Ripoti ya uchafuzi mto Mara, ukweli uko wapi?

Ripoti ya uchafuzi mto Mara, ukweli uko wapi?

Taarifa ya uchafuzi wa mto mara na kufa kwa samaki, je taarifa iliyotolewa imejaa siasa au uhalisia?
Au ni mkakati maalum kama tulivyoanza na machinga (wanachafua jiji) tukaja kwa wamasai ngorongoro wamevamia mbuga,
sasa ni zamu ya wanaoishi kandokando ya mito, na pengine hatmaye ni tz nzima, inachafua dunia, tupelekwe sayari nyingine! [emoji119]

Kama kinyesi kimewezekana kuchafua mto, iweje taka za mgodini zishindwe?

View attachment 2156897

View attachment 2156898

View attachment 2156899
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Yaani uamini ripoti ya kijinga namna hiyo??
Angalia ripoti ya ufugaji wa samaki na ng'ombe hapa chini

View attachment 2157203
Nimecheka kwa sauti at Ng'ombe mmoja anatoa kinyesi Cha kilo 25 kwa siku serious?? Pia Ng'ombe Mmoja anakojoa Lita 21 kwa siku yaani ndoo nzima kubwa ya mkono na sehemu.Hata watanzania mmewaona ni wajinga hampaswi kuwadharau kiasi hiki
 
Tunaufuga Samaki tunajua,Kinyesi cha kuku na ng'ombe kinazalisha protein ukubwa sana kwa samaki akitumia direct au indirect kikioza kinazalisha wadudu ambao samaki ushambulia dakika chache kimeisha
 
Aliye leta ile taharuki akamatwe na kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi
 
Nimecheka kwa sauti at Ng'ombe mmoja anatoa kinyesi Cha kilo 25 kwa siku serious?? Pia Ng'ombe Mmoja anakojoa Lita 21 kwa siku yaani ndoo nzima kubwa ya mkono na sehemu.Hata watanzania mmewaona ni wajinga hampaswi kuwadharau kiasi hiki
Muwe mnasoma. Hilo ni kweli na hizi ni ng'ombe za kiswahili. Wa kizungu wanatoa mpaka kilo 45 kwa siku.
Hayo mengine ya ripoti nipo dillema. Ni ngumu kuwaamani wanasiasa kwa sababu tayari washatudanganya kwenye mambo mengi.
 
  • Thanks
Reactions: F4B
Hiyo tume ilikuwa na watu wa hydrology? Seepage analysis ya eneo hilo ilifanyika? Naunga mkono hoja.
 
Muwe mnasoma. Hilo ni kweli na hizi ni ng'ombe za kiswahili. Wa kizungu wanatoa mpaka kilo 45 kwa siku.
Hayo mengine ya ripoti nipo dillema. Ni ngumu kuwaamani wanasiasa kwa sababu tayari washatudanganya kwenye mambo mengi.
Kiongozi nisaidie nikajiongezee experience kumbuka practically inaweza isiwe kweli lkn ducumentary inaweza ikawa sawa
 
Kuna uhasama Kati ya mgodi na WANANCHI ambao hauwezi kuisha kila siku WANANCHI kuuzunguka mgodi WANAFANYA kila wanachoweza ili kujaribu kuvamis na KUPORA madini imelazimika kuweka ulinzi mkubwa Kwa ghalama kubwa.Wazee wa mazingira wamekuwa wakipishana ili kuhakiki hali ya usalama na namna MAJI taka yanavyo tibiwa.

Migodi binafsi inaendelea na Kazi bila TAHADHALI yoyote na hakuna kinachofanyika.

Kuhusu uchafuzi wa MTO taasisi za uchunguzi zinapaswa kuaminika.
Big up Mkuu. Kinachifanyika ni kukwepa kuwawajibisha wenye mgodi. Ukifika pale mgodini kuna maji yanatirishwa kwenye mto. Kamati ilitakiwa ichukue sampuli za maji hayo ili yapimwe na matokeo yake yaambatanishwe na ripoti hiyo kuliko kuwasingizia ng'ombe.
Mifugo imekuwepo miaka na miaka na no part and parcel ya maisha yetu na mito hiyo inamwaga maji yake kwenye maziwa kama Nyasa na hatujawahi kusikia uharibifu huo.
 
Hichi kinyesi na hiyo mikojo mbona miaka hiyo yote hakijawahi kuchafua huu Mto tena na idadi ya ng`ombe imepungua sana siku hizi.
 
Screenshot_20220323-213539.png
 

Attachments

"...VIFO VYA SAMAKI MARA NA NEMC YETU by Yahya Msangi

Onyo: kama WA kusoma hadithi na kutizama cartoon pita zako hapakufai!

Nimesoma dondoo (exécutive summary) ya report ya Tume. Kuna mizaha sana nchini. Kinyesi na mkojo kiasi kile? Kiliagizwa toka Ukraine au Yémen? Hivi kweli NEMC hamuoni soni?

Hii NEMC ina historia chafu mno. Huenda wengi hamuijui au mumesahau. Nikumbushe vituko vichache VYA NEMC:

1. 1992 kulifanyika mikutano uliitwa "EARTH SUMMIT" aka Rio Conference on Sustainable Development". Nilihudhuria mkutano huu nikiwakilisha kundi la wafanyakazi duniani. Waziri wa Nje alikuwa larehemu Hassan Diria. Ujulbe wa NEMC ulihusisha mahawara wa aliyekuwa mkurugenzi na wenzie. Mgogoro huu ulizungulzwa mon kwenye Gazeti la MOTO MOTO enzi za marehemu STAN KATABALO. Uozo haukuishia kwenye ujulbe wa NEMC bali hâta msafara wa wizara. Msafara WA wizara ulijaa wake, mahawara na watu wasiohusika. Baadhi waliishia London! Wakasubiri watu wao warudi toka Rio Janeiro! Wakawapitia na kurudi nyumbani. Kituo Cha mwaka ni wingi wa msafara wa Tanzania. Ilisemeka a Japan kupitia JICA ndio walifadhili ujulbe wa Tanzania. Msafara wa Tanzania ukawa mkubwa kuliko wa Japan! Bila aibu yakakodishwa limosines kuhudumia msafara wa Tanzania! Msafara huu wengi wao wakawa hâta mkutano hawahudhurii. Wao na Copa Cabana na Ipanyema beach! Mwaka 2012 ukifanyika Earth Summit II (Rio+20). Nilikaa hoteli jirani na Copacabana. Walipoona passport yangu wahudumu wakakumbukia 1992! Tuliacha sifa mbaya ya watanzania kuwa watu wa matanuzi! Nakumbuka 1992 jinsi wajapani walivyotushangaa! Wenzenu wanatanua kuliko wafadhili. Wenye nakala za gazeti la moto moto mwana 1992 warejee. Vituko hivi vilielezwa kwa kina na majina yaliyajwa.

2. Mara tu baada ya kudundwa NEMC aliteuliwa marehemu R. Mengi kuwa mkiti! Wenye uelewa tukapinga! Tukaambiwa tuna wivu. Hoja yetu ilikuwa hii: Mwenye uwezo wa kuharibu mazingira kwa kiwango kikubwa (potential and serious polluter) unampaje uenyekiti wa baraza la kuhifadhi mazingira ? Enzi hizo hâta hizi asasi za mazingira hazikuwapo na zilizokueopo uchwara mwingi! Mengi akaungwa mkono! Haukupita muda ikazuka migogoro na wenzie. Ikawa NEMC inakagua wenzake na kuwapiga faini na kuwafungia. Kiwanda Cha KTM Mbagala ni mfano hai! Ndioo wahusika wakaona mantiki ya hoja yetu! Kina Bonite na wenzao wakichafua mazingira NEMC wanajifanya vipofu! Hatimaye Mengi akaondolewa lakini baada ya uharibifu mkuubwa.

3. Ukitaka Kujenga haswaa viwanda au mradi mkubwa unatakiwa ufanye KITU inaitwa ESIA (Environmental and Social Impact Assessment). Ili ESIA ifanye kazi unatakiwa ifanywe na mtu au taasisi huru n'a yenye wataalamu wabobezi na waaminifu. Na report yao ikaguliwe na chombo cha kitaaluma.

Lakini pale NEMC ukazuka ufisadi. Mkurugenzi WA NEMC (Namhifadhi) akaanzisha utaratibu wa kuomba wadau wanaotaka kufanya EIA wampeleke maombi kwake na waingizwe kwenye orodha ya "qualified EIA specialists). Matokeo zikaanzishwa taasisi zikapeleka maombi. Ukizichunguza taasisi zilizopitishwa utabaini ni za mkurugenzi na maafisa wa NEMC. Ikitokea tender mkiomba zitapewa wao. Hâta kama hazikidhi vigezo. Nadra kusikia kuna mradi umekataliwa kwa kuwa ESIA inaonyesha utaathiri watu na mazingira! Wakishapewa héla ya tender na wakitathmini wanaonyesha Kuna uharibifu. Mazungumzo yanafanyika na wawekezaji. Wanakula pwani na bara! Mamilioni yanakombwa. Mradi ukijakuleta madhara wao weshaweka chao kiunoni. Mtajiju!
Ukitaka kapitie ESIA zilizopo NEMC! Utazungushwa usizione. Miaka nenda miaka rudi wanafanya EIA walewale! Copy and Paste!

Nina hakika hâta huo mgodi wa mara utaratibu uliotumika ni huu!

Huu mgodi siijui una zimwi? Kuna wakati badala ya kupeleka wataalamu bunge lilipeleka wabunge kuuchunguza! Halafu Éti wamiliki wa mgodi wakagharamikia safari mpaka usafiri wa helikopta! Toba! Mtuhumiwa analipa makachero wakamchunguze!

Je kifanyike nini ukweli kuhusu vifo vya samaki ujulikane? Tujue mkojo na mavi kiasi kile waliagiza meli ngapi?

1. Wataalamu wakapitie ESIA iliyosababisha kibali kutolewa. Je EISA ni ya kiwango stahiki? Aliyeifanya akipatikana kwa utaratibu upi? Kama EISA Iko Sawa je kilicho kwenye EISA kinazingatiwa n'a mamlaka na mwekezaji? Nani anakagua? Je kwa muda na utaratibu uliopo kisheria?

2. Mgodi unatumia kemikali Gani? Zipo zilizopigwa marufuku? Mgodi unamwaga wapi maji taka? Mtoni? Kama sio mtoni wapi? Wana constructed wetlands? Mabwawa ya "kupoozea" au "kutakasa" sumu? Kama mabwawa yapo yana mimea au bakteria husika (bioremediation plants or bacteria?

3. Sample za samaki, maji, viumbe hai chini ya mto (benthic organisms) zichukuliwe zikafanyiwe analysis kwa mkemia mkuu. Ni Siku chache majibu yatapatikana. Majibu haya yalinganishwe na kemikali zinazotumuka mgodini. Je majibu yanafanana n'a kinyesi na mkojo au na kemikali za mgodini?

Bila haya ni usanii tu WA NEMC, Mgodi na wanasiasa.

Nieleze jinsi tuliwabana Mribwa sugar KIPINDI fulani. Kuna mto unapita JIRANI na kiwanda. Nadhani iLIKUWA 2002 walionekana samaki (kambale) wamekufa kama hivi n'a Watoto kutokwa mapele baada ya kuongelea. Baada ya danadana tuliamua kuingia mzigo! Tukashuka samples za kambale na maji. Tukazipeleka SUA kwenye maabara. Tukachunguza kiwanda cha sukari. Tukakuta bado kilikuwa kinatumia sulphur kusafishia sukari! Madini ya sulfur yametulika sana kufanya sukari uwe "nyeupe"! Kutokana na madhara ya sulfur ukipigwa marufuku kung'arisha sukari. Lakini ndio njia ya bei nafuu na wenye viwanda wasipozuiwa hawaachi kirahisi! Majibu ya uchunguzi wa kimaabara na uchunguzi kiwandani ukabaini pasipo shaka kuwa Mtibwa ilikuwa inatumia Sulfur kung'arisha sukari!

Licha ya matokeo ya kitaaluma bado Mtibwa haikushughulikiwa na SERIKALI! Tukaamua kupanda Juu! Wazalishaji sukari wana shirikisho la Kimataifa. Tukapeleka huko na kulisimamia. Matumizi ya sulfur yakaisha. Sina uhakika baada ya sie kuondoka walirudia? Kama walirudia nyie bugieni sukari! Mtajua mbele ya safari.

Nyie wanaharakati uchwara. Badala ya kushinda space na Twitter mnatangaza kesi mnaonaje mkifuatilia mambo kama haya?...""
 
Back
Top Bottom