Risasi sio suluhisho (kumbukumbu zangu 1996)

Risasi sio suluhisho (kumbukumbu zangu 1996)

Ninaandika katika platform nyingi za nchi tofauti tofauti
na ninatafsiri kwa lugha kuu nne.
Ambazo ni KISWAHILI NA KIFARANSA NA KINGEREZA NA KIARABU.
Lakini kwenye social platform za kiarabu walinipiga ban,s almost kila platform ya waafidhina ninayojiunga kuandika makala.
NB:JF IPO WORLDWIDE NA INA MEMBER ALMOST DUNIA NZIMA
Hongera
 
Ninaandika katika platform nyingi za nchi tofauti tofauti
na ninatafsiri kwa lugha kuu nne.
Ambazo ni KISWAHILI NA KIFARANSA NA KINGEREZA NA KIARABU.
Lakini kwenye social platform za kiarabu walinipiga ban,s almost kila platform ya waafidhina ninayojiunga kuandika makala.
NB:JF IPO WORLDWIDE NA INA MEMBER ALMOST DUNIA NZIMA
Big up brother and Thanks for your service
 
HEKA HEKA ZA NYAKAMBA
Pale mjini d'jamena kulikua na ubalozi wa Zaire,lakini Nyakamba au Simba wa nyika hakutaka kuomba msaada pale,sababu alikua hataki kujulikana kama yupo mjini D "jamena.
Kitu ambacho hakujua usiku ule ni kwamba*MWINDAJI KAWA MUWINDWAJI YEYE***
Pale nje ya nyumba aliyofikia alikua amewekewa mtego mmoja matata sana,na hakujua pia nyaraka na mzigo aliokua anautafuta tayari ulikua njiani kuelekea nchini Ufaransa.
Lakini kuna ule usemu usemao kua
MWANAJESHI NI MWANAJESHI TU.
Machale yakamcheza utosini.
Nyakamba ni mtu ambae alikua anatumia ushirikina kwa mujibu wa wanaomfahamu kiundani tokea mjini Kinshasa.
Akafungua mlango kwa nia ya kutoka nje ila akasita na kuufunga tena.
Akarudi dirishani kuchungulia nje kupitia floor ya pili ya jengo like alilokua anakaa.
Upande wa kushoto akaona kwenye ile barabara ya kutoka nyumbani pale mpaka barabara kuu kuna gari imepaki ila inawaka indiketa,hiyo ilimaanisha hali ya hatari kichwani mwake.
""""""Namnukuuu Nyakamba""""""""
Duuuh hii sasa ishakua tabu nadhani kuna watu watakua na taarifa zangu kuhusu mimi kuja mjini D'jamena****
Duuh hii sasa imeshakua gundu inabidi niondoke hapa mara moja na nikimbilie ubalozini kupata hifadhi
Ikumbukwe kwamba kipindi hicho Nyakamba alikua anasubiri maelekezo tu ya kujua wapi pa kuanzia ili kuanza kupambana na TARGET na alishangaa mpaka mda huo alikua bado hajaletewa ripoti aliyokua anaisubiria.
Hakujua kua hata mtu aliyetakiwa kumletea ripoti ya TARGET alikua tayari kashatangulizwa peponi na TARGET.
Nyakamba akarudi ndani akachukua silaha zake na kushuka chini ghorofani,akapitia mlango wa chini ya aridhi uliokua umeunganishwa na jiko la ndani na chemba ya maji machafu mtaa wa pili palepale Kabalaye D'jamena akaenda mpaka nje kabisa ya ile nyumba na kutoweka mitaa ile na ndio hiyo ilikua ponea yake kukaa katika nyumba zenye milango ya ziada.
Alitambua kua ile ishara ni haki ya hatari na kama akizembea basi yatamkuta yaliyowakuta wenzake.
Ikumbukwe Nyakamba alikua hatembei na aina yoyote ya mzigo ili kutoacha ushahidi sehemu yoyote ile,na hilo lilikua kanuni yake kubwa sana katika kazi zake za kijasusi.
Alikua anajua kua ni wazi alikua na maadui wengi sana ndani ya Zaire na hata nje ya Zaire.
Na hata BOSI WAKE MUTOMBO""KALULU"" alikua hamwamini pia katika masuala nyeti.Na hasa linapokuja suala la ulinzi wake binafsi.
Na alihisi pia kua""KALULU"" alikua anawazunguka yeye na TARGET ili wauane na afaidike yeye mwenyewe japokua hakua na ushahidi dhabiti
KINSHASA ZAIRE.
Hali ya kisiasa mjini Kinshasa ilikua ya Kichekesho sababu kulikua na maasi ndani ya jeshi ,hasa baada ya mji wa Kisangani kuangukia mikononi mwa waasi wa Kinyarwanda na Banyamulenge maarufu kama KADOGOO.
Waasi walikua wanaua watu hovyo na kuiba maduka na kukaba na kubaka na kufanya mauaji ya kikabila.
Mzee Desire Kabila hapa ndipo alipoanza kukosana na wanyarwanda waliokua wanaongozwa na JAMES KABAREBE baada ya kuwakataza wasiwe wanaua na kubaka na kupora raia wa Kikongo.
Mjini Kinshasa makamanda wa vitengo vyote vya kijeshi walianza kulaumiana na kutafuta nani mchawi mpaka vikosi vyao mjini Kisangani vimeshindwa na waasi wa Kinyamulenge.
KONGOLO""SADDAM HUSSEIN""KINSHASA:
Alikua mkuu wa vikosi vya kumlinda raisi na alipoiona hiyo hali ya kushindwa akaanza kupambana na watu aliowaita wasaliti ndani ya jeshi.
Kwanza akamuua mnadhimu mkuu wa jeshi la Zaire.
Akamuua mlinzi mkuu binafsi wa raisi.
Akamuua daktari wa raisi
Akaua baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani.
Na akawafuta jeshini,zaidi ya wanajeshi 3000 na kuua wanajeshi 407 kati yao akiwaita wahaini au wasaliti wa serikali.
MUTOMBO""KALULU"" KINSHASA ZAIRE
Huyu alikua ndie mweka hazina mkuu wa serikali ya Zaire upande wa jeshi.
Na alihusika na manunuzi yote na matumizi yote ya jeshi la taifa,kama muhasibu mkuu pia wa serikali.
Na ni mtu aliyekua na mawasiliano mazuri na TARGET na hata ule mzigo uliosafirishwa kwenda nchini ufaransa ulikua unamuhusu yeye moja kwa moja na washirika wake wa iliyokua serikali ya Rwanda ambayo ilipinduliwa madarakani 1994.
BAADAE TUTAMZUNGUMZIA MUTOMBO"""KALULU"""
""""""""""KINSHASA""""""""1997
Mji ulikua umepwaya na vita vilikua vimeharibu hali ya maisha ya kawaida mjini Kinshasa.
Japokua watu walikua wanajitahidi kuendelea na maisha yao kama kawaida ila hali ya maisha haikuweza kurudi kua kama mwanzo.
Raia wengi kutoka majimbo ya mashariki mwa Zaire walikua wamerundikana mjini Kinshasa kutafuta hifadhi kama wakimbizi wa ndani ya nchi wasiokua na makazi.
Ikulu ya raisi ilikua imegeuzwa kua kambi ya kijeshi na Mzee Mobotu alikimbia mji kwa haraka sana kuelekea nyumbani kwake GABORITE,huku boti zote za kuvukia upande wa pili wa mto kongo,kwenda jijini Brazzaville zilikua zimechukuliwa na wanajeshi,,chini ya
MBABE KONGOLO""SADAM HUSEIN"".
ITAENDELEA...............!!!!!!!!
Screenshot_20231116-164755_1.jpg
Screenshot_20231116-165042.png
Screenshot_20231116-164943.png
 
Back
Top Bottom