Ripoti ya Sky News kuhusu Magufuli na COVID-19

Ripoti ya Sky News kuhusu Magufuli na COVID-19

Hawawezi kurudi tena kuongelea swala hili.

Mabeberu hao hawatutakii mema hata siku moja.

Mshambulizi wetu kaucheza na bao kalifunga.......majirani zetu wamebaki kutafuta mpira na mpaka sasa hawauoni.
mrembo upo ?
 
Serikali ilijitoa, sasa hivi korona ni ishu ya kila familia kujijua kivyakevyake
Hatuna takwimu halisi za kiwango cha korona nchini
Kwenye level ya familia na ukoo wako, kuna wagonjwa wangapi..!? Unakosali/unakoswali je, wapo wangapi!? Majirani zako wapo wangapi walioathirika!? Unakofanya kazi je, kuna wagonjwa!? Etc... KAMA KILA MMOJA WETU MAENEO HAYO HANA MTU ANAYEUMWA, BASI HAIPO..!!
 
Hiki ni kipande cha ripoti ya Sky News, moja ya shirika la habari la binafsi huko Uingereza.

Ni kipande kilichorushwa tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu.

Ni kipande kinachozungumzia jinsi ambavyo Rais Magufuli na serikali yake ilivyoamua kukabiliana na huo ugonjwa wa Coronavirus.

Ni karibu miezi miwili sasa tokea Sky News wairushe hiyo ripoti yao.

Sky News waliirejea hofu ya shirika la afya duniani [WHO] kwamba Tanzania iko juu ya orodha ya nchi ambazo shirika hilo la afya lilikuwa na hofu nazo sana.

Miezi miwili kasoro juma moja, maisha bado yanaendelea tu kama kawaida!

Maiti hazijatapakaa mabarabarani. Hakuna makaburi ya halaiki. Spitali hazijajaa wagonjwa. Nikijizungumzia mimi binafsi, hakuna ndugu, jamaa, jirani, wala rafiki ambaye nimempoteza kutokana na hiyo Corona.

Kwa muktadha wa kinachoendelea sasa hivi baina ya Tanzania na Kenya, nadhani kuna kitu ambacho Wakenya wanaweza kujifunza kutoka Tanzania ya Magufuli.

Wameamua kukata sijui ndege toka Tanzania. Kuna kipindi sijui walifunga mpaka na Tanzania, na mengineyo.

Ninachokiona toka huko Kenya ni [1] uoga wa viongozi wao na [2] ukosefu wa uthabiti katika maamuzi yao.

Ni kama vile Kenya inaiga mataifa ya Ulaya na Marekani, kwa jinsi ilivyoamua kukabiliana na hiyo Coronavirus.

Tokea dunia ikumbwe na hilo janga, ni karibu miezi 6 sasa au hata na zaidi.

Kama yangekuwepo madhara makubwa sana basi yasingeweza kufichika kabisa.

Haiwezekani kuficha vifo na maradhi. Watanzania tulio wengi hatujaathirika na hiyo Corona. Maisha yetu yanaenda kama kawaida.

Hofu ya WHO haijatimizika. Natamani hao Sky News warudi tena Tanzania baada ya miezi miwili tokea warushe hicho kipande cha habari yao. Natamani warudi waje kufanya ‘follow-up’.

Sijui wakirudi watasemaje tu!!?

NB: Baadhi ya tafsiri zao za watu walioongea Kiswahili katika hii video yao Naona ni kama hazipo sahihi.....

Eti wanasema ni nchi ya demokrasia, hawawezi kuficha ungonjwa chini ya kapeti kufanya wananchi wao wasife kimya kimya! Tumbafu zao unaweza ficha kifo kweli? Hill li nchi lishajifia kitambooooo! Sisi tunachapa kazi tu!
 
Baada ya kutafakari kwa muda kuhusu hili swala la corona nionavyo mimi ni kwamba:
1. Corona ina athari kubwa kwa watu ambao kinga zao ziko chini. Wazee sana, watu wenye magonjwa ya kudumu kama kisukari, kansa, pressure etc.
2. Kwa nchi za Ulaya na america kutokana na standard of living na huduma za afya kuwa juu zilikuwa/zina wazee wengi na wagonjwa wengi wa hayo magonjwa niliyoyataja hapi juu.
3. Kwa nchi za Africa kutokana na uduni wa huduma za afya wagonjwa wenye hayo magonjwa wako wachache, maana wengi wanakufa kutokana na ukosefu wa huduma za kuwalinda (care servises). Yaani huku kwetu ukiwa na kisukari, cancer, pressure n.k na kama huna uwezo unakufa mara moja. Hivyo hatuna kundi kubwa la watu wanaoishi na haya magonjwa. Hivyo target ya watu wanaofariki na corona ni ndogo sana.
4. Kenya wameamua kufuata mkumbo bila kuangalia demographic data zao. Wataahiri uchumi wao kwa uzembe wa kufikiri.
5. Kuishi na ku survive Africa lazima afya yako iwe vizuri. So tuna population kubwa ya watu ambao afya zao ziko vizuri kuliko wale amabao afya zao haziko vizuri. So.wachache ambao walikuwa wanaishi na afya mgogoro wameondoka au watandoka. Ila majoritytumepata corona na tume survive
 
Ila sky news wanachekesha kwl maana huyo dkt waliyesema hataki kujulikana yuko ccm na katia nia jimbo la ubunge...waendelee analysis yao
 
afadhali umejizungumzia wewe, ok, sasa wewe mwenyewe uko kwa mabeberu, utapatia wapi ndugu? ndugu zako wanadedi kimya kimya, unadhani wakivuta kuna Wa kunyanyua domo lake kua kavuta na hio kitu? thubutu yake!
ataambiwa au kuandikiwa kua ni kwa changamoto za upumuaji, jifanye unajitangazia hio kitu ndio utawajua hao unaowapamba!
nikwambie tu watu tunaishi kwa kudra za god basi!
Ni kama hujui usemalo!

Yani kwa lugha nyepesi hujielewi
 
Mkuu,hapa unaruka ruka kama maharage ,ulitakiwa utoe jibu la moja Kwa moja, je kuna ndugu ,au jamaa yako yeyote alieathirika Kwa namna yeyote na Corona?

Utajuaje umeathirika au la bila kupima hiyo korona?
Huduma za vipimo kwa nchi nzima ni very little.
 
Baada ya kutafakari kwa muda kuhusu hili swala la corona nionavyo mimi ni kwamba:
1. Corona ina athari kubwa kwa watu ambao kinga zao ziko chini. Wazee sana, watu wenye magonjwa ya kudumu kama kisukari, kansa, pressure etc.
2. Kwa nchi za Ulaya na america kutokana na standard of living na huduma za afya kuwa juu zilikuwa/zina wazee wengi na wagonjwa wengi wa hayo magonjwa niliyoyataja hapi juu.
3. Kwa nchi za Africa kutokana na uduni wa huduma za afya wagonjwa wenye hayo magonjwa wako wachache, maana wengi wanakufa kutokana na ukosefu wa huduma za kuwalinda (care servises). Yaani huku kwetu ukiwa na kisukari, cancer, pressure n.k na kama huna uwezo unakufa mara moja. Hivyo hatuna kundi kubwa la watu wanaoishi na haya magonjwa. Hivyo target ya watu wanaofariki na corona ni ndogo sana.
4. Kenya wameamua kufuata mkumbo bila kuangalia demographic data zao. Wataahiri uchumi wao kwa uzembe wa kufikiri.
5. Kuishi na ku survive Africa lazima afya yako iwe vizuri. So tuna population kubwa ya watu ambao afya zao ziko vizuri kuliko wale amabao afya zao haziko vizuri. So.wachache ambao walikuwa wanaishi na afya mgogoro wameondoka au watandoka. Ila majoritytumepata corona na tume survive
💯%
 
Back
Top Bottom