...Nijuavyo mimi ni kwamba ripoti haikusomwa in full kwa sababu ilikuwa ni ndefu mno na kanuni za bunge haziruhusu Mwakyembe kupewa masaa mawili aliyopewa kuisoma ile ripoti, ingawa alifanya hivyo lakini kilikuwa ni kinyume na kanuni za bunge, kama walivyoniambia wabunge wengi walioshirki ile siku.
Wabunge wamechanganyikiwa kwa sababu walichokwambia kinajipinga.
Tatizo sio ripoti kusomwa au kutokusomwa au muda hautoshi. Ripoti ile kila mtu anaipata, hata mja kama mimi ninayo.
Ishu hapa ni timing and extent of debate.
Mwakyembe anasema mjadala ulisha isha, mbona wanaibuia ishu tena, huku wanatetea tea kina Lowassa?
Tatizo, alipochemka, ni pale alipoanza kusema, eti, ooooh, kama ndio hivyo na mimi niruhusuni niongee tena, nitaanza kujadili vitu ambavyo sikuvisema wakati wa muda niliopewa ili "kutunza heshima ya Serikali."
Mwakyembe ameharibu kwa sababu, kama ni mtu mwenye integrity -na Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi lazima awe na integrity - anatakiwa akisema anatunza heshima ya Serikali basi iwe ni principle ambayo hatishii tishii kuivunja maadui zake wakimsakama.
Na, kama ili kuthibitisha kwamba kina Lowassa waliharibu ilibidi avunje heshima ya Serikali, basi ina maana hakuthibitisha, maana hakuivunja.
Kwa maneno mengine, Mwakyembe alileta vi evidence viko tenuous, halafu vikapeta peta, ishu ikaisha. Sasa watetezi wa Lowassa wameamka usingizini, vidhibiti tenuous vya Mwakyembe vinakuwa unraveled, Mwakeyembe ana panic.
Alichotakiwa kusema Mwakyembe ni hiki: Katikati ya mjadala, Lowassa na wenzake walijiuzulu. Na ndio lilikuwa pendekezo la Tume, kwamba watu wawajibike au wawajibishwe, na kwamba Tume ililiweka swala zima mikononi mwa Lowassa aamue yeye cha kufanya.
Kwa hiyo, baada ya mawaziri watatu kujiuzulu, hakukuwa na haja ya kina Mwakyembe kuendelea kuipigia madebe ishu ya kuwajibika kwa wahusika. Lakini kama wanataka kuibua ishu tena, turuhusuni turudi tena, tujadili vitu ambavyo hatukujadili kwa sababu hakukuwa na huu utetezi mnaokuja nao sasa. Hakukuwa na haja. Utetezi wenu wakati ule ulikuwa ni kwamba tatizo ni Uwaziri Mkuu, na mkaachia ngazi. Kama mmekata rufaa, turudisheni tukamilishe mashitaka.
Ndio hicho Mwakyembe alitakiwa kusema. Na sio ku imply kwamba ni bora kuficha ufisadi kwa ajili ya kutunza heshima ya Serikali.
Alichokisema Mwakyembe ndicho kile kile Pinda alicholiambia Taifa aki cover wizi wa Meremeta.