Wakazi wanaoishi karibu na River Kibos, Kisumu, wanataka mamlaka kutoa majibu kuhusu madai mapya ya uchafuzi wa mto huo, huku wakitaka shughuli za Kibos Sugar and Allied Industries zichunguzwe na sheria za mazingira zitekelezwe.
Lakini ukifuatilia rekodi, swali linakuwa kubwa zaidi: Kwa nini River Kibos bado inatajwa katika malalamiko ya uchafuzi miaka kadhaa baada ya serikali na mahakama kuingilia kati?
Mwaka 2017, National Environmental Complaints Committee ilifanya ukaguzi katika viwanda vya Kibos na kubaini uwepo wa vinasse, mabaki ya shughuli za distillery, na kuagiza kampuni kuacha kuitumia katika barabara huku ikipendekeza ufuatiliaji zaidi.
Mwaka uliofuata, ripoti ya Serikali ya Kaunti ya Kisumu ilieleza maji ya River Kibos kuwa meusi na yenye harufu, huku samaki wakiripotiwa kuelea majini. Ripoti hiyo ilihusisha vinasse iliyopatikana mtoni na shughuli za Kibos Distillers.
Hata katika ESIA iliyowekwa kwenye tovuti ya NEMA mwaka 2019 kuhusu kiwanda cha bio-fertilizer, taka za viwanda vya Kibos, ikiwemo vinasse, fly ash na boiler ash, zilielezwa kuwa zimekuwa changamoto kubwa ya uchafuzi wa maji, hewa na ardhi.
Baadaye, ukaguzi wa NEMA wa 2019 ulisema kampuni ilikuwa imetekeleza kati ya asilimia 95 na 100 ya hatua za kurekebisha mazingira, na kupendekeza ukaguzi wa kila robo mwaka ili kuzuia tatizo kujirudia.
Mwaka 2020, Court of Appeal ilibatilisha amri ya kufunga viwanda lakini ikaagiza NEMA na NECC kuendelea kufanya ukaguzi, huku kampuni ikitakiwa kufanya environmental audit kila mwaka.
Kibos Sugar kwa upande wake inasema hufanya vipimo vya maji upstream na downstream na kwamba matokeo yake yanaonyesha inafuata viwango vya NEMA.
Sasa wananchi wanapolalamika tena, jibu halipaswi kuwa maneno pekee.
NEMA iko tayari kuweka hadharani matokeo ya hivi karibuni ya vipimo vya River Kibos? Audits za kila mwaka zinasema nini? Na ukaguzi ulioamriwa na mahakama umekuwa ukifanywa mara ngapi?
Kwa sababu baada ya miaka ya malalamiko, closure notices, kesi na ahadi za compliance, swali sasa si tu “nani anachafua River Kibos?”
Swali ni: Mfumo uliowekwa kuilinda umekuwa ukifanya kazi kweli?