Risasi sio suluhisho (kumbukumbu zangu 1996)

Risasi sio suluhisho (kumbukumbu zangu 1996)

Nelson Jacob Kagame

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2022
Posts
9,576
Reaction score
13,545
Ilikua usiku wa manane simu ikaita, na mara nyingi namba za nje ya nchi inamuwiaga vigumu kupokea..Akapokea na moja kwa moja sauti akaitambua ni ya nani""Safari hii mpigaji anazungumza vizuri kiswahili kuliko awali"".

Mpigaji alikuja na ofa na akaiweka wazi kwa mlengwa namaanisha mpigiwaji simu.Kuna valid item inatakiwa ichukuliwe kutoka kwa muhusika kabla makachero wengine hawajaiwahi na kuharibu mpango endelevu.

Na mpaka simu hii inapigwa muhusika yupo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Senou pale Bamako na haijulikani anaunganisha ndege ya kwenda wapi,ila cha muhimu kinachotakiwa ni mzigo alioubeba kwenye begi zake ndogo mbili.

Baada ya maelezo hayo mafupi mpigaji akawa kimya kisha akauliza""Upo tayari komredi kuchukua hii ofa"""au tuwape wale wayahudi?. Una dakika kumi na moja za kunipa jibu.

Kijana akapata ukakasi kujibu,kwanza simu imekuja ghafla,pili hataki ugomvi tena na vyombo vya dola vya nchi yoyote ile na tatu hataki kuiweka roho yake rehani kisa pesa, maana hajui hii oparesheni kiundani asije kua mbuzi wa kafara kuwanufaisha wanasiasa.

Kilichomuumiza kichwa ni kua ukikataa ofa ni kama umevunja kiapo na malipo yake ni kuonekana msaliti au mhaini unayestahili kifo ndani ya taasisi.

Bila kusita akasema nimekubali nipe details mkuu,nijue naanzia wapi.Na pia mkuu hakikisha target yetu pale Bamako Senou international airport, hapandi ndege za kwenda Athens au Kigali au Bangui au Brazzaville,ila arudi N"Djamena itakua kazi rahisi.

Na yeye kijana tumwite""Nyakamba"akasema baada ya 44hrs atakua Kabalaye akimsubiria amalize kazi ya kumpokonya mizigo hitajika..Nanukuu""Fanya chochote unachoweza mkuu jamaa arudi Chad"""mwisho wa kunukuu.

Mpiga simu akauliza nikuwekee kiasi gani cha pesa cha kuanzia operasheni,na akajibiwa dola elfu tisini za kuanzia zipatikane akifika Nairobi atazichukua cash na hati ya kusafiria ya Uganda pamoja na hati ya kusafiria ya Tanzania.

Baada ya hapo akifika Nairobi akute tiketi za ndege kwenda Bangui zipo tayari mezani.Mpiga simu akasema tutakutana kesho jioni Nairobi na akakata simu.

Nyakamba hakupata usingizi tena akaanza kuwaza mambo mengi sana na akakumbuka misheni ya mwisho ilivyofeli vibaya na akaishia kua mtu anaetafutwa na vyomba vya ulinzi na usalama nchini Congo Brazzaville.

Lakini akajipa moyo hii ndio kazi aliyoichagua cha msingi ni awe tu mwangalifu,akaamka na kuanza kujiandaa na safari ya kesho kwenda Nairobi kukutana na mkuu.

ITAENDELEA...
Kufika asubuhi na mapema hii ilikua july 16 1996 kijana Nyakamba anasikia honi nje ya geti la nyumba aliyokua amepanga kule kurasini kota""Pooh pooh""na upigaji wa honi hii ulikua sio mgeni kwake sababu ni code za mawasiliano za washirika wa taasisi.Fasta fasta akajua kumeiva akatokea mlango wa nyuma wa ua ya ile nyumba mpaka barabarani akaisogelea ile gari kwa nyuma.Mazungumzo yakawa hivi na yule mtu aliekaa kwenye usukani wakaanza kuzungumza kwa lugha ya kinyarwanda na kifaransa kwa sauti ya chini kabisa.
NYAKAMBA: Kaka sio kawaida yako kunipigia honi kwa code hiyo vipi kuna tatizo na usijisahau kaka tupo nchi ya watu huwezi kujua watu wanaotuzunguka.
DEREVA: Ndugu ebu tulia kwanza nisikilize kwa umakini""Jana ulipokea simu""namaanisha ulipokea simu kutoka kwa mkuu???
NYAKAMBA:Ndio kaka nilipokea maagizo ambayo ni amri siwezi kuyapinga na leo mchana naondoka kwenda nairobi kupokea maagizo zaidi na vitendea kazi.
DEREVA:Ndugu hivi mkuu amekupa details kamili kuhusu hiyo oparesheni????
NYAKAMBA:Hapana ndugu
DEREVA:Nyakamba wewe ni ndugu yangu sitokuficha kitu na unakumbuka yaliyotukuta kule Congo Brazzaville na sitaki yajirudie na pili tutafanyia kazi hawa wanasíasa mpaka liní???.Hii fursa tuitumie kaka na sisi tujitajirishe au wewe hutaki kupigiwa saluti na kutandikiwa zuria jekundu???
NYAKAMBA:Ndugu tukutane nairobi kesho tuzungumze hili suala maana hapa tulipo sio salama sana kulijadili hili suala na ukumbuke Kisangani hakukaliki waganda wamevamia na wenzetu wote wamekimbilia Burundi ili warudi Ubelgiji hakuna maisha tena Zaire.
DEREVA:Sawa kaka kesho nitakuepo nairobi ila kumbuka lengo ni sisi kujitanua ili tufikie malengo na hii ndio fursa hata mkuu ikibidi tumzunguke tu kwa manufaa yetu katika hii operasheni.
NYAKAMBA:Ndugu tutazungumza nairobi,na ukiwa dar es salaam usipende sana kutumia magari yenye namba za usajili za ubalozi.Be careful subiri nije unifikishe kariakoo.
Nyakamba akarudi ndani akachukua begi lake akafunga mlango wa ile nyumba na kumwita mlinzi afu akampa maelekezo mafupi kisha akatoka nje akapanda ile gari kuelekea kkoo.
Hawakujua kua nyuma yao walikua wanafuatiliwa na makachero wa serikali ya Zaire waliokua wanamuziki pia wa Bendi maarufu hapa mjini Dar es salaam,lakini bahati ilikua upande wao maana wale makachero walipata hitlafu ya gari lao hivyo wakaacha kuwafuatilia.Lakini Nyakamba alihisi kitu ndio maana walipofika kariakoo akamwambia dereva ""nipeleke uwanja wa ndege niende nairobi mda huu sababu kuna mtu ana tiketi yangu ya kwenda nairobi ananisubiri,ila chochote tulichoongea ibakie siri yetu""na tuzingatie kiapo.
ITAENDELEA..............
July 17 inamkuta Nyakamba ndani ya mitaa ya Kayole Nairobi amekwisha onana na mkuu na kupewa vitendea kazi kwa oparesheni ile alioitiwa.Lakini kuna kitu aliona hakijakaa sawa alipokua anaongea na mkuu.Na akajiapiza kama mkuu ana mpango wa kumsaliti basi ataanza yeye kuwasaliti na kutokomea sababu Zaire hakuna maisha tena kwa upande wake.Pale nairobi hakutaka kuzurura kabisa alikaa ndani pale kwa mkuu kusubiria tu aletewe hati zake za kusafiria akatimize wajibu.Lakini kichwani alikua na mawazo mengi maana aliona hakuna haja ya kupokea amri kutoka kwa serikali inayoelekea kupinduliwa,lakini viapo alivyoapa vilimfanya atulie kwanza.
SIMU TATA:Mara akaona simu yake ya mkononi inayotumia satellite inaita"Kumbuka huo mwaka 1996"simu za mkononi zilikua chache hasa kwa maeneo mengi ya afrika.Yeye alikua na simu ya satellite sababu alikua mfanyakazi wa ubalozi wa Zaire nchini Tanzania kama kazi yake kivuli.
SIMU TATA:Mpigaji alikua yule dereva waliekutana kule dar es salaam nchini tanzania mitaa ya kurasini alipokua amepanga karibia na kota za wafanyakazi wa bandari.Na mazungumzo yao yalikua kwa lugha ya kinyarwanda na kibangubangu hawakuongea kuswahili tena.
SIMU TATA:Kaka unajua waasi wanakaribia kinshasa na hakuna wa kuwazuia.
NYAKAMBA:Kwani Kongolo yupo wapi mpaka mda huu???
SIMU TATA:Kongolo anaharibu mambo kutokana na umri wake na watu wanaogopa kumwambia ukweli kwa heshima ya mzee.
NYAKAMBA:Nenda moja kwa moja kwenye pointi ndugu.
SIMU TATA:Inaweza kutuchukua miaka kumi mpaka ishirini kurudi tena Kinshasa kaka.Sasa ukumbuke mpango wetu ukifika N"Djamena.Maana hata siku ile nilipokuja kwako pale dar es salaam tulikua tunafuatiliwa,kabla hawajatusaliti lazima tuwaonyeshe sisi ni akina nani.
NYAKAMBA:Tukutane N"Djamena usipige simu tena sio salama kwa sasa sababu hakuna wa kumwamini.
SIMU TATA:Sawa kaka tukutane N"Djamena umeeleweka vyema.

Nyakamba alikua anawaza mengi sana kichwani,kama kinshasa itaangukia mkononi mwa wale wanyarwanda basi hana kitu tena.Lakini akajiapiza kua lazima apambane na lolote litakalokuja mbele hakuna jinsi na mambo mengine atayamaliza baada ya kujua hatima ya hii oparesheni.
Jioni ile palepale kayole kwenye ile nyumba ya mkuu,kila kitu kikawekwa sawa kwa ajili ya kazi baina yake na mkuu na malipo ya pesa cash za kianzio akapewa.Kilichobaki kilikua ni kupata zile hati za kusafiria ili apande ndege kuelekea Bangui kama mfanyakazi wa WFP tawi la Kenya,na akifika Bangui atatafuta usafiri wa kuingia Chad either kwa kupitia Cameroon au ndege za umoja wa mataifa.
Kuhusu target (Mlengwa) taarifa zikaja kua yupo tayari ndani ya ndege na atatua uwanja wa kimataifa wa Chad pale N"Djamena international airport (IATA) baada ya masaa matatu ila ni kwa upande ule wa ndege za kijeshi sio upande wa ndege za kiraia na amebeba item zote anazotakiwa kunyanganywa.Hiyo ilikua tarehe 17 July 1996 saa mbili na dk 45 usiku kwa saa za afrika mashariki na saa moja na dk 45 usiku kwa saa za afrika ya kati.
Hati za kusafiria zililetwa na Nyakamba akafanikiwa kupata ndege ya umója wa mataifa akafika Bangui usiku ule kutokea nairobï.Na kutokea Bangui akapata ndege ya mizigo ya WFP mpaka N"Djamena hiyo ilikua tarehe 19 July 1996.Akafikia mitaa ya Kabalaye moja ya vitongoji vilivyochangamka jijini N"Djamena Chad.
 
Huu uzi nilipigwa marufuku 🔫🔫🔫🔫🔫🔫na wenye story zao kuendelea nao mkuu.
Wachambuzi wa habari waga tunatii sheria bila shuruti mkuu.
Bado naipenda Ndjamena na Kinshasa na Bangui,,nina ndugu zangu kule.
BILA KATAZO NINGEENDELEA NAO NISIMULIE ANGUKO LA MZEE MOBUTU SESESEKO.
 
Huu uzi nilipigwa marufuku 🔫🔫🔫🔫🔫🔫na wenye story zao kuendelea nao mkuu.
Wachambuzi wa habari waga tunatii sheria bila shuruti mkuu.
Bado naipenda Ndjamena na Kinshasa na Bangui,,nina ndugu zangu kule.
BILA KATAZO NINGEENDELEA NAO NISIMULIE ANGUKO LA MZEE MOBUTU SESESEKO.
pole sana "anko" ila turudishe kwa kamanda F tunakusubiri😆
 
KABALAYE D'JAMENA:
Mlengwa alivyotoka uwanja wa ndege akaenda moja kwa moja katika nyumba ya mwanabalozi mitaa ya Kabalaye.
Swali watakalokua wanajiuliza wasomaji ni kwamba mlengwa kwanini anatafutwa na kwanini alichonacho anatakiwa kunyanganywa?
JENERALI NYAKAMBA.
Alikua na plan kichwani mwake ya kutokurudi Kinshasa na aliamua akishamalizana na target yake aende mjini Gaborone akaanze maisha mapya na familia yake iliyokua nchini afrika kusini.
Na alijua kabisa akishamalizana na kazi aliyotumwa kutokea Nairobi basi wenzake watamgeuka na kumdanganya arudi Gaborite auawe kama muhaini.
Sasa alipanga lazima ampokonye mlengwa mzigo na apoteze ushahidi.
Zaire hakuna maisha tena na waasi walikua wanakaribia mji mkuu wa Kinshasa na amri jeshi mkuu wa nchi alikua yupo mbali na Kinshasa.
N"DJAMENA CHAD:
Mji wa n'djamena upo tofauti sana na mji mingine ya afrika mashariki au mji ya ukanda wa maziwa makuu na ni mji wenye asili ya jangwa,na nyumba zake nyingi ni za matofali makavu ya kuchoma na majumba yenye asili ya ujenzi wa kiarabu.
Na ni mji ambao hauna usalama wa uhakika na ni jambo la kawaida kwa waasi kuvamia ndani ya D'jamena na kufanya uhalifu na kukimbia kurudi jangwani.
Ni mji ambao wakazi wake wengi ni waumini wa dini ya kiislamu hasa madhehebu ya Shia.
Na miziki inayopendwa zaidi ni miziki yenye asili ya kituareg na kiarabu.
Ni mji ambao kifaransa na kiarabu vinatumika sana kuliko hata lugha za asili,na utamaduni wa watu wengi umeathiriwa na tamaduni za kiarabu na kifaransa.
Ukiwa mjini D'jamena ni jambo la kawaida sana kukutana na asikari wa doria wakiwa katikati ya magari ya kijeshi yenye utayari wa kushambulia wakati wowote,maana ni jambo la kawaida kabisa kwa waasi kuingia na kutoka mjini D'jamena.
Kabalaye ndio mitaa wanayokaa watu matajiri na viongozi wa serikali na mabalozi mjini D'jamena.
NA TARGET YA NYAKAMBA ILIKUA MITAA YA KABALAYE D'JAMENA**
Jenerali Nyakamba hakujua kitu kimoja kua ""Target"" ni muuaji wa kutupwa na bingwa wa kuchukua roho za watu wasio na hatia.
Na yupo katika listi wanted za mashirika ya kijasusi mengi sana duniani kama double agent.
Hakujua pia kua""Target"" alikua na habari zake kikamilifu kuhusu yeye na washirika wake wa kijeshi mjini Kinshasa na Brazaville.
Hakujua pia hata huo mzigo aliokua anautaka kutoka kwa ""Target""tayari ulikua mikononi mwa mtu mwingine tayari ukiwa njiani kuelekea nchini Ufaransa na yeye tayari amekwisha kupokea malipo yake,kwa kuufikisha ule mzigo mjini D"Jamena.
Hakuna kitu kilichokua kinamkera Jenerali Nyakamba kama kuona nchi yake pendwa ya Zaire inaangukia mikononi mwa waganda na wanyarwanda na wanyamulenge.
Aliona wazi kabisa wacongomani waliokua jeshini hawana uzalendo
Na huo ndio ulikua mtazamo wake toka waasi walipoanza uasi wao mashariki mwa Zaire mwaka 1996.
KUMBUKUMBU YA JULAI 16
TUKUMBUSHANE KIDOGO WASOMAJI
DAR ES SALAAM TANZANIA.
SIMU TATA: Nyakamba unazo habari.
NYAKAMBA:Sina mkuu nipo Tanzania mwezi mzima sasa ubalozini.
SIMU TATA:Mzee Mobutu ameshamalizana na sisi,,sasa kila mtu afe na chake,nitakupa maelekezo.
NYAKAMBA:Upo Dar es Salaam au Nairobi mkuu??
SIMU TATA:Nakuja Dar es Salaam tutaongea ila jua hakuna gawio tena sababu Mzee Mobutu ameshamalizana na sisi na kuna kazi mbele yako lazima uimalize wewe.
NYAKAMBA:Sawa mkuu utanikuta ubalozini.
Hii simu ndio ilimpa muongozo wa kazi zoote Jenerali Nyakamba au SIMBA WA NYIKA KAMA ANAVYOJIITA.
CHAD 1996 JULY 22
JENERALI NYAKAMBA AKAANZA KAZI RASMI KATIKA MJI WA D'JAMENA ILI KUTIMIZA ALICHOTUMWA.
ITAENDELEA..............!!!!!!!!
 
NIMEPATA RUHUSA KUENDELEA NA UZI.
WAZEE WA KINSHASA WAMENIRUHUSU TUENDELEE,,,,,,,,,!!!!
Hiv, samahan mkuu hiz mambo za kupigwa stop kuandika hiz mambo ni kwel au vibwagizo tu?
Wanajuaje kama unaadnika humu au unaandika pia kwenye platform zingine popular? Wanaokuzuia ni wa kinshasa like u said au wa hum hum nchin? Na je ni kwel wapo humu ndani jukwaan???
 
Hiv, samahan mkuu hiz mambo za kupigwa stop kuandika hiz mambo ni kwel au vibwagizo tu?
Wanajuaje kama unaadnika humu au unaandika pia kwenye platform zingine popular? Wanaokuzuia ni wa kinshasa like u said au wa hum hum nchin? Na je ni kwel wapo humu ndani jukwaan???
Ninaandika katika platform nyingi za nchi tofauti tofauti
na ninatafsiri kwa lugha kuu nne.
Ambazo ni KISWAHILI NA KIFARANSA NA KINGEREZA NA KIARABU.
Lakini kwenye social platform za kiarabu walinipiga ban,s almost kila platform ya waafidhina ninayojiunga kuandika makala.
NB:JF IPO WORLDWIDE NA INA MEMBER ALMOST DUNIA NZIMA
 
Back
Top Bottom