Sala na maombi ni muhimu. Hata hivyo, kwa kuwa hatujawahi kusikia wala kuafiki kufanyika kwa sala, dua na maombi yanayoombea wala yanayokusudia kuombea na kukumbatia uzembe; uzembe huu unaothibitika katika taarifa ya media house moja ambapo mwanahanari mmoja anadaiwa kusikika akinukuu; polee,sauti ya mtanzania mwenzetu mmoja akisema bado yupo chini ya kifusi na kuongeza, "mahali hapa nilipo kuna watu 10." Na mara, kwa masikitikiko na simanzi sana tunasikia zinakuja sauti za watu wengi wa jinsi ya kike na kiume kama uthibitisho wa kauli ile ya sauti ya kaka anayeomba msaada kwa ajili na kwa niaba yao wote, ili waweze kuokolewa mapema. Sasa ni mapema gani hii jamani, tukio hili baya la kusikitisha na kububujisha machozi mithili ya bomba la maji, limetokea juzi 15/11/2024 asubuhi. Kwa nini tuendelee kukumbatia uzembe mpaka leo hii Jumapili 17/11/2024? Sauti za wa-Tanzania walipa Kodi wenzetu 10 na pengine zaidi bado zinatoka chini ya kifusiiiii! Wakati Kitengo cha Majanga chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kikijiandaa kwa kuwa ni jambo la dharura, kwa nini Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam isitumie mafungu mengine yaliyopo ya bajeti kuokoa uhai wa ndugu zangu hawa wa-Tanzania wenzetu? Tunaomba sana Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam itupe jibu la swali hili na mengine husika, katika taarifa yake ya baadaye leo, tafadhali.