Fortunatus Buyobe
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 463
- 1,127
ILIPOISHIA
“Hongereni kwa hilo”
“Usitupongeze, hata wewe unatakiwa kujipongeza kwa maana kwa sasa familia yetu inakwenda kuwa na furaha, kama pale awali, ngoja ni mpigie Zari nimuambie aje hapa hospitalini”
“No usimpigie”
“Kwa nini?”
Gafla mlango ukafunguliwa kwa nguvu, akaingia Hussein akiwa ameshika tumbo lake huku anavuja damu tumboni na mdomoni, sote tukajikuta tukistuka sana.
“Wamemchuku…..a mto…..to”
Hussein baada ya kuzungumza maneno hayo, akaanguka chini mzima mzima, jambo lililo zidi kutuchanganya mimi na mama hata simu aliyo ishika mkononi mwake ikaanguka chini kitokanana mwili wake kumtetemeka sana.
ENDELA
Kwa haraka nikachomoa sindano ya dripu niliyo chomwa mkononi mwangu, nikashuka kitandani huku ninapepesuka kwani maumivu ya mshono bado yananiuma japo si sana. Nikamgeuza Hussein na kumuangalia sehemu ya jeraha lake, nikaona jinsi lilivyo kubwa.
“Dokta Dokta”
Nilita kwa nguvu ila sikuapata muitikio wa mtu yoyote, nikatoka kwa haraka kwenye chumba hichi nakumuacha mama akiwa katika hali ya bumbuazi na mshangao.
“Nesi nesi”
Nilimuiota nesi mmoja aliye toka kwenye chumba cha pili.
“Vipi kaka yangu”
“Kuna mgonjwa nakomba msaada wako wa haraka”
Nesi kwa haraka akaanza kunifwata kwa nyuma, tukaingia ndani ya chumba hichi, nikajikuta nikizidi kuchanganyikiwa baada ya kumkuta mama akiwa amenguka chini na kupoteza fahamu. Kwa haraka nikaokota simu yake na kuanza kuingia upande wa majina. Nikaatafuta jina la baba kwa haraka nikalipata na kuipiga namba yake ya simu.
“Sekretari wa bwana Alemida, tafahdali ninaweza kukusaidia”
Nilisikia sauti ya kike, nikatamani kuzungumza jambo ila nikakata simu. Nikamtazama nesi jinsi anavyo zungumza na simu ndogo ya upepo aliyo ishika mkononi mwake akiomba msaada zaidi wa madaktari.
“Nesi waangalie”
Kwa haraka nikatoka katika chumba hichi huku nikikimbia kwa kasi kuelekea nje, nikatazama kwenye maegesho ya magari katika kila eneo sikuona dalili ya kumuona mwanagu Brian.
“Kaka unatakiwa kurudi ndani”
Nesi mmoja aliniambia baada ya kuniona nikiwa ninashangaa shangaa, kitu ambacho limemfanya nesi huyu kuweza kunitambua kwa haraka kwamba mimi ni mgonjwa, ni haya mavazi niliyo yavaa.
“Kuna mtoto mdogo wa kiume hivi mweupe mweupe umemuoana”
“Kaka yangu watoto ni wengi katika hii hospitali kwani kuna kitu kilicho tokea?”
“Nimamuomba mkuu wa hospitali”
“Mkuu kwa sasa yupo kwenye kikao”
“Nimekuambia ninamuomba mkuu wa hospitali”
Nilizungumza kwa kufoka hadi watu wanao pita pembeni yetu wakatushangaa, nesi akanitazama usoni kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kuongoza kuelekea eneo linalo fanyika kikao hicho. Nikiwa njiani simu ya mama ikaita, kwa haraka nikaipokea.
“Haloo”
Nikaisikia sauti ya baba akizungumza, nikaka kimya kwa muda huku nikimtazama nesi usoni mwake, kwa ishara nikamuomba tuendelee kutembea kuelekea kwenye ofisi yenye kikao.
“Kuna tatizo”
Nilizugumza kwa sauti nzito.
“Nani wewe unaye shika simu ya mke wangu”
“Baba Brian ametekwa na mama amezimia yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi”
Nilijikuta nikizungumza kwa sauti yangu halisi, nesi akasimama na kunitazama baada ya kuyasikia maneno hayo.
“Erick!!”
“Ndio baba ni mimi”
“I…i..ime…ime kuwaje hadi upo hai?”
“Baba huu sio muda wa kuelezana maswali, ninacho kuambia ni kwamba mwanangu ametekwa na watu wasio julikana, kijana wagu mmoja amepigwa risasi, ninankuomba kwa kutumia cheo chako cha sasa, ripoti hili swala polisi haraka iwezekanavyo”
“Sawa sema upo wapi sasa hivi nije?”
“Nipo hospitali ya Muhimbili”
“Ninakuja”
Baba akakata simu, tukaendelea kuongozana na huyu nesi kwa haraka kuelekea kwenye hiyo ofisi.
“Umesema kwamba kuna mtoto ametekwa?”
“Ndio”
“Imekuwaje kuwaje?”
“Ningejua ningekuuliza?”
Nesi ikambidi kukaa kimya tu kwa maana hata jibu nililo litoa ni jubu lililo jaa hasira kali. Tukafika kwenye jengo ambalo ndio kuna kikao cha madaktari, nikaingia na nesi huyu na kuwafanya watu wote walimo ndani ya hii ofisi kututazama. Nikamfwata daktari mkuu mbele alipo simama kwenye kipaza sauti.
“Erick kuna tatizo gani?”
Mzee aliniuliza kwa sauti ya chini huku akizima kipaza sauti kilichopo mbele yake.
“Kuna utekaji wa mwanangu umetokea hapa hospitalini kwako, mtu wangu mmoja amepigwa risasi, mama yangumzazi amepoteza fahamu, kwahiyo ninakuomba msaada wako tafahali”
Mzee akaonekana kushangaa sana kwa taarifa hizi, akawasha kipaza sauiti chake.
“Jamani madaktari sahamani kwa usumbuku, kuna dharura imejitokea na ni yalazima. Kikao chetu kitaendelea badae, tutawanyikeni”
Daktari mkuu akazima kipaza sauti chake na tukaanza kuongozana na kuelekea mlangoni.
“Erick, Erick”
Nilisikia sauti ya kike nyuma yangu, nikageuka kwa haraka huku jasho likinimwagika, nikakutana na Jackline mwanafunzi mwenzangu niliye kuwa naye katika chuo cha udaktari.
“Ni wewe”
Jackline alizungumza huku akitabasamu akanipatia mkono, nikautazama kwa sekunde pasipo kuzungumza neno lolote.
“Dokta Jackline, ninakuomba utulie utazungumza na Erick badae kama munafahamiana kwa sasa kuna jambo tunatakiwa kulishuhulikia, sawa dokta”
“Nimekuelewa mkuu”
“Erick tuondoke”
Daktari mkuu akanishika mkono wangu wa kulie, nikamtazama Jackline kwa macho makali, kisha nikageuka na kuendelea na safari ya kuondoka na dokta na daktari mkuu ninaye muheshimu kama baba yangu.
“Erick ilitokeaje tokeaje”
“Doka siwezi kuelewa kwa maana kila jambo limetokea kwa muda mfupi sana”
Daktari mkuu akatoa simu yake mfukoni, akaminya minya batani zake na kuiweka sikioni.
“Ninaomba mumeweze kuangalia kamera zaote za ulinzi hapa hospitalini, kuna mtoto ametekwa”
“Nipo njiani nina kuja sasa hivi”
Daktari mkuu akata simu yake na kuirudisha mfukoni, tukaelekea katika chumba kinacho tumiwa kwa uangalizi wa kamera zote za ulinzi.
“Erick tukio lilitokea kwa dakika ngapi kutoka hivi sasa?”
“Kama dakika kumi hivi”
“Hembu angalia dakika kumi na tano nyuma, jengo la ICU si ndio?”
“Ndio dokta”
Injinia anaye ongoza Tv nyingi zilizomo humu ndani ya chumba akisaidia na wezake wanne, akaanza kurudisha matukioya nyuma yaliyo rekodiwa na kamera zilizo zagaa kwenye hii hospitali. Kamera ikamuonyesha mama jinsi alivyo kuja na walinzi wake wawili pamoja na Brian akawaomba walinzi wake kubaki nje ya mlango. Walinzi hao baada ya mama kuingia ndani wakaondoka katika eneo la mlango na Hussein akatoka, hazikupita hada dakika nyingi Hussein akaingia na akatoka na mtoto.
“Ehee sasa fwatilia Hussein alielekea wapi?”
Tukaendelea kumuona Hussein jinsi alivyo mbeba Brian na kutoka naye nje huku akizungumza naye, mlinzi mmoja wa mama akamfwata Hussein, akazungumza naye maneno mawili matatu ambayo hatuyasikii, Hussein akamkabidhi mtoto mlinzi huyu wa mama, mlinzi huyo akatoa bastola yake ya kwa siri na kumpiga Hussein tumboni na kumfanya Hussein aanguke chini.
“Ehee alimpeleka wapi?”
Tukio likahamia kwenye kamera nyingine ambapo mlinzi huyo akaingia kwenye gari aina ya Range rover nyeusi, ambayo nilivyo tazama namba zake kwa haraka niliweza kufahamu kwamba ni gari la Rose.
“Malaya huyuuuu”
Nilizungumza kwa hasira huku niking’ata meno yangu kwa jazba.
“Unamjua aliye mchukua mwanao?”
“Ndio ni Rose”
“Rose?”
“Mwanamke niliye kuambia kwamba ninampenda na nilihitaji kumrudisha kwenye maisha yagu”
“Jesus Christ. Unatakiwa kutoa taarifa polisi”
“Sihitaji polisi waweze kujua hili kwa maana mwanagu atakuwa katika hali mbaya”
“Erick huwezi kulifanya hili jambo peke yako mwangu”
“Baba niamini mimi, ninacho kihitaji kwa sasa. Ninaomba unichome sindano ya kuzuia maumivu kwa muda mrefu”
“Erick hiyo ni hatari kwa afya yako hususani kwa dozi unayo itumia”
“Ninakuomba ufanya hivyo dokta, maisha yangu hayana umuhimu sana kama mwanangu, ambaye kwa sasa ndio kila kitu. Sinto hitaji mtu yoyote aweze kunaynyua mkono wake juu ya mwanangu”
Daktari mkuu akaka kimya huku akinitazama machoni mwangu.
“Please ninakuomba ufanye hivyo”
“Sawa”
Tukatoka na daktari mkuu katika hichi chumba, tukaelekea hadi kwenye ofisi yake, akachukua kichupa kidogo ambacho kwa haraka sikukisoma jina kutokana na mawazo mengi yaliyo nitawala. Akanifunga mpira unao vutika kwenye msuli wa mkono wangu wa kishoto na kuifanya mishipa yangu kuonekana vizuri. Akaifunga sindano kwenye bomba la sindano hiyo kisha akavuta dawa kwenye kichupa hicho kwa kutumia bomba la sindano hadi likafika nusu.
“Erick ila hichi ninacho kifanya sio vizuri”
“Baba ninamini kwamba unanipenda, ila yule pia ni mjukuu wako ambaye alipaswa leo acheze mbele yako ila kuna huyu mjinga kwa sasa anaingia kwenye kumi na nane zangu, sasa muache nimuonyeshe kwamba mimi sio mtu mzuri”
“Sawa”
Daktari mkuu akanichoma sindano kwenye mdiba wangu ulipo kwenye kikonjio cha mkono, akasukuma dawa hii taratibu hadi ikaisha, akachoma sindano na kunipatia pamba. Simu ikaanza kuita mfukoni mwangu, nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Ndio baba”
“Upo wapi?”
“Nipo katika chumba cha daktari mkuu”
“Ninakuja”
Nikakata simu na kuirudisha mfukoni.
“Ni nani huyo?”
“Ni baba yako”
“Ahaa sawa sawa”
Hazikupita hata dakika mbili mlango ukagongwa kwa nje, dokta akamruhusu mtu anaye ingia. Mlano ukafunguliwa na mlimzi aliye valia suti nyesui, baba akaingia ndani na mlinzi huyo akabaki nje.
“Muheshimiwa mgombea uraisi”
“Habari yako dokta Benjamini”
“Salama tu, naona umestukiza kufika hospitalini kwangu”
“Nikuja kumuona kijana wangu huyu hapa”
Baba alizungumza huku akinishika shika begani mwangu.
“Erick kumbe baba yako ni muheshimiwa Almeida?”
“Ndio dokta”
“Ohoo siamini jamani”
Daktari mkuu akaonekana kufuhi sana na kushangaa sana.
“Mama yako yupo wapi?”
“Nilimuacha katika chumba nilicho kuwa nimelazwa”
“Twende”
Tukatoka wote watatu, nje nikakutana na walinzi sita walio valia suti nyeusi, wakatuweka kati na tukaendelea kutembea kuelekea kwenye chumba nilicho kuwa nimelazwa. Kila sehemu tunayo pita watu wengi walibaki wakishangaa huku wengine wakimshangilia baba na kujisahau kabisa kwamba wapo hospitalini. Tukaingia kwenye chumba nilichokuwa nimelazwa, nikawakuta manesi wawili na daktari mmoja wakimshuhulikia mama ambaye hadi sasa hivi hajazinduka. Sikumuona Hussein zaidi ya damu zilizo mwagika chini.
“Hussein yupo wapi?”
Nilimuuliza nesi mmoja huku nikimazia macho
“Amekimbizwa katika chumba cha oparesheni”
“Hali yake inaendeleaje?”
“Sio nzuri sana, ila madaktari watajitahidi kutoa risasi yake”
“Risasi!!?”
Baba aliuliza kwa msangao huku akinitazama usoni mwangu
“Ndio mmoja wa walinzi wa mama amempiga risasi mtu wangu wa karibu, tena akamuiba mtoto na kuondoka naye”
“Nimetoa ripotii polisi tayari wataanza kufanya msako”
“Msako gani huo ikiwa wanacho kitafuta hawakijui”
“Niliwaambia wamtuafute mjukuu wangu amekamatwa”
“Baba ikiwa watu wako tu ndani ya utawala wako upande wa ulinzi ni wasaliti, hao polisi kuna asilimia gani ya kuweza kuwaamini kama wanaweza kufanikisha swala la mawanangu kutekwa”
Niliuliza kwa sauti ya ukali huku nikimtazama baba usoni mwake. Taratibu daktari mkuu, akasimama karibu yetu na kunishika mkuno.
“Erick ninakuomba utulie, mgonjwa anagitaji kutulia la sivyo kelele zinaweza kumpelekea kifo mama”
Baba akang’ata meno yake kwa hasira huku akinitazama kwa macho yaliyo jaa hasira, kisha akafungua mlango na kutoka nje, akaubamiza kwa nguvu hadi mama akastuka na kujikuta akikaa kitako.
“Mamama”
Nilimuita mama huku nikimtazama jinsi anavyo hema kwa nguvu akipigania pumzi yake. Manesi kwa haraka wakamshika na kuarudisha chini.
“Erick ninakuomba unipe nafasi nimshuhulikee mama”
Daktari mkuu alizungumza kwa upole na sauti iliyo jaa hekima ndani yake. Nikafungua mlango na kutoka, nikamkuta baba akiwa amesimama huku akiwa ameegemea ukuta, walinzi wake wote wamezagaa katika hili eneo wakiwa makini sana na hata mtu aliye hitaji kupita katika hii kordo alizuiwa. Baba akanitazama kwa macho yaliyo jaa hasira, taratibu akanisogelea na kunikazia macho. Nikastukia akinipiga kofi zito la shavu lililo nifanya niweweseke, nikajikuta nikipandwa na hasira kali nilipo hakikisha kwamba nimesimama wima, nikamsogelea na kumsukuma kwa nguvu akaanguka chini jambo lililo wafanya walinzi wake kadhaa kunivamia na kunishika kwa nguvu huku wengine wakishuhulika na kunyanyua baba kutoka sehemu alipo angukia.
ITAENDELEA