DOKEZO RITA changamoto ni nini? Angalieni jinsi ya kuboresha tovuti yenu kutujali sisi wateja wenu!

DOKEZO RITA changamoto ni nini? Angalieni jinsi ya kuboresha tovuti yenu kutujali sisi wateja wenu!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

MXMXMXMX

New Member
Joined
Dec 30, 2019
Posts
2
Reaction score
15
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) nawapongeza mmeanzisha mfumo mzuri wa wananchi kufuatilia taratibu za kupata cheti cha kizazi na vifo katika mtandao badala ya kuja kupanga foleni kwenye ofisi zenu.

Ila bado kuna changamoto nadhani kwakua watumishi sasa hawakutani na wateja nadhani wanafanya kazi kwa kubweteka au kutokujali wateja.

Changamoto iliyonikuta mimi, sasa ni mwezi toka nifanye maombi ya cheti cha mtoto wangu kupitia mtandao wa erita.rita.go.tz na kwa maelezeo yaliyopo kwenye mtandao ni kuwa taratibu zote zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku 10 toka nifanye maombi hadi kupata cheti.

Mmeweka sehemu ya kuweka viambatanisho na mmesema viambatanisho si chini ya vitatu chochote kati ya mlivyoviorodhesha kwenye mtandao, cha kushangaza kila siku narudishiwa ujumbe kuwa weka kiambatanisho fulani, nikiweka naletewa niweke kiambatanisho kingine nikiweka naambiwa tena niweke tena kuambatanisho nilichokwisha weka nafanya yote lakini bado mnanirudia niweke viambatanisho ambavyo nimekwishaweka au kingine kipya na kunipotezea muda mpaka imefika mwezi sasa.

Kwanini msiorodheshe viambatanisho vya muhimu tu kwenye orodha yenu na sio kuweka vingi na kumbe hamvihitaji au kumwambia mtu aweke si chini ya vitatu(achague vyovyote vitatu kati ya mlivoviweka) halafu badae kumwambia tena aweke kiambata flani na kuzidi kupoteza siku za kushughulikia huduma yake anayohitaji. Ni uzembe au.

Na nilifika hadi ofisi za rita nikaambiwa majibu nitapewa kwenye mtandao na mbaya zaidi hata namba za simu zote za ofisi hazipatikani. Hii si sawa.
 
Kila kinachosimamiwa na CCM n majangaa ,
IMG-20250217-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom