Ripoti ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuhusu maboresho ya elimu ya Tanzania

Ripoti ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuhusu maboresho ya elimu ya Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imetoa ripoti baada ya kupokea maoni ya wadau kupitia mikutano mikubwa mitatu iliyofanyika Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.

TET imesema imekusanya maoni kupitia vikao vilivyofanywa na makundi mbalimbali yakiwemo Baraza la Watoto Tanzania, viongozi wa dini, umoja wa wakuu wa shule za Msingi na umoja wa wakuu wa shule za sekondari. Pia, maoni mengine yalipokelewa kwa kutumia namba ya simu, barua pepe, sanduku la barua, kiunganishi kwenye tovuti ya TET, dodoso na hojaji.

Mkurugenzi Mkuu Dkt. Aneth A. Komba amesema Kamati ya Kitaifa ya Mitaala iliyoteuliwa na waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Adolf Mkenda (MB.), inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ya wadau.

“Siku za hivi karibuni tunatarajia kukutana na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kwa kupitia mkutano huu ninawaomba wadau na wananchi kwa ujumla waendelee kutoa maoni yao kupitia barua pepe maoniyawadau@tie.go.tz na namba ya simu 0735 041169,” anasema Dkt. Komba.
 
Elimu ni biashara tutasomaje? Uu...Ah!

D-Knob
 
Back
Top Bottom