KERO RITA Lindi Mjini wamekosea majina yangu sahihi wakati wa marekebisho mara mbili mfululizo, inanigharimu zaidi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Huko hamuombi kupitia mtandao,hata kama manual kama attachment ya marekebisho mkirejea na ikaonyesha kosa lilikuwa kwao huwa hualipi tena. Utalipaje marekebisho wakati aliyekosea ni afisa wao?
 
Watanzania wengi hatuna umakini kwenye mambo ya msingi.
Mpaka Ubalozi tena nje kwa wazungu walikosea pasi ya mwanangu
Kabla sijaondoka nikasema hebu nijiridhishe niisome kwa umakini
Lahaula jina tofauti hebu fikiria
Hata kwenye vyeti vya ndoa bongo wanakosea sana tena unamwambia nakili majina ila anakosea hopeless kabisa
Tena kila sehemu ni hivyo akili zetu zinatutosha kwa mambo machache sana
 
Ni huzuni kwakweli.
 
wazi sasa ni kwamba umakini unakuwa mdogo kwa wengi wa watumishi wetu tumebakiwa na tabia za wakoloni za kusahau nafasi zetu ni kwa ajili ya wale tunaowatumikia. wengi tunafanya kazi siku ipite tulipwe na ndio maana tunafeli kutoa huduma sahihi...
 
Huko hamuombi kupitia mtandao,hata kama manual kama attachment ya marekebisho mkirejea na ikaonyesha kosa lilikuwa kwao huwa hualipi tena. Utalipaje marekebisho wakati aliyekosea ni afisa wao?
ukinadi hivi wao wananadi yao. Ukizingatia wewe ndi mwenye umuhimu wa kitu chako unabaki huna namna kwa kuwa hutaki kucheleweshwa.
 
wazi sasa ni kwamba umakini unakuwa mdogo kwa wengi wa watumishi wetu tumebakiwa na tabia za wakoloni za kusahau nafasi zetu ni kwa ajili ya wale tunaowatumikia. wengi tunafanya kazi siku ipite tulipwe na ndio maana tunafeli kutoa huduma sahihi...
Sahihi, utakuta Uzembe wa Afisa wa Tasisi halafu anataka kumbebesha Mzigo Mwananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…