Ripoti ya wataalamu wa UN yaitia hatiani Rwanda kuivamia DR Congo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ripoti ya wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa wanajeshi wa Rwanda walifanya mashambulizi ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kulisaidia kundi la waasi la M23.

Ugunduzi huo unafuatia miezi kadhaa ya mvutano kati ya DRC na Rwanda, kuhusu kundi hilo lenye sifa mbaya.

Kongo imeilaumu mara kwa mara Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao, ambao waliteka maeneo makubwa ya Kongo katika miezi ya karibuni, tuhuma ambazo Rwanda inazikanusha vikali.

Lakini kwa mujibu wa ripoti hiyo ya wataalamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yenye kurasa 131, Rwanda imefanya uingiliaji wa kijeshi katika ardhi ya Kongo tangu alau Novemba 2021.

Pia imesema Rwanda ilitoa wanajeshi makhsusi kwa ajili ya operesheni za M23, hasa wakati kundi hilo lilipoteka miji na maeneo ya kimkakati.

Ripoti hiyo pia imebaini kuwa wanajeshi wa Kongo wamekuwa wakitoa msaada kwa makundi yenye silaha katika eneo linalozongwa na machafuko la mashariki.

DW
 
Lakini si juzi juzi tu Bintu Keita alitangaza oposite na haya!!!! Au kwa Vile Congo inawafukuza ndi wanataka kutangaza story ambayo Congo inataka kuisikia Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom