JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Boris Johnson ajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta Waziri Mkuu mpya
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson Jumapili alijiondoa katika kinyang'anyiro cha kumrithi Liz Truss kama kiongozi wa nchi hiyo inayoendelea kukabiliwa na misukosuko ya kisisasa.
Johnson alisema wabunge wachache walikuwa wanamuunga mkono, ikilinganishwa na wale wanaomuunga mkono Waziri wa Fedha wa zamani Rishi Sunak, katika juhudi za kuwania wadhifa huo.
Hata hivyo, Johnson alisema kwama awali, alikuwa katika nafasi nzuri ya kufaulu katika uchaguzi na wanachama wa Chama cha Conservative, kabla ya Sunak kuonekana kuwa na ufuasi mkubwa zaidi.
Mwanasiasa huyo, ambaye hakuwahi kutangaza rasmi azma yake ya kurejea Downing Street, alitumia wikendi nzima kujaribu kuwashawishi wabunge wa Conservative kumuunga mkono na akasema Jumapili kwamba alikuwa na uungwaji mkono wa 102 kati yao.
Alihitaji kuungwa mkono na wabunge 100 kufikia Jumatatu ili kuendelea hadi hatua inayofuata, ambayo ingempelekea kupambana na Sunak.
Sunak, ambaye kujiuzulu kwake kama waziri wa fedha mwezi Julai kulichangia kuondoka kwa Johnson, alikuwa ameondoa kizingiti cha wabunge 100 waliohitajika kuendelea hadi hatua inayofuata.
Iwapo Sunak atakuwa Waziri Mkuu, atamridhi Truss aliyejiuzulu wiki jana baada ya kukabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa.
===
Rishi Sunak could be named as the new Prime Minister later today after Boris Johnson bowed out of the Tory leadership race - as Penny Mordaunt insists she will 'fight on' despite appearing to be significantly short of the 100 supporters she needs to remain in contention ahead of the 2pm deadline.
The former Chancellor, who officially launched his campaign yesterday morning, has received the public backing of more than 150 Tory MPs - with more joining team Sunak following Mr Johnson's departure from the race.
As of last night, 155 MPs had said they are backing Mr Sunak, while just 25 had spoken out in support of Ms Mordaunt. But a further 54 who were hoping Mr Johnson would return to the premiership are yet to publicly reveal to whom they have switched allegiance.
Source: DailyMail