalini ndio mafisadi, lakini sio serikali yote na ndio maana tunakubaliana na Mwakyembe kuwa ilikuwa ni sawa kutosema yote yanayoihusu serikali kwa sababu mbali mbali moja wapo ikiwemo ya kficha majina ya maofisa wa usalama wa taifa waliohusika, ambao bado wako active na kazi zao za kutulinda na kulilinda taifa letu,
Mwakyembe aliyoyafanya yametosha, kwa sababu yeye kama mwanasheria anazo akili za kutosha kujua mstari ulipochorwa, na sio yeye tu hata sisi wananchi pia tunajua hilo tena kwa mapana sana na marefu, kwa sababu tunajua vizuri yaliyompata Baharia Memba, kwa kusikiliza maneno kama yenu.
Kwa kifupi ni kwamba kuna watu wetu wa uwt waliohusika na hii ishu kwa nia njema na mbaya, lakini bado huwezi kuziweka habari hizo zote hadharani kwa sababu wengine wahusika bado ni active wa uwt, sasa hizi ndio tunaita siasa za kiutu-uzima,
Mbunge na Shujaaa Mwakyembe, amefanya the best he could kulingana na mazingara ya kiserikali na kisiasa tuliyonayo Tanzania, kumbukeni wakuu kuwa siasa za bongo sio za huko majuu, naona mara nyingi tunachanganya sana hili,
Mwakyembe bado ni shujaa wangu na wa taifa langu, asiyekubali uwanja uko wazi na wewe ni kuingia tuone vitu vyako, nafikri Mwakyembe anayo haki ya kuwauliza wabongo kama muanzisha topic kuwa je toka atoe hii ripoti iliyowapeleeka mwaziri wawili na waziri mkuu kujiuzulu, wewe kama mwananchi umefanya nini hasa kama nyongeza ya pale alipoishia?
Mkuu ni haki yako kuuliza, kama ilivyo haki yetu not only kukuuliza ila ni pamoja kukuelimisha zaidi, kwani sio siri kuwa uwezo wako wa kufikiri na kuelewa unapoishia ni level ndogo sana kwa hii JF.
Ahsante Mkuu!
Mkuu heshima yako, hakuna anayetaka kumchafua Mwakyembe hapa, bali tunachosema alichokifanya siyo sawa sawa. Kama alipewa mipaka ya nini cha kuandika katika ripoti hiyo basi Watanzania tuna kila haki ya kufahamishwa hilo na ni nani aliyemwekea mipaka hiyo.
Hebu fikiria wale Ernst & Young waliopewa kazi ya kuchunguza ufisadi mkubwa uliofanywa pale BoT kama wangeamua kutoandika baadhi ya mambo waliyoyaona katika ukaguzi wao ili 'kulinda heshima' heshima ya serikali. haya yote kuhusiana na wizi wa shilingi bilioni 133 tusingeyajua maana yote yanahusiana kwa namna moja au nyingine na serikali. Hivyo na wao wangeweza kutoa ripoti kama waliyoitoa PCCB kuhusiana na ripoti kwamba tuhuma zilizotolewa ni za uwongo.
Hakuna yeyote aliyempa Mwakyembe na kamati yake authority ya kipi cha kuandika na kipi hakistahili kuandikwa, hivyo yeye kujipa authority hiyo ni makosa. Pamoja na kuwa tunaheshimu kazi waliyoifanya lakini sasa kuna utata, Watanzania tutajuliza je, yaliyoachwa kuandikwa ndani ya ripoti ile ni mazito zaidi kuliko yaliyoandikwa? Na ndivyo inavyoelekea kama yaliyoandikwa yalisababisha kuanguka kwa Waziri Mkuu basi yaliyoachwa labda yangesababisha kuanguka kwa serikali nzima pamoja na Rais.
Hivi kweli mtu mzima na akili timamua na Mtanzania, unaweza kumlinganisha Mkapa na Mwakyembe?
Mwakyembe amewaondoa Mawaziri wawili na waziri mkuu kwa kusema wazi jinsi walivyokula rushwa , Mkapa alimuondoa kiongozi gani kwa rushwa?
Mama,
Mimi sifahamu kwa undani kanuni za Bunge la Tanzania, lakini nafahamu kwamba waheshimiwa wabunge wanafuata kanuni katika kuwasilisha hoja au zile reports ambazo huzisoma baada ya kufanya uchunguzi wa jambo fulani.
Kwa mantiki hio nafikiri kwamba hata mheshimiwa Zitto (kijana mwenzetu mwingine) alipata adhabu kwa kukiuka kanuni za Bunge na akafungiwa.
Sasa cha msingi ni kurudi katika report ile na kuisoma kwa uzuri ili tuelewe na tulinganishe na kauli ya Mheshimiwa Mwakyembe, halfu ndio (kama wananchi) tupime kati ya anaezuia "report" kusomwa yote na ana nguvu gani au mbunge ambae anabanwa na ama kanuni za Bunge au mamlaka ya juu ya Bunge hilohilo.
Mkuu heshima yako, hakuna anayetaka kumchafua Mwakyembe hapa, bali tunachosema alichokifanya siyo sawa sawa. Kama alipewa mipaka ya nini cha kuandika katika ripoti hiyo basi Watanzania tuna kila haki ya kufahamishwa hilo na ni nani aliyemwekea mipaka hiyo.
Shida, tuliyonayo sasa ktk vita dhidi ya ufisadi, ni kutofautisha kati ya fisadi na mzalendo!!!!
Sina shaka, Rostam, Lowassa, Karamagi, Bangushiro na wenzao wanachekelea makombora anayopigwa mwakyembe humu!!!! Kwao wao Kuhani na wenzake ni mashujaaa!!!
Teh teh teh!!
hivi mtu mzima na akili zake tena Mtanzania anaweza kusema Mwakyembe asichafuliwe eti kwa mtu kuquestion credibility yake kwa vile kaficha siri za ufisadi
Shida, tuliyonayo sasa ktk vita dhidi ya ufisadi, ni kutofautisha kati ya fisadi na mzalendo!!!!
Sina shaka, Rostam, Lowassa, Karamagi, Bangushiro na wenzao wanachekelea makombora anayopigwa mwakyembe humu!!!! Kwao wao Kuhani na wenzake ni mashujaaa!!!
Teh teh teh!!
hivi mtu mzima na akili zake tena Mtanzania anaweza kusema Mwakyembe asichafuliwe eti kwa mtu kuquestion credibility yake kwa vile kaficha siri za ufisadi
Nani kasema hajafanya kazi nzuri?
Kwa nini haingii akilini kwa wengi kusema shujaa kakosea?
Kwani ye Nyerere mpaka asikosee?
Hata Mimi Sikubali Kabisa Mwakyembe Kuchafuliwa!
Mkuu tumekuambia mara nyingi sana hapa kuwa hata kuisoma ile ripoti yote pale bungeni yalikuwa ni makosa kisheria za bunge, hakutakiwa kufanya vile ila kuna viongozi wenye uchungu na taifa ndio waliomruhsu kwa kupindisha hseria kwa makusudi, na besides umeambiwa sana kwenye kile kikako cha bunge kwua kama unataka ile ripoti nenda bunge ukaombe hansard ya ile siku, ambayo ina ripoti yote na sehemu nyingi ambazo Mwakyembe hakuzipitia kabisa kutokana na muda kuwa mchache,
Nyinyi msitudanganye hapa, riopit hata ya USA inayohusu kuvamiwa kwao iel siku September 11, ina sehemu nyingi sana ambazo zimezibwa, wale wananchi waliotaka kum-sue Bin Laden wakashindwa kabisa kuendelea na kesi, sasa itakuwa sisi bongo?