Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Any attempt ya kuiweka uchi serikali ingeresult into political instability. unaweza ukapapambana na watu but not the system. Mheshimiwa alijaribu kuilinda system. Amejitahidi jamani.

kailinda system na katusaliti wananchi. Kwa mantiki hiyo huyo ni shujaa wa system na sio shujaa wa wananchi.
 
Wakati ripoti zote zimeshatoka na hivyo kutufanya kujuwa NANI NI FISADI...BADO MAMLUKI WA MAFISADI WANAPITA PITA HUKU NA HUKO KUENEZA CHUKI ZA KIDINI NA KIKABILA!
Kabla hamjamyooshea kidole mtoa ripoti...TUNATAKA TUANZIE NA HAO MAFISADI WA EPA WALIOPIKA HIZI PROPAGANDA...MWEMA...KAMATA IDDI SIMBA,LUKAZA NA MALEGESI...HAO NDIO WALIOSUKA DILI LOTE!
 
Any attempt ya kuiweka uchi serikali ingeresult into political instability. unaweza ukapapambana na watu but not the system. Mheshimiwa alijaribu kuilinda system. Amejitahidi jamani.

...kwa hiyo alikuwa anaichunguza systema ili aone namna ya kuilinda au?!
 
kuna tatizo hapa kwa baadhi yetu kutotaka kuelewa au kwa makusudi au kikomo cha kuelewa, turejee katika kauli ya Dk Mwakey, alisema ataongezea yaliyomo kwa maandishi au alisema atasema yale yaliyomo ambayo hayakusemwa?
 


Brother, I am definitely running out of FIVES, But take another ONE just the same !!🙂
 
Bubu message sent, tuseme wabunge hawakugaiwa ful-report, walisomewa ile summary basi wakatosheka!!?? Ukweli haufichiki na utaendelea kusimama daima dumu hata ukitwistiwa kwa maneno mengi kiasi gani.



I definitely love the new word...ukitwistiwa...teh teh teh!!
 
Kwani kwenye ripoti ya Mwakyembe mnataka kusema walioitwa mafisadi si mafisadi? Nani kasema MWAKYEMBE NDIYE JAJI? HAO HAO WALIOTAJWA WATATAJANA WAKISHAJUWA SHIDA YA ROKAPU! LOWASSA KAMA HATA KI KUMTAJA KIKWETE NA BADALA YAKE ANAWATUMA WAPAMBE KULIA NA MWAKYEMBE...THEN AKAMATWE KWANI AKIWEKWA NDANI ATAUSEMA UKWELI! HAWA NI WATUHUMIWA NA HATUTAKI SIASA!
 

Mkuu hili sio kosa la Mwakyembe ni kosa letu wananchi na wabunge wetu walionyamaza kimyaa badala ya kudai isomwe ripoti yote.

Aliye-form kamati ni bunge, yaani wawakilishi wetu sisi wananchi, sio Mwakyembe aliyei-form ile kamati.
 
Bubu message sent, tuseme wabunge hawakugaiwa ful-report, walisomewa ile summary basi wakatosheka!!?? Ukweli haufichiki na utaendelea kusimama daima dumu hata ukitwistiwa kwa maneno mengi kiasi gani.

Huuu ndio ukweli hasa wa hiii ishu, meaning kwamba tatizo sio Mwakyembe, tatizo ni wabunge wetu waliokaa kimyaaaa wakati hii ripoti ikijadiliwa mpaka kumalizika,

Mwakyembe has nothing to do na ripoti kutosomwa yote.
 
Mkuu hili sio kosa la Mwakyembe ni kosa letu wananchi na wabunge wetu walionyamaza kimyaa badala ya kudai isomwe ripoti yote.

Aliye-form kamati ni bunge, yaani wawakilishi wetu sisi wananchi, sio Mwakyembe aliyei-form ile kamati.

Ndiyo maana baadhi ya Wananchi tunalihoji maana kama ni makosa basi yanaweza kurekebishwa maana uchunguzi ule ulifanywa kwa manufaa ya Watanzania na siyo kwa manufaa ya Bunge au CCM. Kwa sababu bunge hili uchwara lipo pale kwa sababu ya maslahi ya chama cha mafisadi matokeo yake ni ufisadi kuzidi kushamiri kila kukicha na idadi ya mafisadi kuongezeka.

Tunachokiona ni mafisadi kuwa matajiri wa kupindukia wakati Watanzania wengi wanaendelea kuishi maisha ya dhiki. Kuna kasoro, tena kubwa sana ni lazima tuiseme. Na hili linasababishwa na haya mambo ya 'kulindana na kulinda heshima ya serikali'

Mkapa katuibia Watanzania Kiwira Coal Mining lakini mpaka hii leo wanaogopa hata kumhoji ili 'kulinda heshima' yake. Tangu lini mwizi akastahili kulindiwa heshima yake? Wadanganyika baadhi yetu ndivyo tulivyo hatuhoji mambo kwa mapana na marefu ili kujua undani wake na sasa yanaigharimu nchi kwa kiasi kikubwa. Mikataba mibovu ya madini, hakuna aliye tayari kuiangalia upya ili iwe na maslahi kwa Watanzania. Mafisadi wamechota mabilioni ya shilingi na wote bado wako nje wanakula kuku kwa mrija ili 'kulindiwa heshima zao' Wanajua hawa ni wadanganyika tu hawatafanya lolote.
 
Huuu ndio ukweli hasa wa hiii ishu, meaning kwamba tatizo sio Mwakyembe, tatizo ni wabunge wetu waliokaa kimyaaaa wakati hii ripoti ikijadiliwa mpaka kumalizika,

Mwakyembe has nothing to do na ripoti kutosomwa yote.

Kama hili la kwamba wabunge hawakugaiwa report ni kweli na wakakubali hivyohivyo, basi tuna shida kubwa kuliko ninavyodhani! Hebu nielimisheni maana mwenzenu naweza nikawa nipo dunia ingine kabisa, ina maana ni kawaida hii kwamba wabunge huwa wanapewa summary tu za report lakini hawapati report nzima, could this truly be true wajemeni?
 
ripoti kamili ilitolewa. Tatizo waliisoma? Siku wanazungumza na Waziri Mkuu kujiuzulu wengi walikuwa wamesoma ile summary (iliyosomwa Bungeni) lakini hawakuwa wamepepitia ripoti nzima na vielelezo. Ukienda kwenye KLH News utaona ripoti zote mbili (ya summary na full). Mimi nadhani kitu ambacho kinatakiwa kuwekwa hadharani ni vile vile vielelezo. Na hicho ndicho hakikusemwa Bungeni.
 
1. Nijuavyo mimi ni kwamba ripoti haikusomwa in full kwa sababu ilikuwa ni ndefu mno na kanuni za bunge haziruhusu Mwakyembe kupewa masaa mawili aliyopewa kuisoma ile ripoti, ingawa alifanya hivyo lakini kilikuwa ni kinyume na kanuni za bunge, kama walivyoniambia wabunge wengi walioshirki ile siku.

2. Lowassa na wenzake walijaribu mbinu nyingi sana za kutaka kuizima ile ripoti isisomwe, ikiwa ni pamoja na mkutano wa usiku wa wabunge wa CCM, ambako Makamba alijaribu kuwatisha sana wabunge kuwa wawe kimya kesho yake, lakini akagonga mwamba, wabunge walimfahamisha rais ambaye alikuwa Chamwino, alitoa amri kwa makamba na wenziwe wasiwatishe wabunge tena.

3. The next thing mafisadi wakaamua kuleta ripoti yao, kitu ambacho the dataz ni kwamba ndivyo walivyofanya kwa Hosea, walimpa ripoti ya kusoma kwa taifa waliyoiandika wao, ile ya Hosea ikafichwa, walipojaribu hili wakashindwa kwa sababu Spika hauwa nao, juhudi zote hizi ziliposhindikana kesho yake asubuhi Lowassa akawa-suprise wabunge kwa kusema anajiuzulu,

ukiangalia kwenye video ya hiyo siku unaona kuwa bunge halikutegemea kuwa haya yatatokea, bunge likawa in confusion kuna mahali Masilingi anawaomba wabunge na Spika kuwa bunge liaairishwe kwa sababu form there on hawajui cha kufanya as far as kanuni za bunge is concerned, kweli bunge likaahirishwa, waliporudi tena kesho yake ikawa majadiliano yasiyokuwa na anything to do na ile ripoti,

Kwa hiyo hapa the ishu tuliyonayo hapa mbele yetu ni kwamba ile ripoti haikusomwa yote, na kwamba wabunge hawakuwa makini kwenye kuisoma kwa sababu wangekuwa wangegundua kuwa kuna sehemu nyingi ambazo zilikuwa zimezibwa kwa ajili ya kulinda siri za serikali, kwa hiyo wangedai kanuni ivunjwe ili isomwe yote, ndio maana ninasema hivi kutokusomwa kwa ripoti nzima bungeni ni kosa la wabunge sio Mwakyembe, na hata sasa hivi wabunge wakidai Spika hatakuwa na njia ila kuvunja kanuni tu ili siwkewe wazi!

Lowassa was smart enough kujua kuwa hawezi kupona na ile ripoti ikisomwa yote kutakuwa na kudaiwa aende jela, akaamua kuleta confusion kwa kujiuzulu ghafla, na ku-create kilio cha kuonewa kuwa hakuitwa kwenye kamati, ile ilikuwa ni janja ya mwizi tena ya dakika za mwisho baada ya juhudi zote kushindwa, sasa ndio tuelewe kuwa kujiuzulu ghafla kwa Lowassa, ilikuwa ni ujanja tu wa kuizima ripoti.
 

Wabunge wamechanganyikiwa kwa sababu walichokwambia kinajipinga.

Tatizo sio ripoti kusomwa au kutokusomwa au muda hautoshi. Ripoti ile kila mtu anaipata, hata mja kama mimi ninayo.

Ishu hapa ni timing and extent of debate.

Mwakyembe anasema mjadala ulisha isha, mbona wanaibuia ishu tena, huku wanatetea tea kina Lowassa?

Tatizo, alipochemka, ni pale alipoanza kusema, eti, ooooh, kama ndio hivyo na mimi niruhusuni niongee tena, nitaanza kujadili vitu ambavyo sikuvisema wakati wa muda niliopewa ili "kutunza heshima ya Serikali."

Mwakyembe ameharibu kwa sababu, kama ni mtu mwenye integrity -na Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi lazima awe na integrity - anatakiwa akisema anatunza heshima ya Serikali basi iwe ni principle ambayo hatishii tishii kuivunja maadui zake wakimsakama.

Na, kama ili kuthibitisha kwamba kina Lowassa waliharibu ilibidi avunje heshima ya Serikali, basi ina maana hakuthibitisha, maana hakuivunja.

Kwa maneno mengine, Mwakyembe alileta vi evidence viko tenuous, halafu vikapeta peta, ishu ikaisha. Sasa watetezi wa Lowassa wameamka usingizini, vidhibiti tenuous vya Mwakyembe vinakuwa unraveled, Mwakeyembe ana panic.

Alichotakiwa kusema Mwakyembe ni hiki: Katikati ya mjadala, Lowassa na wenzake walijiuzulu. Na ndio lilikuwa pendekezo la Tume, kwamba watu wawajibike au wawajibishwe, na kwamba Tume ililiweka swala zima mikononi mwa Lowassa aamue yeye cha kufanya.

Kwa hiyo, baada ya mawaziri watatu kujiuzulu, hakukuwa na haja ya kina Mwakyembe kuendelea kuipigia madebe ishu ya kuwajibika kwa wahusika. Lakini kama wanataka kuibua ishu tena, turuhusuni turudi tena, tujadili vitu ambavyo hatukujadili kwa sababu hakukuwa na huu utetezi mnaokuja nao sasa. Hakukuwa na haja. Utetezi wenu wakati ule ulikuwa ni kwamba tatizo ni Uwaziri Mkuu, na mkaachia ngazi. Kama mmekata rufaa, turudisheni tukamilishe mashitaka.

Ndio hicho Mwakyembe alitakiwa kusema. Na sio ku imply kwamba ni bora kuficha ufisadi kwa ajili ya kutunza heshima ya Serikali.

Alichokisema Mwakyembe ndicho kile kile Pinda alicholiambia Taifa aki cover wizi wa Meremeta.
 
Quote:- Fact

2. However, if some MPs are dissatisfied with any decisions made on this (Richmond saga) issue, we should agree to annul the provisions prohibiting us from deliberating on the matter to allow them to speak their minds.``


Kwakweli ninakuwa guided na huu ukweli hapa juu katika hoja yangu, umesema mengi lakini kwangu it comes down to this, kwamba kuna ambayo hakusema kwa sababu ya kubanwa na sheria za kulinda siri za serikali.

Mengine yote uliyosema ni kweli tupu, lakini integrity ya Mwakyembe abdo iko pale pale kwa sababu ya sheria iliyomzuia asiseme yote, ikivunjwa kama alivyomuomba Spika, na akashindwa basi integrity ya Mwakyembe itakuwa na tatizo, lakini so far bado ni shujaaa wangu na integrity yake iko sawa sana.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amethibitisha kuwa alikikopesha chama chake sh. milioni 500 kwa ajili ya kampeni na pia amekuwa akikikopesha chama hicho mara kwa mara mahitaji yakijitokeza. Huyu ndio Mbowe anayedaiwa na taifa la Tanzania na ameshindwa kulipa deni hilo kwa taifa kwa madai ya kushindwa kufanya hivyo! kwa hili Mbowe amedhihirisha kuwa kwake yeye chama na maslahi yake binafsi ni muhimu kuliko maslahi ya taifa.

Mbowe hafai kuongoza nchi yetu.
 

Na hii inahusianaje na hoja ya Mwakyembe? Au ndiyo yale yale ya ku-flood kila thread na hoja zako za chuki?
 
Nashindwa kuelewa what was so irritating about this thread that someone had the guts to send this message to me.
'kwanza we kijana mtoto wa Arusha mbona una kasi sana? Nna wasiwasi maana unaonesha una sura ya kifisadi. Hata hilo li joka ni ufisadi mtupu. Unatutisha kutaja jina lako!taja basi tuone kama si la kifisadi.Halafu koma kumtaja mwakyembe ovyo.JF si sehemu ya kutapikakila unachohisi. Tupo tulioanzisha. Tunaelewa maana ya jambo forum. Msalimu mkeo
 

Kevo.. naomba utume nakala ya message hiyo na mtumaji kwa "Invisible"... PM hazitumiki kutisha watu au kuharassa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…