Ripoti ya Uchunguzi wa pesa zilizotolewa BoT kupokelewa Juni 30, 2021

Ripoti ya Uchunguzi wa pesa zilizotolewa BoT kupokelewa Juni 30, 2021

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hii ni moja ya habari katika magazeti ya leo na pia iko mitandaoni, hivyo wacha tusubiri hiyo kesho kusikia kilichomo katika hiyo ripoti.

Swali ni je, ripoti hiyo itajibu maswali watu waliyonayo au ndio itaongeza maswali na pengine kukatisha watu tamaa?

Kuna mtu ukimuona amehudhuria uwasilishaji wa hiyo ripoti, basi usitegemee la maana kwani sidhani kama anaweza kuumbuliwa na yeye akiwa yupo katika eneo la tukio unless wamfiche jambo ambalo nalo si rahisi kutokea.

Tusubiri.
 
Kuna mtu sahvi,
Kimba linagonga kyupi na kurudi[emoji4]
 
[emoji4]
IMG_20210607_120644.jpg
 
Mama ameitafakari sana naona pamepoa sitaki kuamini kwamba hii itakayosomwa ndio Ile version original.

Anyway hakuna namna maana lazima nchi iendelee na wengine wapewe maonyo tu watulize mazaga yao maana walimzingua sana maza.

Walileta madharau ya wazi na kutaka kuipindua Katiba simply yale mabadiliko ya 1984 ambayo yalifuata American system ya kuwa na Makamu wa Rais hayakutoa maelezo mengi ila hawakujua kwamba Makamu ni kiraka anakaa pale ili mkulu akidanja hatuingii kwenye uchaguzi maana inaweza kuleta machafuko.

Hawakujua kwamba Makamu wa Rais anapaswa kuapishwa kwanza kabla ya kuendelea na maziko maana nchi haipaswi kukaa bila Mkuu wa nchi hata kwa dakika moja.

Hiyo ndio maana ya kile kofungu cha Katiba, thanks to General Mabeyo.
 
Inaweza kabisa kufanyiwa uchakachuaji na hivyo kuambiwa ripoti haina chochote kibaya au pesa zilizochukuliwa taratibu zote zilifuatwa. Kumbuka CAG Kichere alipotoa ripoti yake nadhani ilikuwa mwishoni mwa March au mwanzoni mwa April maCCM walimtishia maisha yake.
 
Inaweza kabisa kufanyiwa uchakachuaji na hivyo kuambiwa ripoti haina chochote kibaya au pesa zilizochukuliwa taratibu zote zilifuatwa. Kumbuka CAG Kichere alipotoa ripoti yake nadhani ilikuwa mwishoni mwa March au mwanzoni mwa April maccm walimtishia maisha yake.
Usemalo linawezekana kabisa kwani CCM ni ile ile.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hii ni moja ya habari katika magazeti ya leo na pia iko mitandaoni, hivyo wacha tusubiri hiyo kesho kusikia kilichomo katika hiyo ripoti...
Jamaa kapewa safari ya ufaransa huko ngoja tuone itakuaje sidhani kama hiyo tarehe atakua kasharudi nadhani kama ni kweli Itakua Noma sana
 
Inaweza kabisa kufanyiwa uchakachuaji na hivyo kuambiwa ripoti haina chochote kibaya au pesa zilizochukuliwa taratibu zote zilifuatwa. Kumbuka CAG Kichere alipotoa ripoti yake nadhani ilikuwa mwishoni mwa March au mwanzoni mwa April maccm walimtishia maisha yake.
Yeah sure, lakini pia yawezekana wakawa wameambiwa warudishe mchuzi mambo yaishe kiutu uzima then wakae kimya kama adhabu yao.
 
Hilo linawezekana kabisa Mkuu. Ngoja tusubiri kusikia ripoti husika, ila maccm yote machafu, majizi na mafisadi hivyo kukingiana vifua ni jadi yao.

Better the devil you know than the angel you don't know.
 
Inaweza kabisa kufanyiwa uchakachuaji na hivyo kuambiwa ripoti haina chochote kibaya au pesa zilizochukuliwa taratibu zote zilifuatwa. Kumbuka CAG Kichere alipotoa ripoti yake nadhani ilikuwa mwishoni mwa March au mwanzoni mwa April maccm walimtishia maisha yake.
Yaani serikali ya CCM ijifanyie uchunguzi halafu itoe ripoti inayoichafua serikali??

Hahahahaa jamani eeeh…tutumiage akili zetu tulizozaliwa nazo!
 
Inawezekana inasomwa kwasababu ya lile shinikizo lililokuwepo, kama ndio hivyo, basi pasitegemewe kuwepo na chochote cha maana, hao jamaa kulindana ni jadi yao.
 
27 June 2021
Tanga, Tanzania

MKUTANO MKUU WA BARAZA LA BAKWATA

Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango hii leo Juini 27,2021 amefungua Mkutano mkuu wa baraza la waislamu Tanzania (BAKWATA) Unaofanyika Jijini Tanga.

Makamu wa Rais amewahakikishia BAKWATA kwamba serikali ipo pamoja nao na ipo tayari katika kupokea ushauri na maoni watakayotoa juu ya mwenendo wa serikali wakati wowote.

Makamu wa Rais amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa , kuwahimiza wananchi kufanya kazi ambazo ni halali, kudumisha Amani na umoja katika taifa, kusisitiza maadili mema kwa jamii pamoja na umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha Makamu wa Rais amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuwahimiza waumini kuchukua tahadhari juu ya janga la corona, ikiwa ni pamoja na kufuata maelekezo byote yanayotolewa na wataalamu wa afya nchini.

Makamu wa Rais amesihi BAKWATA, Viongozi wote wa dini ya Kiislam na dini nyingine na pia Wakuu wa Taasisi zote za Dini kujitahidi kuziendesha Taasisi hizo kwa mujibu wa Katiba zao na mafundisho ya Dini.

Awali akisoma hotuba ya BAKWATA Katibu wa Baraza hilo Sheikh Nuhu Jabir Mruma amesema Bakwata itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na kuwahimiza waumini wa dini ya kiislamu kulipa kodi kwa manufaa ya taifa.

Kwa Upande wake Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakar Zuber Bin Ali amewataka waislamu nchini kote kuongeza umoja na mshikamano ambao utaleta utulivu katika nchi.
 
Inatakiwa iwe hivyo lakini haiko hivyo ni viini macho tu vya kutuzuga Watanzania. Kama CAG anatishiwa kuuawa na Rais na Serikali yote iko kimya kukemea vitisho hivyo na kuwasaka wahusika ili wapandishwe kizimbani. Kweli ccm ni ile ile hawana jipya.
Yaani serikali ya CCM ijifanyie uchunguzi halafu itoe ripoti inayoichafua serikali??

Hahahahaa jamani eeeh…tutumiage akili zetu tulizozaliwa nazo!
 
Aliona kuna shida pahala....akataka uchunguzi....na sasa ripoti imetoka
tuwe wavumilivu maana angeweza kukaa kimya.
na hapa kuna watakaochomoka mazima.
nakuamini sa100
 
Hii ni moja ya habari katika magazeti ya leo na pia iko mitandaoni, hivyo wacha tusubiri hiyo kesho kusikia kilichomo katika hiyo ripoti.

Swali ni je, Ripoti hiyo itajibu maswali watu waliyonayo au ndio itaongeza maswali na pengine kukatisha watu tamaa?

Kuna mtu ukimuona amehudhuria uwasilishaji wa hiyo Ripoti, basi usitegemee la maana kwani sidhani kama anaweza kuumbuliwa na yeye akiwa yupo katika eneo la tukio unless wamfiche jambo ambalo nalo si rahisi kutokea.

Tusubiri.
Tukae mkao upi?
Tunaendelea na teuzi
Hakuna jipya
Katiba Mpya
Tutawawajibissha mbele ya safari
 
Back
Top Bottom