Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ikiwa Uhuru utatishiwa, basi Demokrasia na Uchaguzi vyote vitaathirika, kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, mazingira ya Vyombo vya Habari yalijipambanua kwa kufungiwa kabisa kufanya kazi, kuzuiwa kwa muda, kufutwa kwa leseni na kuporomoka mno katika vipimo vinavyoonesha viwango vya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Mwaka 2016, Gazeti la Mseto lilifungiwa kwa miaka mitatu, Mwaka 2017 Tanzania Daima lilifungiwa kwa siku 90, mwaka 2017 Gazeti la Mawio lilifungiwa kwa miaka miwili, mwaka huo huo pia Gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa kwa miaka miwili na Mwaka 2019 Gazeti la The Citizen lilifungiwa kwa siku saba.
Mwaka wa Uchaguzi wa 2020, Vyombo vitatu vya Habari viliadhibiwa. Juni 23, 2020, miezi miwili kabla ya kuanza kwa Kampeni za Uchaguzi, Serikali ilifuta leseni ya uchapishaji ya
Gazeti la Tanzania Daima, sababu zikatajwa kuwa ni gazeti kuendelea kukiuka Sheria za Nchi na maadili ya taaluma ya Uandishi wa Habari.
Ukijibu hatua hii, Juni 25, 2020, Ubalozi wa Marekani nchini ulitoa tamko ukionesha kuguswa na “ufutaji wa leseni ya gazeti linalomilikiwa na upande wa upinzani”.
============
Ripoti za ufuatiliaji na Ripoti za Tafiti zilizopita kuhusu uripoti wa Vyombo vya Habari wakati wa Chaguzi Kuu nchini zimebainisha mianya kadhaa ikiwemo;
Kuegemea na kupendelea upande mmoja katika ushindani ambao ni Chama Tawala (CCM) na Wagombea wake
Uripoti mbaya wa wagombea Wanawake. Kuegemea zaidi kwa Wanaume na uripoti unaoegemea matukio ya habari badala ya masuala ya msingi yanayogusa Jamii.
Kutokuzingatiwa kwa viwango vya kitaaluma kwa Vyombo vya Habari na Waandishi, ikiwemo kuwa na Habari zenye vyanzo mbalimbali vya Habari.
Kutokuwepo kwa uwiano sawa wa Uripoti kwa walioko madarakani kunakofanywa na Vyombo vya Habari vya Serikali.
Kutokuzingatia utoaji nafasi kwa usawa kwa Vyama vya Siasa na Wagombea, hivyo kuwanyima raia Haki yao ya kupata taarifa za pande zote mbili.
Kushindwa kuwahoji Wagombea kuhusiana na kutekelezeka au kutimizwa kwa ahadi, tuhuma au matamshi wanayoyatoa kwenye Uchaguzi.
4.1 Uripoti wa chaguzi mbalimbali
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 ulijumuisha upigaji kura wa aina mbalimbali (za urais, ubunge, uwakilishi [kwenye Baraza la Wawakilishi-Zanzibar] na udiwani) kwenye muungano na Zanzibar.
Uchaguzi wa Rais wa Muungano uliripotiwa kwa kiwango kikubwa cha asilimia 43 ya habari zote zihusianazo na uchaguzi zilizochunguzwa ukifuatiwa na uchaguzi wa wabunge uliopata asilimia 28, uchaguzi wa rais wa Zanzibar uliopata asilimia 20, uchaguzi wa madiwani Tanzania Bara asilimia 10, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi asilimia 5, na madiwani wa Zanzibar asilimia 1.
Ni asilimia 32 tu ya habari zilizohusiana na uchaguzi zilikuwa na masuala nje ya makundi haya manne ya uchaguzi.
Uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ulihusisha asilimia 5 ya habari zote zilizofanyiwa uchambuzi, ikiwa ni pungufu kuliko zile za udiwani kwa Tanzania Bara uliokuwa na asilimia 10.
Hali hii inaweza kuhusishwa na ukweli kwamba sampuli kubwa ya vyombo vya habari ilichukuliwa kutoka Tanzania Bara ambapo palikuwa na sampuli 28 kati ya 33 zilizofanyiwa uchunguzi.
Vyombo vya habari vya Tanzania Bara viliripoti habari za uchaguzi wa muungano kwa asilimia 83 ikilinganishwa na chaguzi za Zanzibar zilizoripotiwa kwa asilimia 17.
Vyombo vya habari vya Zanzibar viliripoti uchaguzi wa Zanzibar
kwa asilimia 70 ikilinganishwa na zile za muungano zilizoripotiwa kwa asilimia 30 tu. Hii inadhihirisha kwamba vyombo vya habari vinaangalia zaidi maeneo vilivyopo.
Vyombo tofauti vya habari viliripoti uchaguzi wa rais Tanzania Bara na Zanzibar kwa namna tofauti. Raia Mwema na Uhuru viliripoti uchaguzi wa rais wa muungano mara nyingi zaidi ya vyombo vingine vya habari kwa asilimia 56, vikifuatiwa na The Citizen asilimia 54, TBC Taifa asilimia 53, Mwananchi asilimia 51, na Azam TV asilimia 44.
Kwa upande mwingine, uchaguzi wa rais wa Zanzibar uliripotiwa zaidi na ZBC Radio kwa asilimia 41, Zanzibar Leo asilimia 38, Chuchu FM asilimia 34, ZBC TV asilimia 32, Zenji FM asilimia 31, na Azam TV asilimia 24.
Licha ya utofauti uliojitokeza, baadhi ya vyombo vya habari vilijitahidi kuripoti chaguzi zote mbili. Kwa mfano Azam TV waliripoti kuhusu uchaguzi wa Rais wa muungano kwa asilimia 44 dhidi ya asilimia 24 za uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.
Wakati Daily News waliripoti kwa asilimia 42 dhidi ya asilimia 17, Mwananchi asilimia 51 dhidi ya asilimia 18 na Uhuru asilimia 56 dhidi ya asilimia 18.
Visababishi vya Uripoti kuhusu Uchaguzi
Ukiviangalia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali, uripoti wa uchaguzi uliofanywa na gazeti la Zanzibar Leo kwa matukio ya CCM na kwa vyama vya upinzani haukuwa na usawa kwa asilimia 44 dhidi ya asilimia 15 mtawalia, Habari Leo kwa asilimia 41 dhidi ya asilimia 22, TBC Taifa asilimia 44 kwa CCM ikilinganishwa na asilimia 19 kwa vyama vya upinzani.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa ZBC Radio ambayo iliripoti matukio ya CCM kwa asilimia 69 dhidi ya asilimia 5 kwa upinzani. Hali ilikuwa kama hiyo pia kwa TBC1 ambayo iliripoti matukio ya CCM kwa asilimia 14 dhidi ya 7 kwa upinzani. Kwa ZBC TV ilikuwa asilimia 33 kwa CCM dhidi ya asilimia 21 kwa upinzani.
Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti zaidi matukio au matamko ya vyama vya upinzani kuliko yale ya CCM. Vyombo hivi ni pamoja na The Citizen asilimia 40 kwa upinzani ikilinganishwa na asilimia 17 kwa CCM, Mwananchi kwa asilimia 42 kwa upinzani ikilinganishwa na asilimia 20 kwa CCM, Mwanahalisi Online asilimia 46 ikilinganishwa na asilimia 24, Nipashe asilimia 34 dhidi ya asilimia 27, na ITV asilimia 31 kwa upinzani dhidi ya asilimia 18 mtawalia.
Ukiangalia kwa ukaribu uripoti huu wa vyombo hivi vya habari utabaini kwamba, vyombo hivi viliripoti matukio mbalimbali kuanzia vyama tofauti vya upinzani (Chadema, ACT-Wazalendo, CUF, NCCR-Mageuzi), mpaka masuala ya uchaguzi, na siyo chama kimoja tu. Jedwali picha hapa chini linaonesha matukio gani yalileteleza uripoti wa habari zote zilizofanyiwa uchambuzi.