INAENDELEA.........!!!
MUTOMBO""KALULU""KINSHASA 1997
:General Mutombo alikua katika wakati mgumu sana kuamua mambo mawili nayo ni
1:Kumwadabisha Kongolo
2:Kuchukua madaraka kwa niaba ya Mzee.
Lakini mwisho wa siku aliachana na maamuzi yote mawili na kuamua kuelekeza nguvu zake katika kukamilisha mpapango wake na TARGET ili kujihakikishia maisha yake ya baadae nje ya Zaire.
Hata taarifa zote za Nyakamba kuufuatilia mzigo wa TARGET mjini Djamena alikua nazo na aliratibu mpango wote kwa ukamilifu zaidi kuhakikisha kua washirika wote wa mpango ule akiwemo Nyakamba na TARGET wanaondolewa duniani baada ya mpango kazi kukamilika na maisha mengine yaendelee nje ya siasa,,sababu alikubali ukweli kua Zaire hana chake tena.
DJAMENA CHAD 1997:
Nyakamba alianza kupata wasiwasi baada ya kuona kua katika rada zake ghafla TARGET amepotea na haonekani na alipenyezewa habari kua hata mzigo unaolengwa uliopo mikononi mwa TARGET kuna uwezekano wa asilimia 40% tayari umeshawasili nchini ufaransa.
Na vile vile alipata taarifa kua nchini Zaire waasi walikua tayari wapo nje ya mji wa Kinshasa na tayari walikua wameshapinduliwa na wanyarwanda na waganda na wanyamulenge.
Ili kujihakikishia usahihi wa taarifa hizi ilibidi Nyakamba aingie kazini haraka iwezekanavyo ili kujua mbichi na mbivu.
KISANGANI 1997:
Mjini kisangani hali ilikua tete miongoni mwa vikundi vya waasi na vikosi vya wanajeshi wa Uganda na Rwanda.
Kulikua na malalamiko katika komandi kuu ya kamati ya mapambano ya waasi.
Malalamiko yaliwahusu waasi wa kitusi na kinyarwanda ambao walikua wanatuhumiwa wao wanyaruanda na waganda wanataka kuhodhi madaraka yoote na maamuzi yoote katika harakati za uasi na kuwanyima fursa wazawa wazaire.
Kukatokea mkaganyiko mkubwa wa kikabila na kikanda na habari zilipomfikia MUTOMBO""KALULU""aliona hiyo ni fursa kwa siku zijazo kwake kisiasa.
Mjini kisangani baada ya waasi wa banyamulenge kuvifurumisha vikosi vya serikali ya Zaire,,,,waasi walianza kuiba na kupora mali za raia na kuanza kuwaua wakimbizi wa kinyarwanda wenye asili ya kihutu.
Jambo hilo halikumpendeza kiongozi wa vikundi vya waasi ambae alikua mzaire.Hapa namzungumzia ""MZEE WA KONYAGI"""au kwa jina la utani MZEE UPARA au alijulikana vile vile kama MSWAHILI.....na alipoanza kuwakemea makamanda wa banyamulenge kuhusu hali hiyo,,,,bas wale makamanda wakaanza kumuhujumu katika mstari wa mbele wa mapambano.
Na taarifa zilimfikia MUTOMBO a.k.a KALULU na aliiona hii kama fursa pia ya siku za usoni.
IKUMBUKWE:
Mutombo alikua ameshaamua kuitelekeza kinshasa na alikua yupo mjini Gaborite na mzee JOSEPH....na wote walikua na mipango ya kuitelekeza Zaire ,,kila mtu ashike njia yake kivyake.
Kilichokua kinawapeleka baadhi ya majenerali na makamanda wa jeshi la Zaire mjini Gaborite,,,ilikua ni kuchukua baraka za kiimla na kiuchumi kutoka kwa mzee JOSEPH.
Pia walipewa access za bank accounts zilizosambaa everywhere worldwide.
Na ilikua lazima kila mtu afe na chake mapema kabla hawajastukiwa.
Sasa turudi KISANGANI 1997.
Hali ilikua tete sana na hata nidhamu ya vikosi vya waasi wa kinyamulenge ilikua ya kutia shaka.Na ilionekana wazi kua kampeni ya kuingia Kinshasa ikiisha basi hawa watu wataanza kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu za ukabila na uroho wa vitalu vya uchimbaji wa madini ya almasi na dhahabu na shaba kule kivu kaskazini na kivu kusini.
DJAMENA CHAD 1997:
Nyakamba alikua anahisi kuchanganyikiwa sasa,,maana pamoja na ujasusi wake wa kutosha lakini alishindwa kuelewa kwanini TARGET haonekani mjini Djamena na hata vyanzo vyake vya kumletea habari mjini humo,,vilikua vinauawa kimoja baada ya kingine takribani watu tisa.
Hii ilimchanganya sana Nyakamba na taa nyekundu ikaanza kuwaka kichwani mwake kua pale mjini Djamena sio salama kabisa kwake kwa yeye kuendelea kukaa na kushangaa shangaa.
Labda akimbilie ubalozini au aondoke Chad na akubali kua misheni imefeli.
DAR ES SALAAM TANZANIA 1997:
Ikumbukwe kua Nyakamba alikua anakaa maeneo ya kurasini mjini Dar es salaam na connection zake zilitoka moja kwa moja ubalozi wa Zaire mjini Dar es salaam na ikumbukwe pia aliyemuagiza Nyakamba atimize hili suala mjini Djamena ni mtu aliyekuepo mjini Dar es salaam aitwae SIMU TATA.
TUMJADILI SIMU TATA""LESAPEE"".
SIMU TATA""LESAPEE""hakujulikana katika ubalozi wa Zaire mjini Dar es salaam alikua na wadhifa gani.
Mara alikua kama dereva na mara nyingine alikua kama afisa habari wa ubalozi....
Ila mara nyingi alionekana katika kumbi za muziki wa dansi wa bendi nyingi za kizaire mjini Dar es salaaam.
Na haikujilikana dhamira yake ni nini
Lakini watu wa udaku walimng'amua kama mpelekezi wa serikali ya Zaire dhidi ya wapizani wao walioko nje ya Zaire****
SIMU TATA"""LESAPEE"" alikua ni mtu wa viwalo vya kufa mtu na ndio maana akabatizwa jina la LESAPEE.
Huyu alikua ndio injini ya MUTOMBO""KALULU""katika kupangilia mambo yake na ndie aliyempangia majukumu NYAKAMBA wakiwa kule Nairobi na kumwambia nini cha kufanya kule Chad na kwa wakati huo huo alikua na mawasiliano na TARGET mjini Djamena.
Mwisho wa makala ndugu msomaji utaelewa kwanini huyu kijana aliitwa SIMU TATA"""LESAPEE""
DJAMENA CHAD 1997:
Nyakamba alianza kuingiwa na ubaridi kuhusu hali halisi ya mpango ule na utayari wa wahusika wenzake katika kuukamilisha.Kama TARGET haonekani na baadhi ya watoa taarufa wake wameuawa kinyemela....basi anayefuatia atakua yeye.
Na kama kweli"""TARGET"""ameshavusha mzigo mpaka nchini ufaransa,basi hakuna sababu ya kuendelea kukaa nchini Chad na ile mali tayari ameshaikosa.
Vp arudi Tanzania au aende Ubeligiji akakae ukimbizini.Maisha ya ukimbizini hayana thamani kwa jenerali kama yeye.
Na pili kwanini aikimbie Zaire kuwakwepa wanyamulenge,,wakati yeye anayo support kubwa katika majimbo ya Katanga na Tanganyika na Kivu Kaskazini na Kivu kusini.
Wanajeshi hawakimbii bali wanapambana mpaka tone la mwisho.
Mzee JOSEPH aliwatendea meama mengi sasa ni zamu ya yeye kulipa fadhila kwa vizazi vya mzee JOSEPH na washirika wake.Na pia sio busara kuachia machimbo ya dhahabu mikononi mwa wanyarwanda na wagaganda.Nyakamba aliwaza mengi sana kabla ya kuchukua maamuzi sahii kwa upande wake.
Alijiapiza kua*Akijua kua TARGET ameshapeleka mzigo Ufaransa basi na yeye ataachana na mpango huu na kurudi Zaire kuanzisha vuguvugu la kisiasa na kijeshi****
Kwahiyo alijipa mda mfupi tu wa kuwepo mjini Djamena na ilikua ama zake au ama za TARGET.
Na alihisi kabisa kua MUTOMBO""KALULU""atakua kamzunguka kwa namna flani.
KINSHASA ZAIRE 1997:
KONGOLO""SADAMU HUSSEIN"""alikua na wakati mgumu sana katika jeshi,,,maana washirika wake wote muhimu alikua either amewaua au wameuawa au wamemkimbia na kumtelekeza kwa namna moja au nyingine.
Alikua amebakia na vikosi vya askari 600 ambao wakikua ni makomando wa kumlinda mzee JOSEPH na kwa uhalisia wa uwanja wa vita waasi walikua tayari wameshaingia mjini Kinshasa.
KONGOLO aliona isiwe tabu yanini afe vitani bas akapanda boti za mwendokasi na kuvukia upande wa pili wa mto Kongo kutokea upande wa Kinshasa Zaire mpaka upande wa Brazzaville Congo.
Kwa mara ya kwanza mji mkuu wa Zaire ulikua chini ya waasi wa Banyamulenge ambao waliudhibiti.
Taarifa za waasi kuudhibiti mji wa kinshasa zilimuumiza sana MUTOMBO akiwa mjini Gaborite na Mzee JOSEPH na aliona huu ndio wakati muafuaka wa kucheza karata zake za kisiasa kwa manufaa yake mwenyewe akiwa na marafiki zake wa kihutu.
NA ALIPOJIHAKIKISHIA KUA TARGET AMESHAFIKISHA MZIGO PARIS ILA HAONEKANI NA AMEONDOKA DJAMENA KWA KIFICHO BILA KUONEKANA NA NYAKAMBA NA WATOA HABARI WAKE NA AKIWA TAYARI AMESHAUA TISA KATI YAO.BASI ALIAMURU KWA KIKOSI KAZI KUA NYAKAMBA AUAWE MJINI DJAMENA NA ALIAMURU SIMU TATA NAE AUAWE MJINI NAIROBI MAANA TAYARI WALIKUA WAMESHAINGIA KWENYE MITEGO YAKE YEYE MUTOMBO***.
ITAENDELEA.................!!!!!!!!!!!!!!