Ripoti ya Sky News kuhusu Magufuli na COVID-19

Nawaambia watu kila siku, kama Corona kweli ipo na inaua kama wanavotisha watu duniani, basi vifo vingetuumbuwa tu Tanzania.

Tanzania watu siku hizi hawafi?

Umejuaje kati ya hivyo vifo hakuna watu wa korona?

Maana huduma ya vipimo vya korona nchini ni very minimal, na serikali haina interest ya kupima watu enmasse.

Mimi na wewe hatuna rekodi za vifo vya watu kwa sasa ili tuweze kuwa na data za hali halisi ya vifo nchini
 
Mungu hashindwi na chochote. Sisi Kama taifa chini ya uongozi wa Rais Magufuli tuliiweka imani yetu kwa Mungu nae amejibu maombi.

Tuwe makini na maadui wa ndani na nje wanaweza fanya lolote ili kuonesha Rais na Tanzania tulikosea.

Mungu ni mwema sana, tuendelee kumuamini
 
Mungu hashindwi na chochote. Sisi Kama taifa chini ya uongozi wa Rais Magufuli tuliiweka imani yetu kwa Mungu nae amejibu maombi.

Tuwe makini na maadui wa ndani na nje wanaweza fanya lolote ili kuonesha Rais na Tanzania tulikosea.

Mungu ni mwema sana, tuendelee kumuamini
 
Kusoma news kama hizi ni sawa na kuishi nyuma ya wakati... Ujima... Dogo Songa mbele acha kutembea backwards
 
Tokea shule zifunguliwe ingekua hili janga linaua kama utabiri ulivyotolewa na WHO uko sahihi tungeshazifunga tena.

Vifo vya wanafunzi, wanachuo visingeweza kufichika bila kujulikana.

Tunarudi pale pale, kuugua huu ugonjwa wengi umewapata na hapo kuhusu maambukizi wanaweza kuwa sawa ila kwenye madhara ya vifo, hapana. Sio kwa kiasi kilichotarajiwa.

Unatoaje takwimu sahihi wakati haupimi nchi nzima kwa mara moja? Vile vile kuna watu wanamaambukizi na hawaonyeshi dalili, hizo takwimu zitakua sahihi?

Tulishaambiwa tuishi na Corona kama ilivyo Malaria.
 
Wewe hapo ulipo una ngoma?
Kama huna ina maana ngoma haipo?
Sina ndugu aliyewahi kufa kwa Hepatitis B
Haimaanishi kwa mfano kuwa Hepatitis B haipo
Ndiyo maana haujafungiwa ndani (locked down) au kuwekwa kwenye curfew sababu hayo magonjwa kwako siyo kitisho cha kulazimisha ufanyiwe hivyo.
Vivyo hivyo hujatendewa hivyo sababu ya COVID-19 sababu haijawa kitisho sana kwako kama hayo magonjwa uliyosema.

Ni woga tu na biashara za watu wanao tumia huu ugonjwa kama fursa za kiuchumi kwao.
 
Uppo sahihi kabisa mkuu.
Mimi najiuliza tu hivi mtu akipewa hiyo certificate yupo safi hawezi kuambukizwa ugonjwa ndani ya yale masaa ambayo Kenya na zile nchi zingine wanasema wanampokea mtu aliyepima ndani ya huo muda na hatakaa karantini?

Kichekesho sana hizi hatua za kudhibiti huu ugonjwa.
Labda walete chanjo inayofanya kazi wakalazimisha chanjo kama homa ya manjano nitawaelewa.
 
Wewe si upo US?

Wanafahamika kuwa "ni wenye kukaanga mbuyu na kuwaachia we meno watafune."

Waliko wao mabarakoa hadharani si hiari. Kwao maisha ya waliopo 'ikungu lya bashashi' hayana thamani. Ila huko waliko kwenye black lives matter wako mstari wa mbele. Wanataka kuishi.

Hao ndiyo mangedere ngabu, kuona wanaona ya wenzao. Siyo ya kwao.

Jana wilayani Kahama abiria mmoja tokea Dar amefariki njiani jirani na nyumbani kwake. Night kali ya kwenye Saba Saba muda mfupi baada ya kushuka kwenye basi (rip).

Kisa na mkasa? Zile changamoto za zetu.

Kwenye Corona free country, Corona hsipo kabisa. Ila zile changamoto zetu.
 
UKIMWI una miaka zaidi 40 nchini toka ujulikane na Malaki ya watu kote duniani kufariki lakini Tanzania hakuna mtu hata mmoja aliyekufa kwa ugonjwa huo ila kifua kikuu, saratani na magonjwa mengine yaliua watu wengi sana kipindi hicho. Covid-19 kwa muda mfupi imeua malaki ya watu, mamilioni wakiugua kote duniani ikiwa pamoja na nchi zote zinazotuzunguka lakini kwetu ni watu 4 tu walioambukizwa wakifariki kwa magonjwa ya kawaidà kusitukiza ikiwa ni pamoja ugonjwa wa moyo, cancer nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…