Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

... And no.. Yesu hakumuambia kuwa "nguvu zote za kunitesa tumekupa sisi"... check your Bible again.

Twende kule kwenye forum ya Dini nikakupe somo alikuwa ana maana gani aliposema nguvu na mamlaka ya huo Upilato umepewa na Baba yangu, na alikuwa na maana gani alipo mstopisha mfuasi wake aliyetaka kuanzisha fujo baada ya Yesu kuchapwa kibao, akamtumliza akamwambia hawa nguvu ya kutuchapa sio tatizo, naweza kuamuru majeshi ya Mungu yakaibuka hapa sasa hivi. Mimi sina haya ya ku refer neno kwa neno, najaribu kuelewa the whole concept. Hicho kitu hukuambiwa na Padre Mwanakijiji.
 
labda angesema yote, hakuna ambaye angeadhibiwa au kuwajibika! na kusingekuwa na uchaguzi wala nini. Unafikiri nani angekuwa tayari kumfunga paka kengele kama watu wenyewe ni design ya kina Chitalilo. I'm glad he said what he said and we got what we got! Kufikiri kwamba angesema yote basi tungepata zaidi ya tulichopata ni kutokupima siasa. Kama daktari, manesi, na raia wote wagonjwa, nani atampeleka nani hospitali!? mnabakia kuuguzana tu.

Je ni halali kumkosoa Mwakyembe kwa kutokusema yote? Je ni halali kusema ana dalili ya dishonesty kwa kutokusema mabaya yote analiyoyajua? Kama ambayo hajayasema ni makubwa na mabaya zaidi ya aliyoyasema, angeyasema tungemwita shujaa squared?
 
Kama kuna vitu ambavyo hukuviweka hadharani kwa sababu za "kulinda heshima ya serikali" "usalama wa taifa" na maanjumati mengine kama hayo, basi hata kusema "kuna vitu sikuviweka hadharani" kunakuwa na effect ile ile ya ku undermine heshima ya serikali na usalama wa taifa. kwa mfano sasa hivi watu wanajadili hatua ya Mkwakyembe kuficha vitu hivi in the same breath with wizi wa hela za serikali BOT ulivyofanyika "kwa usalama wa taifa".Tunaona kuna pattern ya kutumia vitu kama usalama wa taifa na heshima ya serikali kutetea ufisadi, kwa nini tukupe free pass Mwakyembe?

Kama kuna vitu hujaviweka hadharani usiviongelee kabisa, ama sivyo utafungua the proverbial can of worms na watu wakifanya kichuguu kuwa mlima Kilimanjaro huwezi kuwalaumu.

Ni sawa sawa na kumwambia mtu "najua siri yako lakini sikwambii kwa kulinda heshima" automatically human nature itamfanya mtu afikirie unajua the worst about him, au hata kuinvent vitu ambavyo havipo.

That whole statement was unfortunately distracting and should not have been made.

Kwamba Dr. Harrison Mwakyembe ameonyesha ushujaa wa hali ya juu - hili halina ubishi hata kidogo. Lakini nikikumbuka usemi wa "we will leave no stone unturned in our efforts to get to the truth", nabaki nikijiuliza hivi kwa nini kamati ya bunge iliundwa. Nini mantiki ya bunge kuunda kamati ifanye uchunguzi kwa jambo lenye maslahi mazito kwa taifa halafu hiyo hiyo kamati itoe taarifa nusu nusu kwa hilo hilo bunge.

Kawaida ya wacheza kamari ni kuwa kama unayo "trump card", unaisitiri kwa siri ya ajabu mpaka wakati muafaka. Ninajua Dr. alikuwa provoked lakini siri ya mpiganaji shupavu ni kutoonesha hofu mbele ya adui na kuanza kurusha mabomu bila mpangilio.

Tofauti na mtoa mada, mimi simhukumu Dr, ila nakuta niko njia panda na hiyo statement yake. Je nikianza kuamini kuwa kamati zote zinazoundwa zinafanya kazi zake kwa mtindo huu, nitakuwa nimekosea. Kwa kweli hapa kuna maswali kuliko majibu. Je tuunde kamati ichunguze kwa nini some info was withheld na ni kwa misingi gani hasa.
 
Ingawa hapa sio mahali pa Dini, lakini ni lazima tuelimishane pia:-

Ni kama Yesu vile, huwezi kumkosoa kama umekulia kanisani.

Mkuu kwa sisi wa-Kristo kumkosoa Yesu ni kumkosoa Mungu, ni absolutely NO kwetu!

Lakini ambacho hatuambiwi, ni kwamba hata Yesu nae kuna siku aliharibu

Yesu hakuwahi kuharibu hata siku moja, aliyeharibu ni Moses, pale aliamuru kwa hasira maji yapatikane na ndicho kilichompelekea kwenye kutangulia kwenye haki baada tu ya maji kupatikana, lakini Yesu hakuwahi kuharibu kwa sababu utabiri wa manabii uko clear kuwa hakuletwa dunaini kuharibu hata mara moja, Mungu ana sheria moja isiyopingika wala kuekebishika, ukiharibu ni lazima kuwe na malipo, nayo ni kifo, kifo cha Yesu hakikutokana na kuharibu kwake kama unavyodai, ila ilikuwa imeandikwa kuwa atakufa na kufufuka siku ya tatu na ndicho kilichotokea na baadaye atarudi mbinguni, bin-adam wanaoharibu huwa wakifa hawafufuki kama Moses bin-adam aliyeharibu.

alipomwambia Mungu, Mungu niepushe na kikombe hiki, siku ile walipokuwa wanaelekea Calvary kumfanyia. Yesu hapo hapo akajishtukia kakurupuka, akarekebisha, "ikiwa ni mapenzi yako."

Yesu alisema kuwa kama inawezekana Mungu naomba kiepushe kikombe hiki, lakini hakusema niepuishe na kikombe hiki, mkuu kwenye dini yetu tunafundishwa kila siku kuwa shetani ni mjanja sana kwa kugeuza maneno, ndivyo alivyoweza kumdanganya Hawa, Mungu alisema mkila matunda kwa hakika mtakufa, yeye akamwambia Hawa kuwa Mungu alisema tu kuwa mtakufa na kuliahca neno la kwa hakika, here you are na yale yale ya ujanja wa shetani kujaribu kubadili maneno ili utimize dhambi yako, no mkuu we know better!

That same morning, Yesu alikuwa ametoka kumwambia Pilato kwamba nguvu zote za kunitesa tumekupa sisi, yani yeye Yesu na Mungu.

Pilato alimuambia Yesu kuwa nina nguvu za kuweza kukuokoa na kukuua, Yesu alimuambia kuwa umepewa na Baba yangu, hakusema tumekupa sisi huu ni uongo wa mchana mkuu acha hizi za dini isiyokuwa yako maana ni aibu tupu!

Lakini wakati anaenda kugongelewa misumari, Yesu mwenyewe akataka kuchomoa. Aliogopa. Alichemka. Akarekebisha.

Mwanafunzi wa Yesu, Petro alimkata askari mmoja sikio alipokuja kumkamata Yesu, lakini ni Yesu ndiye aliyemrudishia sikio yule askari na kumpa mikono yake baadaye ili amshike na kumchukua kama neno la Mungu lilivyoandika na kutabiri mapema sana hata kabla Yesu hajazaliwa, sasa kwa nini asikimbie pale alipoona askari anayetaka kumshika amekatwa sikio?

Ni wapi hapo panaposema kuwa Yesu alitaka kuchomoa? Halafu Yesu unamuingizaje kwenye mijadala ya siasa za Mwakyembe na mafisadi, mbona huna heshima kwa dini za wengine mkuu? Hivi kweli unataka tukuwekee hapoa jinsi Mtume Mohamed alivyokuwa akila Nguruwe na kuwakataza waumini wake wasile nyama hiyo tamu ambayo yeye alikuwa akiila kwa siri?

Sasa huyu utamlinganishaje na Mwakyembe, maana wewe ndiye bingwa wa kuchanganya dini na siasa, tuwekee hapa tumkome nyani? Wewe kijana usicheze na dini za watu umeshaonywa sana mambo ya kuleta dini hapa lakini husikii, acha ujinga!
 
Kwa maoni yangu, Mwakyembe alipopewa kazi ya kuchunguza mkataba wa Richmond hakupewa mipaka yoyote, kwamba kama angeona chochote katika uchunguzi wako/wenu ambacho kinaidhalilisha serikali kwa namna moja au nyingine basi usikiweke/msikiweke kwenye final ripoti yenu. Kama alipewa mipaka ya uchunguzi huo, basi Watanzania tufahamishwe, vinginevyo amefanya makosa makubwa. Tunajuaje kama hayo ambayo hawakuyaandika kwenye hiyo ripoti ni mazito zaidi kuliko yale yaliyoandikwa?

Kamati ilipopewa kazi ya kufanya uchunguzi huo ilikuwa ni kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania na siyo kwa maslahi ya serikali iliyopo madarakani. Watanzania tuna haki ya kuyajua yote yaliyojiri katika mkataba huo, hivyo pamoja na kumpongeza Mwakyembe na kamati yake kwa ripoti waliyoiandika na hatimaye kusababisha kujiuzulu kwa Lowassa, Msabaha na Karamagi kuna haja ya kuwashinikiza ili watupe ripoti yote bila kubakisha chochote.

Wenye nchi ni sisi Watanzania na siyo serikali iliyopo madarakani na pesa zinazolipwa/zilizolipwa kwa Richmond/Dowans si za serikali iliyopo madarakani bali ni za Watanzania. Mwakyembe kwa heshima na taadhima tunakuomba utupatie ripoti kamili na siyo nusu nusu kwa sababu kamati yako imetumia millions kama siyo mabilioni katika uchunguzi wenu hivyo tunastahili kupata ripoti kamili zinazoendana na gharama mlizotumia kufanya uchunguzi wenu.
 
"We Chiligati nini?"

Hivyo vitu viwili ulivyovisema hapo, kwa washabiki wengi wa maendeleo na wapinga ufisadi, haviingii akilini kuvisema pamoja. Utaambiwa wewe Makamba unatumia user name ya Bokassa.

Haingii akilini kabisa kwa wengi kusema shujaa kakosea.

Ni kama Yesu vile, huwezi kumkosoa kama umekulia kanisani. Lakini ambacho hatuambiwi, ni kwamba hata Yesu nae kuna siku aliharibu alipomwambia Mungu, Mungu niepushe na kikombe hiki, siku ile walipokuwa wanaelekea Calvary kumfanyia. Yesu hapo hapo akajishtukia kakurupuka, akarekebisha, "ikiwa ni mapenzi yako." That same morning, Yesu alikuwa ametoka kumwambia Pilato kwamba nguvu zote za kunitesa tumekupa sisi, yani yeye Yesu na Mungu. Lakini wakati anaenda kugongelewa misumari, Yesu mwenyewe akataka kuchomoa. Aliogopa. Alichemka. Akarekebisha.

Sembuse Mwakyembe?

Ba Nkwe nawe mpinga mafisadi!!!!?????

Too Confusing!!!!
 
Twende kule kwenye forum ya Dini nikakupe somo alikuwa ana maana gani aliposema nguvu na mamlaka ya huo Upilato umepewa na Baba yangu, na alikuwa na maana gani alipo mstopisha mfuasi wake aliyetaka kuanzisha fujo baada ya Yesu kuchapwa kibao, akamtumliza akamwambia hawa nguvu ya kutuchapa sio tatizo, naweza kuamuru majeshi ya Mungu yakaibuka hapa sasa hivi.

Wewe kijana haya mambo ya dini ya Kikristo huyajui kabisa ni bora uongee siasa, maana ni haki ya kila mwananchi hata asiyejua kusema sema,

1. Askari aliyekuja kumkamata Yesu, alikatwa sikio na Petro, Yesu akamkataza kabisa Petro na kumponya mara moja yule askari kwa kumrudishia sikio lake na kukubali kuchukuliwa na yule askari, that was the ishu haikuwa na uhusiano wowote wa Yesu kupigwa kibao.

2. Aliyesema kuwa ninajua kuwa unaweza kumauru majeshi yako ya malaika yaje hapa na kukusaidia, alikuwa ni shetani alipokuwa akimjaribu Yesu kule milimani, sio Yesu aliyesema kama unavyojikanyaga hapo juu, mkuu acha hizi dini maana you hyave no clue kabisaa na unachosema na it has nothing to do na ripoti ya Mwakyembe.
 
Wakuu hii si ingepelekwa uwanja wa dini?
ama macho yangu?
 
Niambie nini kibaya cha "Siasa za huko Majuu" halafu siku nyingine kabla sijajadili kitu nitaangalia kama kina fanana fanana na "Siasa za huko Majuu" kabla sijakisema au kukipendekeza.

Kwa sababu huko majuu hakuna siasa kama za Mugabe, ambazo ndio hizo hizo za kwetu bongo, lakini haibadili ukweli kuwa Mugabe ni rais,

standard zetu bongo na demokrasia bado ni almost zero hizi kweli ninahitaji kukufundisha hili? Lowassaa angekuwa majuu angekuwa wapi sasa hivi? Mbona unauliza majibu bro?
 
Wakuu,

Mwakyembe alitumwa kazi na aliifanya kazi yake kwa uadilifu wote na akakabidhi riport ile kwa rais na hatimae Bunge.

Sasa wenye jukumu la kumalizia ni sisi wananchi. Mheshimiwa Mwakyembe amefanya kazi ambayo alijua ni nzito sana na kwa ujasiri ameifanya.

Tumwache kijana mwenzetu apumue.
 
Some spades are big spoons; however sometimes dont dare to talk openly.

Thanks a lot Mama. Mwakyembe had no authority to hide anything from that report. We need full repost asap.
 
Twende kule kwenye forum ya Dini nikakupe somo alikuwa ana maana gani aliposema nguvu na mamlaka ya huo Upilato umepewa na Baba yangu, na alikuwa na maana gani alipo mstopisha mfuasi wake aliyetaka kuanzisha fujo baada ya Yesu kuchapwa kibao, akamtumliza akamwambia hawa nguvu ya kutuchapa sio tatizo, naweza kuamuru majeshi ya Mungu yakaibuka hapa sasa hivi. Mimi sina haya ya ku refer neno kwa neno, najaribu kuelewa the whole concept. Hicho kitu hukuambiwa na Padre Mwanakijiji.

Hii issue ya YESU KUPIGWA KIBAO labda inaweza kuwa tofauti na hiyo ya kukatwa sikio la ASKARI POLISI kulikofanywa na PETRO?
 
Mwakyembe amefanya anyoweza na amemaliza kazi, anayetaka kufanya zaidi kwani kuna tatizo gani kuanza kuandika ripoti yako?

Tumesema sana kuwa viongozi wadilifu hawatachafuliwa hapa hata siku moja, halafu tukanyamaza.
 
Wakuu,

Mwakyembe alitumwa kazi na aliifanya kazi yake kwa uadilifu wote na akakabidhi riport ile kwa rais na hatimae Bunge.

Sasa wenye jukumu la kumalizia ni sisi wananchi. Mheshimiwa Mwakyembe amefanya kazi ambayo alijua ni nzito sana na kwa ujasiri ameifanya.


Tumwache kijana mwenzetu apumue.

uadilifu wake umepungua pale aliposema kuna mengine kayamezea. Kwa nini kayamezea, mwadilifu na shujaa wa wananchi hawezi kuficha siri ya adui wa wananchi (mafisadi serikalini). Kwa hili uadilifu wake utakuwa kwenye alama ya kuuliza hadi pale atakapoyasema hayo ambayo hajayasema.
 
Wakuu hii si ingepelekwa uwanja wa dini?
ama macho yangu?

Mushi samahani.

Nilitoa mfano mmoja tu kama fundisho tunaloweza kupata kutoka vitabu vitakatifu. Mwanakijiji akanijibu kistaarabu, na mimi nikamwomba tukoke pempeni tukaelimishane kuhusu hili swala. Ghafla ikatokea kelele na ghasia na watu wakaleta personal issues, sijui Mkuu ana issue gani sijui. Duuh, samahani Mushi.
 
Mwakyembe amefanya anyoweza na amemaliza kazi, anayetaka kufanya zaidi kwani kuna tatizo gani kuanza kuandika ripoti yako?

Tumesema sana kuwa viongozi wadilifu hawatachafuliwa hapa hata siku moja, halafu tukanyamaza.

Wana makosa gani wanaosema mkapa ni mwadilifu!!!!!! in this regard hawana kosa. Mzee wa watu kafannya alichoweza kufanya na amemaliza mihula yake miwili, aachwe apumzike!?
 
Mushi samahani.

Nilitoa mfano mmoja tu kutoka kama fundisho tunaloweza kupata kutoka vitabu vya vitakatifu. Mwanakijiji akanijibu kistaarabu, na mimi nikamwomba tukoke pempeni tukaelimishane kuhusu hili swala. Ghafla ikatokea kelele na ghasia na watu wakaleta personal issues, sijui Mkuu ana issue gani sijui. Duuh, samahani Mushi.

Mkuu lakini kumbuka huyu jamaa hata maisha yake yalikuwa HATARINI!
MMESAHAU ALILAZWA MAJUZI?
MMESHASAHAHU BALLALI?
Hivyo basi...Nakubaliana na FMES kuwa jamaa alifanya kazi nzuri tegemeana na mazingira yaliyowaondoa kina SOKOINE,KOLIMBA NA WENGINEO.
 
Mwakyembe amesema kuwa kwa heshima ya serikali, sasa kwako wewe huenda serikali ni mafisadi, lakini sio kwetu wananchi wote tunaoi ona serikali kuwa ni mafisadi, kuna tunaomaini kuwa kuna viongozi wachache serikalini ndio mafisadi, lakini sio serikali yote na ndio maana tunakubaliana na Mwakyembe kuwa ilikuwa ni sawa kutosema yote yanayoihusu serikali kwa sababu mbali mbali moja wapo ikiwemo ya kficha majina ya maofisa wa usalama wa taifa waliohusika, ambao bado wako active na kazi zao za kutulinda na kulilinda taifa letu,

Mwakyembe aliyoyafanya yametosha, kwa sababu yeye kama mwanasheria anazo akili za kutosha kujua mstari ulipochorwa, na sio yeye tu hata sisi wananchi pia tunajua hilo tena kwa mapana sana na marefu, kwa sababu tunajua vizuri yaliyompata Baharia Memba, kwa kusikiliza maneno kama yenu.
 
Hata Mimi Sikubali Kabisa Mwakyembe Kuchafuliwa!
 
Back
Top Bottom